< תהילים 109 >
למנצח לדוד מזמור אלהי תהלתי אל-תחרש | 1 |
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Mungu, ambaye ninakusifu, usiwe kimya,
כי פי רשע ופי-מרמה--עלי פתחו דברו אתי לשון שקר | 2 |
kwa maana watu waovu na wadanganyifu wamefungua vinywa vyao dhidi yangu; wasema dhidi yangu kwa ndimi za udanganyifu.
ודברי שנאה סבבוני וילחמוני חנם | 3 |
Wamenizunguka kwa maneno ya chuki, wananishambulia bila sababu.
תחת-אהבתי ישטנוני ואני תפלה | 4 |
Wanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki, lakini mimi ninawaombea.
וישימו עלי רעה תחת טובה ושנאה תחת אהבתי | 5 |
Wananilipiza mabaya kwa mema, chuki badala ya urafiki wangu.
הפקד עליו רשע ושטן יעמד על-ימינו | 6 |
Agiza mtu mwovu ampinge, mshtaki asimame mkono wake wa kuume.
בהשפטו יצא רשע ותפלתו תהיה לחטאה | 7 |
Anapohukumiwa, apatikane na hatia, nayo maombi yake yamhukumu.
יהיו-ימיו מעטים פקדתו יקח אחר | 8 |
Siku zake za kuishi na ziwe chache, nafasi yake ya uongozi ichukuliwe na mtu mwingine.
יהיו-בניו יתומים ואשתו אלמנה | 9 |
Watoto wake na waachwe yatima, mke wake na awe mjane.
ונוע ינועו בניו ושאלו ודרשו מחרבותיהם | 10 |
Watoto wake na watangetange wakiomba, na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao.
ינקש נושה לכל-אשר-לו ויבזו זרים יגיעו | 11 |
Mtu anayemdai na ateke vyote alivyo navyo, matunda ya kazi yake yatekwe nyara na wageni.
אל-יהי-לו משך חסד ואל-יהי חונן ליתומיו | 12 |
Asiwepo mtu yeyote wa kumtendea mema wala wa kuwahurumia yatima wake.
יהי-אחריתו להכרית בדור אחר ימח שמם | 13 |
Uzao wake na ukatiliwe mbali, majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho.
יזכר עון אבתיו--אל-יהוה וחטאת אמו אל-תמח | 14 |
Maovu ya baba zake na yakumbukwe mbele za Bwana, dhambi ya mama yake isifutwe kamwe.
יהיו נגד-יהוה תמיד ויכרת מארץ זכרם | 15 |
Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana, ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani.
יען-- אשר לא זכר עשות חסד וירדף איש-עני ואביון--ונכאה לבב למותת | 16 |
Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema, bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo.
ויאהב קללה ותבואהו ולא-חפץ בברכה ותרחק ממנו | 17 |
Alipenda kulaani, nayo laana ikampata; hakupenda kubariki, kwa hiyo baraka na ikae mbali naye.
וילבש קללה כמדו ותבא כמים בקרבו וכשמן בעצמותיו | 18 |
Alivaa kulaani kama vazi lake, nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji, kwenye mifupa yake kama mafuta.
תהי-לו כבגד יעטה ולמזח תמיד יחגרה | 19 |
Na iwe kama joho alilozungushiwa, kama mshipi aliofungiwa daima.
זאת פעלת שטני מאת יהוה והדברים רע על-נפשי | 20 |
Haya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu, kwa wale wanaoninenea mabaya.
ואתה יהוה אדני-- עשה-אתי למען שמך כי-טוב חסדך הצילני | 21 |
Lakini wewe, Ee Bwana Mwenyezi, unitendee wema kwa ajili ya jina lako, uniokoe kwa wema wa pendo lako.
כי-עני ואביון אנכי ולבי חלל בקרבי | 22 |
Maana mimi ni maskini na mhitaji, moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.
כצל-כנטותו נהלכתי ננערתי כארבה | 23 |
Ninafifia kama kivuli cha jioni, nimerushwa-rushwa kama nzige.
ברכי כשלו מצום ובשרי כחש משמן | 24 |
Magoti yangu yamelegea kwa kufunga, mwili wangu umedhoofika na kukonda.
ואני הייתי חרפה להם יראוני יניעון ראשם | 25 |
Nimekuwa kitu cha kudharauliwa kwa washtaki wangu, wanionapo, hutikisa vichwa vyao.
עזרני יהוה אלהי הושיעני כחסדך | 26 |
Ee Bwana, Mungu wangu nisaidie, niokoe sawasawa na upendo wako.
וידעו כי-ידך זאת אתה יהוה עשיתה | 27 |
Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako, kwamba wewe, Ee Bwana, umetenda hili.
יקללו-המה ואתה תברך קמו ויבשו--ועבדך ישמח | 28 |
Wanaweza kulaani, lakini wewe utabariki, watakaposhambulia wataaibishwa, lakini mtumishi wako atashangilia.
ילבשו שוטני כלמה ויעטו כמעיל בשתם | 29 |
Washtaki wangu watavikwa fedheha, na kufunikwa na aibu kama joho.
אודה יהוה מאד בפי ובתוך רבים אהללנו | 30 |
Kwa kinywa changu nitamtukuza sana Bwana, katika umati mkubwa nitamsifu.
כי-יעמד לימין אביון-- להושיע משפטי נפשו | 31 |
Kwa maana husimama mkono wa kuume wa mhitaji, kuokoa maisha yake kutoka kwa wale wanaomhukumu.