< תהילים 106 >
הללו-יה הודו ליהוה כי-טוב-- כי לעולם חסדו | 1 |
Msifuni Bwana. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.
מי--ימלל גבורות יהוה ישמיע כל-תהלתו | 2 |
Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya Bwana au kutangaza kikamilifu sifa zake?
אשרי שמרי משפט עשה צדקה בכל-עת | 3 |
Heri wale wanaodumisha haki, ambao daima wanafanya yaliyo mema.
זכרני יהוה ברצון עמך פקדני בישועתך | 4 |
Ee Bwana, unikumbuke unapowatendea mema watu wako, uwe msaada wangu unapowaokoa,
לראות בטובת בחיריך-- לשמח בשמחת גויך להתהלל עם-נחלתך | 5 |
ili niweze kufurahia mafanikio ya wateule wako, niweze kushiriki katika furaha ya taifa lako, na kuungana na urithi wako katika kukusifu.
חטאנו עם-אבותינו העוינו הרשענו | 6 |
Tumetenda dhambi, kama vile baba zetu walivyotenda, tumekosa na tumetenda uovu.
אבותינו במצרים לא-השכילו נפלאותיך-- לא זכרו את-רב חסדיך וימרו על-ים בים-סוף | 7 |
Wakati baba zetu walipokuwa Misri, hawakuzingatia maajabu yako, wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu.
ויושיעם למען שמו-- להודיע את-גבורתו | 8 |
Hata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake, ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu.
ויגער בים-סוף ויחרב ויוליכם בתהמות כמדבר | 9 |
Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka, akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani.
ויושיעם מיד שונא ויגאלם מיד אויב | 10 |
Aliwaokoa mikononi mwa adui; kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa.
ויכסו-מים צריהם אחד מהם לא נותר | 11 |
Maji yaliwafunika adui zao, hakunusurika hata mmoja.
ויאמינו בדבריו ישירו תהלתו | 12 |
Ndipo walipoamini ahadi zake, nao wakaimba sifa zake.
מהרו שכחו מעשיו לא-חכו לעצתו | 13 |
Lakini mara walisahau aliyowatendea, wala hawakungojea shauri lake.
ויתאוו תאוה במדבר וינסו-אל בישימון | 14 |
Jangwani walitawaliwa na tamaa zao, walimjaribu Mungu nyikani.
ויתן להם שאלתם וישלח רזון בנפשם | 15 |
Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba, lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha.
ויקנאו למשה במחנה לאהרן קדוש יהוה | 16 |
Kambini walimwonea wivu Mose, na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana.
תפתח-ארץ ותבלע דתן ותכס על-עדת אבירם | 17 |
Ardhi ilifunguka ikawameza Dathani, ikawazika Abiramu na kundi lake.
ותבער-אש בעדתם להבה תלהט רשעים | 18 |
Moto uliwaka katikati ya wafuasi wao, mwali wa moto uliwateketeza waovu.
יעשו-עגל בחרב וישתחוו למסכה | 19 |
Huko Horebu walitengeneza ndama, na kuabudu sanamu ya kusubu kwa chuma.
וימירו את-כבודם בתבנית שור אכל עשב | 20 |
Waliubadilisha Utukufu wao kwa sanamu ya fahali, ambaye hula majani.
שכחו אל מושיעם-- עשה גדלות במצרים | 21 |
Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri,
נפלאות בארץ חם נוראות על-ים-סוף | 22 |
miujiza katika nchi ya Hamu na mambo ya kutisha huko Bahari ya Shamu.
ויאמר להשמידם לולי משה בחירו-- עמד בפרץ לפניו להשיב חמתו מהשחית | 23 |
Kwa hiyo alisema kwamba angewaangamiza: kama Mose mteule wake, asingesimama kati yao na Mungu kuizuia ghadhabu yake kuwaangamiza.
וימאסו בארץ חמדה לא-האמינו לדברו | 24 |
Kisha waliidharau ile nchi nzuri, hawakuiamini ahadi yake.
וירגנו באהליהם לא שמעו בקול יהוה | 25 |
Walinungʼunika ndani ya mahema yao, wala hawakumtii Bwana.
וישא ידו להם-- להפיל אותם במדבר | 26 |
Kwa hiyo akaapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba atawafanya waanguke jangwani,
ולהפיל זרעם בגוים ולזרותם בארצות | 27 |
kuwatawanya wazao wao waanguke miongoni mwa mataifa, na kuwatawanya katika nchi zote.
ויצמדו לבעל פעור ויאכלו זבחי מתים | 28 |
Walijifunga nira na Baali wa Peori, wakala dhabihu zilizotolewa kwa miungu isiyo na uhai.
ויכעיסו במעלליהם ותפרץ-בם מגפה | 29 |
Waliichochea hasira ya Bwana, wakamkasirisha kwa matendo yao maovu, nayo tauni ikazuka katikati yao.
ויעמד פינחס ויפלל ותעצר המגפה | 30 |
Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati, nayo tauni ikazuiliwa.
ותחשב לו לצדקה לדר ודר עד-עולם | 31 |
Hili likahesabiwa kwake haki, kwa vizazi visivyo na mwisho vijavyo.
ויקציפו על-מי מריבה וירע למשה בעבורם | 32 |
Kwenye maji ya Meriba, walimkasirisha Bwana, janga likampata Mose kwa sababu yao;
כי-המרו את-רוחו ויבטא בשפתיו | 33 |
kwa maana walimwasi Roho wa Mungu, na maneno yasiyofaa yakatoka midomoni kwa Mose.
לא-השמידו את-העמים-- אשר אמר יהוה להם | 34 |
Hawakuyaangamiza yale mataifa kama Bwana alivyowaagiza,
ויתערבו בגוים וילמדו מעשיהם | 35 |
bali walijichanganya na mataifa na wakazikubali desturi zao.
ויעבדו את-עצביהם ויהיו להם למוקש | 36 |
Waliabudu sanamu zao, zikawa mtego kwao.
ויזבחו את-בניהם ואת-בנותיהם-- לשדים | 37 |
Wakawatoa wana wao na binti zao dhabihu kwa mashetani.
וישפכו דם נקי דם-בניהם ובנותיהם-- אשר זבחו לעצבי כנען ותחנף הארץ בדמים | 38 |
Walimwaga damu isiyo na hatia, damu za wana wao na binti zao, ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani, nayo nchi ikanajisika kwa damu zao.
ויטמאו במעשיהם ויזנו במעלליהם | 39 |
Wakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda; kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba.
ויחר-אף יהוה בעמו ויתעב את-נחלתו | 40 |
Kwa hiyo Bwana akawakasirikia watu wake na akauchukia sana urithi wake.
ויתנם ביד-גוים וימשלו בהם שנאיהם | 41 |
Akawakabidhi kwa mataifa na adui zao wakawatawala.
וילחצום אויביהם ויכנעו תחת ידם | 42 |
Adui zao wakawaonea na kuwatia chini ya mamlaka yao.
פעמים רבות יצילם והמה ימרו בעצתם וימכו בעונם | 43 |
Mara nyingi aliwaokoa lakini walikuwa wamezama kwenye uasi, nao wakajiharibu katika dhambi zao.
וירא בצר להם-- בשמעו את-רנתם | 44 |
Lakini akaangalia mateso yao wakati aliposikia kilio chao;
ויזכר להם בריתו וינחם כרב חסדו | 45 |
kwa ajili yao akakumbuka agano lake, na kutokana na upendo wake mkuu akapooza hasira yake.
ויתן אותם לרחמים-- לפני כל-שוביהם | 46 |
Akawafanya wahurumiwe na wote waliowashikilia mateka.
הושיענו יהוה אלהינו וקבצנו מן-הגוים להדות לשם קדשך להשתבח בתהלתך | 47 |
Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe. Tukusanye tena kutoka kwa mataifa, ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, na kushangilia katika sifa zako.
ברוך יהוה אלהי ישראל מן-העולם ועד העולם-- ואמר כל-העם אמן הללו-יה | 48 |
Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Watu wote na waseme, “Amen!” Msifuni Bwana.