< תהילים 10 >

למה יהוה תעמד ברחוק תעלים לעתות בצרה 1
Kwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali? Kwa nini unajificha wakati wa shida?
בגאות רשע ידלק עני יתפשו במזמות זו חשבו 2
Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.
כי-הלל רשע על-תאות נפשו ובצע ברך נאץ יהוה 3
Hujivunia tamaa za moyo wake; humbariki mlafi na kumtukana Bwana.
רשע--כגבה אפו בל-ידרש אין אלהים כל-מזמותיו 4
Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu, katika mawazo yake yote hakuna nafasi ya Mungu.
יחילו דרכו בכל-עת--מרום משפטיך מנגדו כל-צורריו יפיח בהם 5
Njia zake daima hufanikiwa; hujivuna na amri zako ziko mbali naye, huwacheka kwa dharau adui zake wote.
אמר בלבו בל-אמוט לדר ודר אשר לא-ברע 6
Anajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa, daima nitakuwa na furaha, kamwe sitakuwa na shida.”
אלה פיהו מלא--ומרמות ותך תחת לשונו עמל ואון 7
Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho; shida na ubaya viko chini ya ulimi wake.
ישב במארב חצרים--במסתרים יהרג נקי עיניו לחלכה יצפנו 8
Huvizia karibu na vijiji; kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia, akivizia wapitaji.
יארב במסתר כאריה בסכה-- יארב לחטוף עני יחטף עני במשכו ברשתו 9
Huvizia kama simba aliye mawindoni; huvizia kumkamata mnyonge, huwakamata wanyonge na kuwaburuza katika wavu wake.
ודכה (ידכה) ישח ונפל בעצומיו חלכאים (חל כאים) 10
Mateka wake hupondwa, huzimia; wanaanguka katika nguvu zake.
אמר בלבו שכח אל הסתיר פניו בל-ראה לנצח 11
Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau, huficha uso wake na haoni kabisa.”
קומה יהוה--אל נשא ידך אל-תשכח עניים (ענוים) 12
Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu. Usiwasahau wanyonge.
על-מה נאץ רשע אלהים אמר בלבו לא תדרש 13
Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu? Kwa nini anajiambia mwenyewe, “Hataniita nitoe hesabu?”
ראתה כי-אתה עמל וכעס תביט-- לתת בידך עליך יעזב חלכה יתום אתה היית עוזר 14
Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, umekubali kuyapokea mkononi mwako. Mhanga anajisalimisha kwako, wewe ni msaada wa yatima.
שבר זרוע רשע ורע תדרוש-רשעו בל-תמצא 15
Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya, mwite atoe hesabu ya maovu yake ambayo yasingejulikana.
יהוה מלך עולם ועד אבדו גוים מארצו 16
Bwana ni Mfalme milele na milele, mataifa wataangamia watoke nchini mwake.
תאות ענוים שמעת יהוה תכין לבם תקשיב אזנך 17
Unasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa, wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao,
לשפט יתום ודך בל-יוסיף עוד--לערץ אנוש מן-הארץ 18
ukiwatetea yatima na walioonewa, ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena.

< תהילים 10 >