< מִשְׁלֵי 30 >
דברי אגור בן-יקה--המשא נאם הגבר לאיתיאל לאיתיאל ואכל | 1 |
Maneno ya Aguri mwana wa Yake - mausia: Mtu huyu alimwambia Ithieli, kwa Ithiel na Ukali:
כי בער אנכי מאיש ולא-בינת אדם לי | 2 |
Hakika nipo kama mnyama kuliko mwanadamu na sina ufahamu wa wanadamu.
ולא-למדתי חכמה ודעת קדשים אדע | 3 |
Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya Mtakatifu.
מי עלה-שמים וירד מי אסף-רוח בחפניו מי צרר-מים בשמלה-- מי הקים כל-אפסי-ארץ מה-שמו ומה-שם-בנו כי תדע | 4 |
Je ni nani amekwenda juu mbinguni na kurudi chini? Je ni nani aliyekusanya upepo kwenye mikono yake? Je ni nani aliyekusanya maji kwenye kanzu? Je ni nani aliyeziimarisha ncha za dunia yote? Jina lake ni nani, na jina la mtoto wake ni nani? Hakika unajua!
כל-אמרת אלוה צרופה מגן הוא לחסים בו | 5 |
Kila neno la Mungu limejaribiwa, yeye ni ngao kwa wale wanaokimbilia kwake.
אל-תוסף על-דבריו פן-יוכיח בך ונכזבת | 6 |
Usiyaongezee maneno haya, au atakukemea, na utathibitishwa kuwa mwongo.
שתים שאלתי מאתך אל-תמנע ממני בטרם אמות | 7 |
Vitu viwili ninakuomba, usivikatalie kwangu kabla sijafa:
שוא ודבר-כזב הרחק ממני-- ראש ועשר אל-תתן-לי הטריפני לחם חקי | 8 |
Majivuno na uongo viweke mbali nami. Usinipe umasikini wala utajiri, nipe tu chakula ninachohitaji.
פן אשבע וכחשתי-- ואמרתי מי יהוה ופן-אורש וגנבתי ותפשתי שם אלהי | 9 |
Maana nikipata vingi zaidi, nitakukana wewe na kusema, “Yehova ni nani?” Au kama nitakuwa masikini, nitaiba na kukufuru jina la Mungu wangu.
אל-תלשן עבד אל-אדנו פן-יקללך ואשמת | 10 |
Usimkashifu mtumwa mbele ya bwana wake, au atakulaani na utapata hatia.
דור אביו יקלל ואת-אמו לא יברך | 11 |
Kizazi ambacho kinachomlaa baba yao na hakimbariki mama yao,
דור טהור בעיניו ומצאתו לא רחץ | 12 |
kizazi hicho ni safi katika macho yao wenyewe, lakini hawajaoshwa uchafu wao.
דור מה-רמו עיניו ועפעפיו ינשאו | 13 |
Hicho ni kizazi- jinsi gani macho yao yanakiburi na kope zao zimeinuka juu! -
דור חרבות שניו-- ומאכלות מתלעתיו לאכל עניים מארץ ואביונים מאדם | 14 |
kuna kizazi ambacho meno yao ni upanga, na mifupa ya taya zao ni visu, ili waweze kumrarua masikini wamtoe duniani na mhitaji atoke miongoni mwa wanadamu.
לעלוקה שתי בנות-- הב הב שלוש הנה לא תשבענה ארבע לא-אמרו הון | 15 |
Ruba anamabinti wawili, “Toa na Toa” wanalia. Kuna vitu vitatu ambavyo havitosheki, vinne ambavyo havisememi, “Inatosha”:
שאול ועצר-רחם ארץ לא-שבעה מים ואש לא-אמרה הון (Sheol ) | 16 |
Kuzimu, tumbo tasa, nchi yenye kiu kwa maji, na moto usiosema, “Inatosha.” (Sheol )
עין תלעג לאב-- ותבז ליקהת-אם יקרוה ערבי-נחל ויאכלוה בני-נשר | 17 |
Jicho ambalo linamdhihaki baba na kudharau utii kwa mama, macho yake yatadonolewa na kunguru wa bondeni, na ataliwa na tai.
שלשה המה נפלאו ממני וארבע (וארבעה) לא ידעתים | 18 |
Kuna vitu vitatu ambavyo vinanishangaza, vinne ambavyo sivifahamu:
דרך הנשר בשמים-- דרך נחש עלי-צור דרך-אניה בלב-ים-- ודרך גבר בעלמה | 19 |
njia ya tai angani; njia ya nyoka juu ya mwamba; njia ya meli kwenye moyo wa bahari; na njia ya mtu pamoja mwanake kijana.
כן דרך אשה-- מנאפת אכלה ומחתה פיה ואמרה לא-פעלתי און | 20 |
Hii ni njia ya mzinzi- anakula na kufuta kinywa chake na kusema, “sijafanya ubaya wowote.”
תחת שלוש רגזה ארץ ותחת ארבע לא-תוכל שאת | 21 |
Chini ya vitu vitatu dunia hutetemeka na vinne haiwezi kuvivumilia:
תחת-עבד כי ימלוך ונבל כי ישבע-לחם | 22 |
mtumwa anapokuwa mfalme; mpumbavu anaposhiba vyakula;
תחת שנואה כי תבעל ושפחה כי תירש גברתה | 23 |
mwanamke anayechukiwa anapoolewa; kijakazi anapochukua nafasi ya mkuu wake.
ארבעה הם קטני-ארץ והמה חכמים מחכמים | 24 |
Vitu vinne duniani ni vidogo na bado vinabusara:
הנמלים עם לא-עז ויכינו בקיץ לחמם | 25 |
mchwa ni viumbe ambao sio imara, lakini huandaa chakula chao wakati wa hari,
שפנים עם לא-עצום וישימו בסלע ביתם | 26 |
Wibari siyo viumbe wenye nguvu, lakini hutengeneza makazi yake kwenye miamba.
מלך אין לארבה ויצא חצץ כלו | 27 |
Nzige hawana mfalme, lakini wote wanamwendo wa mpangilio.
שממית בידים תתפש והיא בהיכלי מלך | 28 |
Kama mjusi, unaweza kumkunja kwa mikono yako miwili, lakini wanapatikana katika majumba ya wafalme.
שלשה המה מיטיבי צעד וארבעה מיטבי לכת | 29 |
Kuna vitu vitatu ambavyo ni fahari katika mwendo na vinne ambavyo ni fahari katika namna ya kutembea:
ליש גבור בבהמה ולא-ישוב מפני-כל | 30 |
simba, aliyeimara miongoni mwa wanyama- wala hajiepushi na kitu chochote;
זרזיר מתנים או-תיש ומלך אלקום עמו | 31 |
jogoo anayetembea kwa mikogo; mbuzi; na mfalme ambaye askari wapo kando yake.
אם-נבלת בהתנשא ואם-זמות יד לפה | 32 |
Kama umekuwa mpumbavu, jitukuze mwenyewe, au kama umekuwa ukisimamia vibaya- weka mkono wako juu ya kinywa chako.
כי מיץ חלב יוציא חמאה-- ומיץ-אף יוציא דם ומיץ אפים יוציא ריב | 33 |
Kama kusuka maziwa hufanya siagi na pua ya mtu hutoa damu kama imepigwa, basi matendo yanayofanywa kwa hasira huzalisha mafarakano.