< מִשְׁלֵי 29 >

איש תוכחות מקשה-ערף-- פתע ישבר ואין מרפא 1
Mtu aliyepokea makaripio mengi lakini anashupaza shingo yake atavunjika ndani ya muda mfupi na hata pona.
ברבות צדיקים ישמח העם ובמשל רשע יאנח עם 2
Watenda mema wanapoongezeka, watu wanafurahi, bali wakati mtu mwovu anapotawala, watu huugua.
איש-אהב חכמה ישמח אביו ורעה זונות יאבד-הון 3
Mwenye kupenda hekima baba yake anafurahi, bali anayeshikamana na makahaba huuharibu utajiri wake.
מלך--במשפט יעמיד ארץ ואיש תרומות יהרסנה 4
Mfalme huimarisha nchi kwa haki, bali mwenye kudai rushwa huirarua.
גבר מחליק על-רעהו רשת פורש על-פעמיו 5
Mtu anayejipendekeza kwa jirani yake anatandaza wavu kwenye miguu yake.
בפשע איש רע מוקש וצדיק ירון ושמח 6
Mtu mbaya hunaswa kwenye mtego wa dhambi yake mwenyewe, bali yeye atendaye haki huimba na kufurahi.
ידע צדיק דין דלים רשע לא-יבין דעת 7
Atendaye haki hutetea madai ya masikini; mtu mwovu hafahamu maarifa kama hayo.
אנשי לצון יפיחו קריה וחכמים ישיבו אף 8
Mwenye dhihaka huutia moto mji, bali wale wenye busara huigeuza ghadhabu.
איש-חכם--נשפט את-איש אויל ורגז ושחק ואין נחת 9
Mtu mwenye busara anapojadiliana na mpumbavu, hughadhabika na kucheka, hakutakuwa na utulivu.
אנשי דמים ישנאו-תם וישרים יבקשו נפשו 10
Mkatili humchukia mwenye ukamilifu na hutafuta maisha ya mwenye haki.
כל-רוחו יוציא כסיל וחכם באחור ישבחנה 11
Mpumabavu huonyesha hasira yake, bali mtu mwenye busara huishikilia na kujituliza mwenyewe.
משל מקשיב על-דבר-שקר-- כל-משרתיו רשעים 12
Kama matawala atazinagatia uongo, maafisa wake wote watakuwa waovu.
רש ואיש תככים נפגשו-- מאיר עיני שניהם יהוה 13
Mtu masikini na mkandamizaji wanafanana, maana Yehova huyapa nuru macho yao wote.
מלך שופט באמת דלים-- כסאו לעד יכון 14
Kama mfalme atamhukumu masikini kwa uaminifu, kiti chake cha enzi kitaimarishwa milele.
שבט ותוכחת יתן חכמה ונער משלח מביש אמו 15
Fimbo na maonyo huleta hekima, bali mtoto huru mbali na makaripio humwaibisha mama yake.
ברבות רשעים ירבה-פשע וצדיקים במפלתם יראו 16
Watu waovu wanapotawala, uovu huongezeka, bali wenye kutenda haki wataona anguko la watu waovu.
יסר בנך ויניחך ויתן מעדנים לנפשך 17
Mwadibishe mwanao naye atakupa pumziko; ataleta furaha katika maisha yako.
באין חזון יפרע עם ושמר תורה אשרהו 18
Pasipo na maono ya kinabii watu huenda bila utaratibu, bali mwenye kuitunza sheria amebarikiwa.
בדברים לא-יוסר עבד כי-יבין ואין מענה 19
Mtumwa hawezi kurekebishwa kwa maneno, maana ingawa anaelewa, hakuna mwitikio.
חזית--איש אץ בדבריו תקוה לכסיל ממנו 20
Je unamwona mtu mwenye haraka katika maneno yake? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.
מפנק מנער עבדו ואחריתו יהיה מנון 21
Mwenye kumdekeza mtumwa wake tangu ujana, mwisho wake itakuwa taabu.
איש-אף יגרה מדון ובעל חמה רב-פשע 22
Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi na bwana mwenye hasira sana hutenda dhambi nyingi.
גאות אדם תשפילנו ושפל-רוח יתמך כבוד 23
Kiburi cha mtu humshusha chini, bali mwenye roho ya unyenyekevu atapewa heshima.
חולק עם-גנב שונא נפשו אלה ישמע ולא יגיד 24
Anayeshirikiana na mwizi huyachukia maisha yake mwenyewe; husikia laana na wala hasemi chochote.
חרדת אדם יתן מוקש ובוטח ביהוה ישגב 25
Kumwogopa binadamu ni mtego, bali mwenye kumtumaini Yehova atalindwa.
רבים מבקשים פני-מושל ומיהוה משפט-איש 26
Wengi huutafuta uso wa mtawala, bali kutoka kwa Yehova huja haki kwa ajili yake.
תועבת צדיקים איש עול ותועבת רשע ישר-דרך 27
Mtu dhalimu ni chukizo kwa wenye kutenda haki, bali mwenye njia ya haki ni chukizo kwa watu waovu.

< מִשְׁלֵי 29 >