< מִשְׁלֵי 18 >
לתאוה יבקש נפרד בכל-תושיה יתגלע | 1 |
Yule ambaye hujitenga hutafuta matakwa yake mwenyewe na hupingana na hukumu zote za kweli.
לא-יחפץ כסיל בתבונה כי אם-בהתגלות לבו | 2 |
Mpumbavu hapati raha katika ufahamu, lakini hufunua kile kilichopo katika moyo wake.
בבוא-רשע בא גם-בוז ועם-קלון חרפה | 3 |
Mtu mwovu anapokuja, dharau huja pamoja naye- sambamba na aibu na shutuma.
מים עמקים דברי פי-איש נחל נבע מקור חכמה | 4 |
Maneno ya kinywa cha mtu ni maji yenye kina kirefu; chemchemi ya hekima ni mkondo unaotiririka.
שאת פני-רשע לא-טוב-- להטות צדיק במשפט | 5 |
Si vema kuwa na upendeleo kwa mwovu, wala haifai kukana haki kwa wale watendao mema.
שפתי כסיל יבאו בריב ופיו למהלמות יקרא | 6 |
Midomo ya mpumbavu huletea mafarakano na kinywa chake hukaribisha mapigo.
פי-כסיל מחתה-לו ושפתיו מוקש נפשו | 7 |
Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na hujinasa mwenye kwa midomo yake.
דברי נרגן כמתלהמים והם ירדו חדרי-בטן | 8 |
Maneno ya mmbea ni kama chembe tamu na hushuka katika sehema za ndani sana kwenye mwili.
גם מתרפה במלאכתו-- אח הוא לבעל משחית | 9 |
Basi, ambaye ni mzembe katika kazi yake ni ndugu yake anayeharibu wengi.
מגדל-עז שם יהוה בו-ירוץ צדיק ונשגב | 10 |
Jina la Yehova ni mnara imara; atendaye haki hukimbilia na kuwa salama.
הון עשיר קרית עזו וכחומה נשגבה במשכתו | 11 |
Mali ya tajiri ni mji wake imara na katika fikira zake ni kama ukuta mrefu.
לפני-שבר יגבה לב-איש ולפני כבוד ענוה | 12 |
Moyo wa mtu huwa na kiburi kabla ya anguko lake, bali unyenyekevu hutangulia kabla ya heshima.
משיב דבר בטרם ישמע-- אולת היא-לו וכלמה | 13 |
Anayejibu kabla ya kusikiliza- ni upuuzi na aibu yake.
רוח-איש יכלכל מחלהו ורוח נכאה מי ישאנה | 14 |
Roho ya mtu itajinusuru na madhara, bali roho iliyopondeka nani anaweza kuivumilia?
לב נבון יקנה-דעת ואזן חכמים תבקש-דעת | 15 |
Moyo wa mwenye akili hujipatia maarifa na usikivu wa mwenye busara huitafuta.
מתן אדם ירחיב לו ולפני גדלים ינחנו | 16 |
Zawadi ya mtu inaweza kufungua njia na kumleta mbele ya mtu muhimu.
צדיק הראשון בריבו יבא- (ובא-) רעהו וחקרו | 17 |
Wa kwanza kujitetea katika shitaka lake huonekana kuwa na haki hadi mpinzani wake aje na kumuuliza maswali.
מדינים ישבית הגורל ובין עצומים יפריד | 18 |
Kupiga kura kunamaliza mabishano na kuwatawanya wapinzani imara.
אח--נפשע מקרית-עז ומדונים (ומדינים) כבריח ארמון | 19 |
Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kushawishiwa kuliko mji wenye nguvu, na kugombana ni kama makomeo ya ngome.
מפרי פי-איש תשבע בטנו תבואת שפתיו ישבע | 20 |
Tumbo la mtu litashiba kutoka kwenye tunda la kinywa chake; atatoshelezwa kwa mavuno ya midomo yake.
מות וחיים ביד-לשון ואהביה יאכל פריה | 21 |
Uzima na kifo hutawaliwa kwa ulimi, na wale wenye kuupenda ulimi watakula tunda lake.
מצא אשה מצא טוב ויפק רצון מיהוה | 22 |
Yeye apataye mke anapata kitu chema na kupokea fadhila kutoka kwa Yehova.
תחנונים ידבר-רש ועשיר יענה עזות | 23 |
Mtu masikini huomba rehema, lakini mtu tajiri hujibu kwa ukali.
איש רעים להתרעע ויש אהב דבק מאח | 24 |
Anayejidai kwa marafiki wengi watamleta katika uharibifu, bali yupo rafiki ambaye huwa karibu kuliko ndugu.