< מִשְׁלֵי 17 >

טוב פת חרבה ושלוה-בה-- מבית מלא זבחי-ריב 1
Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi.
עבד-משכיל--ימשל בבן מביש ובתוך אחים יחלק נחלה 2
Mtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye, naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu.
מצרף לכסף וכור לזהב ובחן לבות יהוה 3
Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu, bali Bwana huujaribu moyo.
מרע מקשיב על-שפת-און שקר מזין על-לשון הות 4
Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya; mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara.
לעג לרש חרף עשהו שמח לאיד לא ינקה 5
Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake; yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa.
עטרת זקנים בני בנים ותפארת בנים אבותם 6
Wana wa wana ni taji la wazee, nao wazazi ni fahari ya watoto wao.
לא-נאוה לנבל שפת-יתר אף כי-לנדיב שפת-שקר 7
Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu: je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala!
אבן-חן השחד בעיני בעליו אל-כל-אשר יפנה ישכיל 8
Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; kokote kigeukiapo, hufanikiwa.
מכסה-פשע מבקש אהבה ושנה בדבר מפריד אלוף 9
Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo, bali yeyote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu.
תחת גערה במבין-- מהכות כסיל מאה 10
Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua kuliko mapigo mia kwa mpumbavu.
אך-מרי יבקש-רע ומלאך אכזרי ישלח-בו 11
Mtu mbaya hupenda kuasi tu; mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake.
פגוש דב שכול באיש ואל-כסיל באולתו 12
Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyangʼanywa watoto wake, kuliko mpumbavu katika upumbavu wake.
משיב רעה תחת טובה-- לא-תמיש (תמוש) רעה מביתו 13
Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema, kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake.
פוטר מים ראשית מדון ולפני התגלע הריב נטוש 14
Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji; kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza.
מצדיק רשע ומרשיע צדיק-- תועבת יהוה גם-שניהם 15
Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki, naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki: Bwana huwachukia sana wote wawili.
למה-זה מחיר ביד-כסיל-- לקנות חכמה ולב-אין 16
Fedha ina faida gani mikononi mwa mpumbavu, wakati yeye hana haja ya kupata hekima?
בכל-עת אהב הרע ואח לצרה יולד 17
Rafiki hupenda wakati wote naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.
אדם חסר-לב תוקע כף ערב ערבה לפני רעהו 18
Mtu mjinga hupana mkono ili kuweka rehani, naye huweka dhamana kwa jirani yake.
אהב פשע אהב מצה מגביה פתחו מבקש-שבר 19
Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi; naye ainuaye sana lango lake hutafuta uharibifu.
עקש-לב לא ימצא-טוב ונהפך בלשונו יפול ברעה 20
Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa; naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu.
ילד כסיל לתוגה לו ולא-ישמח אבי נבל 21
Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni; hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu.
לב שמח ייטיב גהה ורוח נכאה תיבש-גרם 22
Moyo wenye furaha ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.
שחד מחק רשע יקח-- להטות ארחות משפט 23
Mtu mwovu hukubali rushwa kwa siri ili kupotosha njia ya haki.
את-פני מבין חכמה ועיני כסיל בקצה-ארץ 24
Mtu wa ufahamu huitazama hekima, lakini macho ya mpumbavu huhangaika hadi kwenye miisho ya dunia.
כעס לאביו בן כסיל וממר ליולדתו 25
Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake na uchungu kwa yeye aliyemzaa.
גם ענוש לצדיק לא-טוב-- להכות נדיבים על-ישר 26
Si vizuri kumwadhibu mtu asiye na hatia, au kuwapiga sana maafisa kwa ajili ya uadilifu wao.
חושך אמריו יודע דעת וקר- (יקר-) רוח איש תבונה 27
Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia, naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu.
גם אויל מחריש חכם יחשב אטם שפתיו נבון 28
Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima kama akinyamaza, na mwenye ufahamu kama akiuzuia ulimi wake.

< מִשְׁלֵי 17 >