< מִשְׁלֵי 11 >
מאזני מרמה תועבת יהוה ואבן שלמה רצונו | 1 |
Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu, bali vipimo sahihi ni furaha yake.
בא-זדון ויבא קלון ואת-צנועים חכמה | 2 |
Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima.
תמת ישרים תנחם וסלף בגדים ושדם (ישדם) | 3 |
Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.
לא-יועיל הון ביום עברה וצדקה תציל ממות | 4 |
Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini.
צדקת תמים תישר דרכו וברשעתו יפל רשע | 5 |
Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka, bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe.
צדקת ישרים תצילם ובהות בגדים ילכדו | 6 |
Haki ya wanyofu huwaokoa, bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.
במות אדם רשע תאבד תקוה ותוחלת אונים אבדה | 7 |
Wakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka; yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu.
צדיק מצרה נחלץ ויבא רשע תחתיו | 8 |
Mtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu, naye mtu mwovu huingia humo badala yake.
בפה--חנף ישחת רעהו ובדעת צדיקים יחלצו | 9 |
Kwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu humwangamiza jirani yake, bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa.
בטוב צדיקים תעלץ קריה ובאבד רשעים רנה | 10 |
Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi; mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.
בברכת ישרים תרום קרת ובפי רשעים תהרס | 11 |
Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa, bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa.
בז-לרעהו חסר-לב ואיש תבונות יחריש | 12 |
Mtu asiye na akili humdharau jirani yake, bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake.
הולך רכיל מגלה-סוד ונאמן-רוח מכסה דבר | 13 |
Masengenyo husaliti tumaini, bali mtu mwaminifu hutunza siri.
באין תחבלות יפל-עם ותשועה ברב יועץ | 14 |
Pasipo ushauri wa hekima taifa huanguka, bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika.
רע-ירוע כי-ערב זר ושנא תקעים בוטח | 15 |
Yeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka, bali yeyote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama.
אשת-חן תתמך כבוד ועריצים יתמכו-עשר | 16 |
Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima, bali wanaume wakorofi hupata mali tu.
גמל נפשו איש חסד ועכר שארו אכזרי | 17 |
Mwenye huruma hujinufaisha mwenyewe, bali mkatili hujiletea taabu mwenyewe.
רשע--עשה פעלת-שקר וזרע צדקה שכר אמת | 18 |
Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu, bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.
כן-צדקה לחיים ומרדף רעה למותו | 19 |
Mtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima, bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake.
תועבת יהוה עקשי-לב ורצונו תמימי דרך | 20 |
Bwana huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu, bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.
יד ליד לא-ינקה רע וזרע צדיקים נמלט | 21 |
Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa, bali wenye haki watakuwa huru.
נזם זהב באף חזיר-- אשה יפה וסרת טעם | 22 |
Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe ndivyo alivyo mwanamke mzuri ambaye hana busara.
תאות צדיקים אך-טוב תקות רשעים עברה | 23 |
Shauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema, bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu.
יש מפזר ונוסף עוד וחשך מישר אך-למחסור | 24 |
Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi, mwingine huzuia, lakini huwa maskini.
נפש-ברכה תדשן ומרוה גם-הוא יורא | 25 |
Mtu mkarimu atastawi; yeye awaburudishaye wengine ataburudishwa mwenyewe.
מנע בר יקבהו לאום וברכה לראש משביר | 26 |
Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka, bali baraka itamkalia kichwani kama taji yeye aliye radhi kuiuza.
שחר טוב יבקש רצון ודרש רעה תבואנו | 27 |
Yeye atafutaye mema hupata ukarimu, bali ubaya huja kwake yeye autafutaye.
בוטח בעשרו הוא יפול וכעלה צדיקים יפרחו | 28 |
Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka, bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.
עכר ביתו ינחל-רוח ועבד אויל לחכם-לב | 29 |
Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo, naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima.
פרי-צדיק עץ חיים ולקח נפשות חכם | 30 |
Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima, naye mwenye hekima huvuta roho za watu.
הן צדיק בארץ ישלם אף כי-רשע וחוטא | 31 |
Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani, si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?