< במדבר 4 >

וידבר יהוה אל משה ואל אהרן לאמר 1
BWANA akanena na Musa na Haruni. Akasema,
נשא את ראש בני קהת מתוך בני לוי--למשפחתם לבית אבתם 2
Fanya sensa ya uzao waume wa Kohathi kutoka kwa Walawi, kwa kufuata jamaa na na familia za koo.
מבן שלשים שנה ומעלה ועד בן חמשים שנה--כל בא לצבא לעשות מלאכה באהל מועד 3
Uwahesabu wanaume ambao wana umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini. Hawa wataungana na kundi linalotumika kutoa huduma kwenye hema ya kukutania.
זאת עבדת בני קהת באהל מועד--קדש הקדשים 4
Uzao wa Kohathi watalinda vile vitu vitakatifu zaidi vilivyohifadhiwa kwa ajili yangu katika hema ya kukutania.
ובא אהרן ובניו בנסע המחנה והורדו את פרכת המסך וכסו בה--את ארן העדת 5
Wakati kambi inapojiandaa kusonga mbele, Haruni na wanawe lazima waende hemani, kulishusha pazia linalotenganisha mahali patakatifu na kulifunika sanduku la ushuhuda kwa pazia hilo. Watalifunika hilo sanduku kwa ngozi za pomboo.
ונתנו עליו כסוי עור תחש ופרשו בגד כליל תכלת מלמעלה ושמו בדיו 6
Watatandika juu yake nguo za rangi ya samawi. Watachomeka hiyo miti ya kubebea.
ועל שלחן הפנים יפרשו בגד תכלת ונתנו עליו את הקערת ואת הכפת ואת המנקית ואת קשות הנסך ולחם התמיד עליו יהיה 7
Watatandika nguo ya rangi ya samawi kwenye meza ya mikate ya wonyesho. Juu yake wataweka sahani, vijiko, mabakuli na vikombe vya kumiminia. Mikate itakuwepo daima mezani.
ופרשו עליהם בגד תולעת שני וכסו אתו במכסה עור תחש ושמו את בדיו 8
Wataifunika na nguo ya rangi nyekundu na ngozi za pomboo. na kuweka miti ya kubebea.
ולקחו בגד תכלת וכסו את מנרת המאור ואת נרתיה ואת מלקחיה ואת מחתתיה ואת כל כלי שמנה אשר ישרתו לה בהם 9
Watachukua nguo ya rangi ya samawi na kukifunika kinara, pamoja na taa zake, na koleo zake, na sahani zake na vikombe vyake vya kuwekea mafuta ya taa.
ונתנו אתה ואת כל כליה אל מכסה עור תחש ונתנו על המוט 10
Wataweka kinara na vifaa vyake vikiwa vimefunikwa na ngozi ya pomboo, na wataweka kwenye miti ya kukibebea.
ועל מזבח הזהב יפרשו בגד תכלת וכסו אתו במכסה עור תחש ושמו את בדיו 11
Watafunika na nguo ya samawi katika madhabau ya dhahabu. Wataifunika na ngozi za pomboo, na kuweka ile miti ya kubebea.
ולקחו את כל כלי השרת אשר ישרתו בם בקדש ונתנו אל בגד תכלת וכסו אותם במכסה עור תחש ונתנו על המוט 12
Watavichukua vyombo vyote vya kazi takatifu na kuvizonga kwenye hiyo nguo ya rangi ya samawi. Watavifunika na ngozi za pomboo na kuviweka hivyo vyombo kwenye miti ya kubebea.
ודשנו את המזבח ופרשו עליו בגד ארגמן 13
Watayaondoa majivu kwenye madhabahu na kutandika nguo ya rangi ya zambarau juu yake.
ונתנו עליו את כל כליו אשר ישרתו עליו בהם את המחתת את המזלגת ואת היעים ואת המזרקת--כל כלי המזבח ופרשו עליו כסוי עור תחש--ושמו בדיו 14
Watavieka kwenye miti ya kubebea vyombo vyote wanavyovitumia kwa kazi ya madhabahuni. Vyombo hivi ni vyetezo, majembe, mabakuli na vitu vingine vya madhabahuni. Wataifuniks madhabahu na ngozi za pomboo na kuweka ile miti ya kubebea.
וכלה אהרן ובניו לכסת את הקדש ואת כל כלי הקדש בנסע המחנה ואחרי כן יבאו בני קהת לשאת ולא יגעו אל הקדש ומתו אלה משא בני קהת באהל מועד 15
Wakati Haruni na wanawe walipokuwa wamekamilisha kupafunika mahali patakatifu na vyombo vyote, na kambi itakapoanza kuendelea mbele, ndipo wana wa Kohathi watakapokuja kubeba vitu vya mahali patakatifu. Kama watagusa vyombo vitakatifu, lazima watakufa. Hii ni kazi ya wana wa uzao wa Kohathi, kubeba mapambo ya hema ya kukutania.
ופקדת אלעזר בן אהרן הכהן שמן המאור וקטרת הסמים ומנחת התמיד ושמן המשחה פקדת כל המשכן וכל אשר בו בקדש ובכליו 16
Eliazari mwana wa Haruni kuhani atalinda na kusimamia mafuta ya taa, ubani mzuri, sadaka za mara kwa mara na mafuta ya upako. Atasimamia ulinzi wa hema lote na vyote vilivyomo, mahali patakatifu na vyombo vyake.”
וידבר יהוה אל משה ואל אהרן לאמר 17
BWANA akanena na Musa na Haruni. Akasema,
אל תכריתו את שבט משפחת הקהתי מתוך הלוים 18
Usiruhusu kabila la Wakohathi kuondolewa kati ya Walawi.
וזאת עשו להם וחיו ולא ימתו בגשתם את קדש הקדשים אהרן ובניו יבאו ושמו אותם איש איש על עבדתו ואל משאו 19
Walinde waishi ili wasije wakafa, kwa kufanya hivi. Wanapokuwa wanasogelea
ולא יבאו לראות כבלע את הקדש ומתו 20
wasije wakaingia ndani ili kuona eneo takatifu hata kwa kitambo, vinginevyo watakufa. Bali Haruni na wanawe wanaweza kuingia, ndipo Haruni na Wanawe watakapowapangia Wakohathi kazi maalumu ya kufanya, kwa kila mmoj.”
וידבר יהוה אל משה לאמר 21
BWANA akanena na Musa tena, Akasema, “Fanya sensa kwa wana Gerishoni pia, kwa kufuata familia za mababu zao, koo zao.
נשא את ראש בני גרשון--גם הם לבית אבתם למשפחתם 22
Uwahesabu wale wenye umri wa mika thelathini hadi miaka hamsini.
מבן שלשים שנה ומעלה עד בן חמשים שנה--תפקד אותם כל הבא לצבא צבא לעבד עבדה באהל מועד 23
Uwahesabu wote ili waje kuungana na wale wanaotumika katika hema ya kukutania.
זאת עבדת משפחת הגרשני--לעבד ולמשא 24
Hii ndiyo itakuwa kazi ya koo za Gerishoni, wanapotumikia na wanachobeba.
ונשאו את יריעת המשכן ואת אהל מועד מכסהו ומכסה התחש אשר עליו מלמעלה ואת מסך--פתח אהל מועד 25
Watabeba pazia la masikani, hema la kukutania, na vifunikio vyake, vifuniko vya ngozi ya pomboo ambvyo viko juu yake, na pazia kwenye lango la hema ya kukutania.
ואת קלעי החצר ואת מסך פתח שער החצר אשר על המשכן ועל המזבח סביב ואת מיתריהם ואת כל כלי עבדתם ואת כל אשר יעשה להם ועבדו 26
Watabeba pazia la ua, pazia la kwenye mlango wa ua, ambao uko karibu na maskani karibu na madhabahu, kamba zake na vifaa vyote vya utumishi wake. Chochote kinachotakiwa kufanywa kutokana na vitu hivi, wao ndio watakaofanya.
על פי אהרן ובניו תהיה כל עבדת בני הגרשני לכל משאם ולכל עבדתם ופקדתם עלהם במשמרת את כל משאם 27
Haruni na wanawe ndio watakaongoza utumishi wa uzao wa Wagerishoni, kwa vitu vyote vile vya kusafirisha, na katika utumishi wao wote. Lazima uwagawie majukumu yao yote.
זאת עבדת משפחת בני הגרשני--באהל מועד ומשמרתם--ביד איתמר בן אהרן הכהן 28
Huu ndio utumishi wa koo za uzao wa wana wa Wagerishoni katka hema ya kukutania. Ithamari mwana wa Haruni kuhani atawaongoza katika utumishi.
בני מררי--למשפחתם לבית אבתם תפקד אתם 29
Utawahesabu uzao wa Merari kwa koo zao, na uwapange katika familia za mabau zao,
מבן שלשים שנה ומעלה ועד בן חמשים שנה--תפקדם כל הבא לצבא לעבד את עבדת אהל מועד 30
kuanzia wenye umri wa miaka thelatini hadi miaka hamsini. Umuhesabu kila atakayeungana na kundi lenye utumishi katika hema ya kukutania.
וזאת משמרת משאם לכל עבדתם באהל מועד קרשי המשכן ובריחיו ועמודיו ואדניו 31
Huu ndio wajibu na kazi yao katika utumishi wao kwenye hema ya kukutania. Watazilinda mbao za maskani, mataluma yake, nguzo na makalishio yake,
ועמודי החצר סביב ואדניהם ויתדתם ומיתריהם לכל כליהם ולכל עבדתם ובשמת תפקדו את כלי משמרת משאם 32
pamoja na nguzo za ua zinazozunguka masikani, makalishio yake, vigingi na kamba zake, na vifaa vinginevya ujenzi. Waorodheshe kwa majina na majukumu yao.
זאת עבדת משפחת בני מררי לכל עבדתם באהל מועד--ביד איתמר בן אהרן הכהן 33
Huu ndio utumishi wa koo za uzao wa Merari, ambao wanatakiwa kufanya katika hema ya kukutania, chini ya uongozi wa Ithmari mwana wa Haruni kuhani.”
ויפקד משה ואהרן ונשיאי העדה את בני הקהתי למשפחתם ולבית אבתם 34
Musa na Haruni na viongozi wa watu waliwahesabu wana wa uzao wa Wakohathi kwa kufuata koo za familia za mababu zao.
מבן שלשים שנה ומעלה ועד בן חמשים שנה--כל הבא לצבא לעבדה באהל מועד 35
Waliwahesabu wale wenye umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini. Walimhesabu kila mmoja aliyepaswa kuungana na kundi linalotoa huduma ya utumishi kwenye hema ya kukutania.
ויהיו פקדיהם למשפחתם--אלפים שבע מאות וחמשים 36
Waliwahesabu wanaume 2, 750 kwa kufuata koo zao.
אלה פקודי משפחת הקהתי כל העבד באהל מועד אשר פקד משה ואהרן על פי יהוה ביד משה 37
Musa na Haruni waliwahesabu wanaume wote kutoka koo na familia za Wakohathi ambao hutumika kwenye hema ya kukutania. Walifanya hivi kwa kumtii BWANA aliyewaagiza kupitia kwa Musa.
ופקודי בני גרשון למשפחותם ולבית אבתם 38
Uzao wa Gerishoni walihesabiwa kufuata koo na familia za mababu zao,
מבן שלשים שנה ומעלה ועד בן חמשים שנה--כל הבא לצבא לעבדה באהל מועד 39
kuanzia umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini, kwa kila mmoja aliyetakiwa kuungana na watu wanaotoa huduma kwenye hema ya kukutania.
ויהיו פקדיהם למשפחתם לבית אבתם--אלפים ושש מאות ושלשים 40
Wanaume wote waliohesabiwa kufuata koo na familia za mababu zao walikuwa 2, 630.
אלה פקודי משפחת בני גרשון כל העבד באהל מועד--אשר פקד משה ואהרן על פי יהוה 41
Musa na Haruni walizihesabu koo za uzao wa Gerishoni ambao watatumika kwenye hema ya kukutania. Walifanya hivi ili kutii ambacho BWANA aliwaamuru kufanya kuptia kwa Musa.
ופקודי משפחת בני מררי למשפחתם לבית אבתם 42
Uzao wa Merari walihesabiwa kwa koo kupitia familia za mababu zao,
מבן שלשים שנה ומעלה ועד בן חמשים שנה--כל הבא לצבא לעבדה באהל מועד 43
kuanzia wenye umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini, kila anayepaswa kuungana na watu wanaotumika kwenye hema ya kukutania.
ויהיו פקדיהם למשפחתם--שלשת אלפים ומאתים 44
Wanaume wote waliohesabiwa kupitia koo za familia za mababu zao walikuwa 3. 200.
אלה פקודי משפחת בני מררי אשר פקד משה ואהרן על פי יהוה ביד משה 45
Musa na Haruni waliwahesabu wanaume hawa, uzao wa Merari. Kw kufanya hivi walitii amri ya BWANA aliyowaaagiza kufanya kupitia kwa Musa.
כל הפקדים אשר פקד משה ואהרן ונשיאי ישראל--את הלוים למשפחתם ולבית אבתם 46
Kwa hiyo Musa na Haruni na viongozi wa Israeli waliwahesabu Walawi wote kw kufuata koo na familia za mababu zao
מבן שלשים שנה ומעלה ועד בן חמשים שנה כל הבא לעבד עבדת עבדה ועבדת משא--באהל מועד 47
kuanzia wenye umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini. walimhesabu kila aliyepaswa kufanya kazi kwenye masikani, na kila aliyepaswa kubeba na kulinda vitu vya kwenye hema ya kukutania.
ויהיו פקדיהם--שמנת אלפים וחמש מאות ושמנים 48
Waliwahesabu wanaume 8, 580.
על פי יהוה פקד אותם ביד משה--איש איש על עבדתו ועל משאו ופקדיו אשר צוה יהוה את משה 49
Kwa agizo la BWANA, Musa alimhesabu kila mwanamume na kutunza kumbukumbu ya kazi ambayo kila mmoja anaweza kufanya. Kwa hivyo, walitii kile ambacho BWANA alikuwa amewaagiza kufanya kupitia kwa Musa.

< במדבר 4 >