< במדבר 2 >
וידבר יהוה אל משה ואל אהרן לאמר | 1 |
BWANA akasema na Musa na Haruni tena. Akamwambia,
איש על דגלו באתת לבית אבתם יחנו בני ישראל מנגד סביב לאהל מועד יחנו | 2 |
Kila mtu atapanga kulingana na mahali pake, pamoja na mabango ya baba zao. Watapanga kuzunguka hema ya kukutania kila upande.
והחנים קדמה מזרחה דגל מחנה יהודה לצבאתם ונשיא לבני יהודה נחשון בן עמינדב | 3 |
Wale watakaopanga mashariki mwa hema ya kukutania, mahali ambapo juu huonekana wakati wa jua kuchomoza, ni makambi ya Yuda nao watakuwa katika kundi lao. Nashoni mwana wa Aminadabu ni kiongozi wa watu wa Yuda.
וצבאו ופקדיהם--ארבעה ושבעים אלף ושש מאות | 4 |
Idadi ya watu wa Yuda ni 74, 600.
והחנים עליו מטה יששכר ונשיא לבני יששכר נתנאל בן צוער | 5 |
Kabila la Isakari litapanga mbele ya Yuda. Nethaneli mwana wa Zuari ataliongoza jeshi la Isakari.
וצבאו ופקדיו--ארבעה וחמשים אלף וארבע מאות | 6 |
Idadi ya kikosi chake ni wanaume 54, 000.
מטה זבולן ונשיא לבני זבולן אליאב בן חלן | 7 |
Kabila la Zabuloni litapanga mbele ya Isakari. Eliabu mwana wa Heloni ndiye atakayeliongoza jeshi la Zabuloni.
וצבאו ופקדיו--שבעה וחמשים אלף וארבע מאות | 8 |
Idadi ya kikosi chake ni 57, 400.
כל הפקדים למחנה יהודה מאת אלף ושמנים אלף וששת אלפים וארבע מאות--לצבאתם ראשנה יסעו | 9 |
Idadi yote ya kambi y a Yuda ni 186, 400. Watakuwa wa kwanza kuondoka.
דגל מחנה ראובן תימנה לצבאתם ונשיא לבני ראובן אליצור בן שדיאור | 10 |
Upande wa kusini kutakuwa na kambi ya Reubeni katika kundi lao. Kiongozi wa kundi la Reubeni ni Elizuri mwana wa Shedeuri.
וצבאו ופקדיו--ששה וארבעים אלף וחמש מאות | 11 |
Idadi ya kikosi chake ni 46, 500.
והחונם עליו מטה שמעון ונשיא לבני שמעון שלמיאל בן צורישדי | 12 |
Simeoni atapanga mbele ya Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Zurishadai.
וצבאו ופקדיהם--תשעה וחמשים אלף ושלש מאות | 13 |
Waliohesabiwa kwenye kikosi chake ni 59, 300.
ומטה גד ונשיא לבני גד אליסף בן רעואל | 14 |
Kabila la Gadi litafuatia. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deuli.
וצבאו ופקדיהם--חמשה וארבעים אלף ושש מאות וחמשים | 15 |
Idadi ya kikosi chake ni 45, 650.
כל הפקדים למחנה ראובן מאת אלף ואחד וחמשים אלף וארבע מאות וחמשים--לצבאתם ושנים יסעו | 16 |
Wote waliohesabiwa kwenye kambi ya Reubeni, kulingana na kikosi chake, ni 151, 450. Watakuwa wa pili kuondoka.
ונסע אהל מועד מחנה הלוים בתוך המחנת כאשר יחנו כן יסעו איש על ידו לדגליהם | 17 |
Kifuatacho, ni hema la kukutania kuondoka kambini pamoja na Walawi likiwa katikati ya kambi zote. Lazima waondoke hapo kambini kwa mpangilio huo kama walivyoingia kwenye kambi. Kila mwanamume lazima awe mahali pake kwa kufuata bango lake.
דגל מחנה אפרים לצבאתם ימה ונשיא לבני אפרים אלישמע בן עמיהוד | 18 |
Migawanyiko ya kambi y Efraimu kufuata mahali pake. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi.
וצבאו ופקדיהם--ארבעים אלף וחמש מאות | 19 |
Hesabu ya kikosi hiki ni 40, 500.
ועליו מטה מנשה ונשיא לבני מנשה גמליאל בן פדהצור | 20 |
Baada ya hao lilifuata kabila la Manase. Kiongozi wa Manase ni Gamaliel mwana wa Pedazuri.
וצבאו ופקדיהם--שנים ושלשים אלף ומאתים | 21 |
Hesabu ya kikosi hiki ni 32, 200.
ומטה בנימן ונשיא לבני בנימן אבידן בן גדעני | 22 |
Kabila litakalofuata ni la Benjamini. Kiongozi wa Benjamini n Abidani mwana wa Gidioni.
וצבאו ופקדיהם--חמשה ושלשים אלף וארבע מאות | 23 |
Hesabu ya kikosi hiki ni 35, 000
כל הפקדים למחנה אפרים מאת אלף ושמנת אלפים ומאה--לצבאתם ושלשים יסעו | 24 |
Wote waliohesabiwa katika kambi ya Efraimu ni 108, 100. Watakuwa wa tatu kuondoka.
דגל מחנה דן צפנה לצבאתם ונשיא לבני דן אחיעזר בן עמישדי | 25 |
Upande wa kaskazini kutakuwa na kambi ya kikosi cha Dani. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.
וצבאו ופקדיהם--שנים וששים אלף ושבע מאות | 26 |
Hesabu ya kikosi hiki ni 62, 700.
והחנים עליו מטה אשר ונשיא לבני אשר פגעיאל בן עכרן | 27 |
Watu wa kabila ya Asheri watapanga mbele ya Dani. Kiongozi wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okirani.
וצבאו ופקדיהם--אחד וארבעים אלף וחמש מאות | 28 |
Hesabu ya Kikosi hiki ni 41, 500.
ומטה נפתלי ונשיא לבני נפתלי אחירע בן עינן | 29 |
Kabila la Naftali ndilo litakalofuatia. Kiongozi wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani.
וצבאו ופקדיהם--שלשה וחמשים אלף וארבע מאות | 30 |
Hesabu ya kikosi hiki ni 53, 400.
כל הפקדים למחנה דן--מאת אלף ושבעה וחמשים אלף ושש מאות לאחרנה יסעו לדגליהם | 31 |
Wote waliohesabiwa kwenye kambi ya Dani ni 157, 600. Hawa watakuwa wa mwisho kuondoka kambini, wakifuata bango lao.
אלה פקודי בני ישראל לבית אבתם כל פקודי המחנת לצבאתם--שש מאות אלף ושלשת אלפים וחמש מאות וחמשים | 32 |
Hawa ndio Waisraeli, waliohesabiwa kufuata familia zao. Wote waliohesabiwa kwenye kambi zao, kwa kufuata vikosi vyao ni 603, 550.
והלוים--לא התפקדו בתוך בני ישראל כאשר צוה יהוה את משה | 33 |
Lakini Musa na Haruni hawakujumuisha Walawi kwenye Hesabu ya Waisrael. Ilikuwa kama BWANA alivyokuwa amemwagiza Musa.
ויעשו בני ישראל ככל אשר צוה יהוה את משה כן חנו לדגליהם וכן נסעו--איש למשפחתיו על בית אבתיו | 34 |
Watu wa Israel walifanya yote ambayo BWANA alimwagiza Musa. Walipanga kwa kufuata mabango yao. Walisafiri kutoka kambini kwa kufuata jamaa zao, kwa mpangilio wa familia za koo zao.