< מיכה 4 >

והיה באחרית הימים יהיה הר בית יהוה נכון בראש ההרים ונשא הוא מגבעות ונהרו עליו עמים 1
Lakini katika siku za mwisho itakuja kuhusu kwamba mlima wa nyumba ya Yahwe utawekwa imare juu ya milima mingine. Utainuliwa juu ya milima, na watu watautakabisha.
והלכו גוים רבים ואמרו לכו ונעלה אל הר יהוה ואל בית אלהי יעקב ויורנו מדרכיו ונלכה בארחתיו כי מציון תצא תורה ודבר יהוה מירושלם 2
Mataifa mengi yataenda na kusema, “Njoni, twendeni juu kwenye mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, na tutembea katika njia zake.” Kwa kuwa kutoka Sayuni sheria itatoka, na neno la Yahwe kutoka Yerusalemu.
ושפט בין עמים רבים והוכיח לגוים עצמים עד רחוק וכתתו חרבתיהם לאתים וחניתתיהם למזמרות--לא ישאו גוי אל גוי חרב ולא ילמדון עוד מלחמה 3
Atahukumu miongoni mwa watu na kuamua kuhusiana na mataifa mengi ya mbali. Watapoga mapanga yao kuwa plau na mikuki yao kuwa miuundu ya kupogolea. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa, wala kutawala kwa vita tena.
וישבו איש תחת גפנו ותחת תאנתו--ואין מחריד כי פי יהוה צבאות דבר 4
Badala yake, wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake. Hakuna mtu atakayewafanya waogope, kwa kuwa mdomo wa Yahwe wa majeshi umesema.
כי כל העמים ילכו איש בשם אלהיו ואנחנו נלך בשם יהוה אלהינו--לעולם ועד 5
Kwa kuwa watu wote wataenenda, kila mmoja, katika jina la mungu wake. Lakini sisi tutaenenda katika jina la Yahwe Mungu wetu milele na milele.
ביום ההוא נאם יהוה אספה הצלעה והנדחה אקבצה ואשר הרעתי 6
“Katika siku hiyo,” aseme Yahwe, “Nitamkusanya achechemeaye na kumkusanya aliyefukuzwa, wale ambao nimewatesa.
ושמתי את הצלעה לשארית והנהלאה לגוי עצום ומלך יהוה עליהם בהר ציון מעתה ועד עולם 7
Nitamrudisha aliyechechemea kwenye mabaki, na yeye aliyetupwa kwenye taifa imara, na mimi, Yahwe, nitatawala juu yao katika Milima Sayuni, sasa na milele.
ואתה מגדל עדר עפל בת ציון--עדיך תאתה ובאה הממשלה הראשנה ממלכת לבת ירושלם 8
Kama kwako, mnara wa saa kwa ajili ya kundi, mlima wa binti wa Sayuni-utakuja kwenu, utawala wenu wa zamani utarudishwa, ufalme ambao unaomilikiwa na binti wa Yerusalemu.
עתה למה תריעי רע המלך אין בך אם יועצך אבד--כי החזיקך חיל כיולדה 9
Sasa, kwa nini unapiga kelele kwa sauti kuu? Je hakuna mfalme miongoni mwenu? Je mshauri wako amekufa? Kwa nini uchungu umekushika kama yule mwanamke akiwa anazaa?
חולי וגחי בת ציון כיולדה כי עתה תצאי מקריה ושכנת בשדה ובאת עד בבל שם תנצלי--שם יגאלך יהוה מכף איביך 10
Kuwa katika uchungu wa kuzaa ili uzae, binti Sayuni, kama mwanamke mwenye uchungu. Kwa sasa utatoka nje ya mji, kuishi kwenye shamba, na kwenda Babeli. Huko utaokolewa. Huko Yahwe atakuokoa kutoka kwenye mikono ya maadui.
ועתה נאספו עליך גוים רבים--האמרים תחנף ותחז בציון עינינו 11
Sasa mataifa mengi yamekusanyika juu yako; wakisema; 'Atiwe unajisi; macho yenu yaangalie Sayuni.”'
והמה לא ידעו מחשבות יהוה ולא הבינו עצתו כי קבצם כעמיר גרנה 12
Nabii asema, “Hawayajui mawazo ya Yahwe, wala hawaelewi mpango wake, kwa kuwa wamewakusanaya kama miganda kupura sakafuni.”
קומי ודושי בת ציון כי קרנך אשים ברזל ופרסתיך אשים נחושה והדקות עמים רבים והחרמתי ליהוה בצעם וחילם לאדון כל הארץ 13
Yahwe asema, “siamama na upure, binti Sayuni, kwa kuwa nitaifanya pembe yako kuwa chuma, na nitazifanya kwato zako kuwa shaba. Utaponda watu wengi. Nitaweka wakfu udhalimu wao kwangu mwenyewe, Yahwe, miliki zao kwangu, Bwana wa dunia nzima.”

< מיכה 4 >