< איכה 3 >

אני הגבר ראה עני בשבט עברתו 1
Mimi ni mwanaume nilyeona maangaiko chini ya gongo la hasira ya Yahweh.
אותי נהג וילך חשך ולא אור 2
Amenifukuza na kunisababisha kutembea kwenye giza kuliko kwenye nuru.
אך בי ישב יהפך ידו כל היום 3
Hakika amenigeuzia mkono wake dhidi yangu tena na tena, siku yote.
בלה בשרי ועורי שבר עצמותי 4
Amefanya mwili wangu na ngozi yangu kufifia; amevunja mifupa yangu.
בנה עלי ויקף ראש ותלאה 5
Amejenga vifusi vya udogo dhidi yangu, na kunizingira na uchungu na ugumu.
במחשכים הושיבני כמתי עולם 6
Amefanya ni ishi sehemu za giza, kama hao walio kufa zamani.
גדר בעדי ולא אצא הכביד נחשתי 7
Amejenga ukuta kunizunguka na siwezi kutoroka. Amefanya minyororo yangu mizito
גם כי אזעק ואשוע שתם תפלתי 8
na japo nina ita na kulilia msaada, anazima maombi yangu.
גדר דרכי בגזית נתיבתי עוה 9
Ameziba njia yangu kwa ukuta wa mawe ya kuchonga; amefanya njia yangu mbaya.
דב ארב הוא לי אריה (ארי) במסתרים 10
Yeye ni kama dubu anasubiri kunishambulia, simba katika maficho;
דרכי סורר ויפשחני שמני שמם 11
amegeuza pembeni njia zangu, amenifanya ukiwa.
דרך קשתו ויציבני כמטרא לחץ 12
Amepindisha upinde wake na kunifanya mimi kama lengo la mshale wake.
הביא בכליתי בני אשפתו 13
Ametoboa maini yangu kwa mishale ya mfuko wake.
הייתי שחק לכל עמי נגינתם כל היום 14
Nilikuwa kichekesho kwa watu wangu wote, kielelezo cha dhihaka yao siku nzima.
השביעני במרורים הרוני לענה 15
Amenijaza kwa uchungu na kunilazimisha kunywa maji machungu.
ויגרס בחצץ שני הכפישני באפר 16
Alivunja meno yangu na kokoto; amenisukuma chini kwenye fumbi.
ותזנח משלום נפשי נשיתי טובה 17
Nafsi yangu imenyimwa amani; nimesahau furaha ni nini.
ואמר אבד נצחי ותוחלתי מיהוה 18
Hivyo na sema, “Ustahimilivu wangu umeangamia na pia tumaini langu kwa Yahweh.”
זכר עניי ומרודי לענה וראש 19
Kumbuka mateso yangu na kuangaika kwangu, maji machungu na uchungu.
זכור תזכור ותשיח (ותשוח) עלי נפשי 20
Ninaendelea kukumbuka na nimeinama ndani yangu.
זאת אשיב אל לבי על כן אוחיל 21
Lakini ni vuta hili akilini mwangu na hivyo nina matumaini:
חסדי יהוה כי לא תמנו כי לא כלו רחמיו 22
Upendo dhabiti wa Yahweh haukomi na huruma zake haziishi,
חדשים לבקרים רבה אמונתך 23
ni mpya kila asubui; uaminifu wako ni mkubwa.
חלקי יהוה אמרה נפשי על כן אוחיל לו 24
“Yahweh ni urithi wangu,” Nilisema, hivyo nitamtumainia.
טוב יהוה לקוו לנפש תדרשנו 25
Yahweh ni mwema kwao wanao msubiri, kwa anaye mtafuta.
טוב ויחיל ודומם לתשועת יהוה 26
Ni vizuri kusubiri taratibu kwa uwokovu wa Yahweh.
טוב לגבר כי ישא על בנעוריו 27
Ni vizuri kwa mtu kubeba nira katika ujana.
ישב בדד וידם כי נטל עליו 28
Acha aketi peke yake katika utulivu, inapo kuwa imewekwa juu yake.
יתן בעפר פיהו אולי יש תקוה 29
Acha aeke mdomo wake kwenye vumbi - kunaweza bado kuwa na matumaini.
יתן למכהו לחי ישבע בחרפה 30
Acha atoa shavu lake kwa yeye anaye mpiga, na ajazwe tele kwa aibu.
כי לא יזנח לעולם אדני 31
Kwa kuwa Bwana hatatukataa milele,
כי אם הוגה ורחם כרב חסדיו 32
lakini japo anatia uzuni, ata kuwa na huruma kwa kadiri ya mwingi wa upendo wake dhabiti.
כי לא ענה מלבו ויגה בני איש 33
Kwa kuwa haadhibu kutoka moyoni mwake au kutesa watoto wa mwanadamu.
לדכא תחת רגליו כל אסירי ארץ 34
Kukanyaga chini ya mguu wafungwa wote wa dunia,
להטות משפט גבר נגד פני עליון 35
kumnyima haki mtu mbele ya uwepo wa Aliye Juu,
לעות אדם בריבו אדני לא ראה 36
mkunyima haki mtu - Bwana hataidhinisha vitu kama hivyo!
מי זה אמר ותהי אדני לא צוה 37
Ni nani aliye zungumza na ikatimia, kama sio Bwana kutamka?
מפי עליון לא תצא הרעות והטוב 38
Sio kutoka mdomoni mwa Aliye Juu majanga na mazuri yanakuja?
מה יתאונן אדם חי גבר על חטאו 39
Mtu aliye hai anawezaje kulalamika? Mtu anawezaje kulalamika kwa adhabu ya dhambi zake?
נחפשה דרכינו ונחקרה ונשובה עד יהוה 40
Natujichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie Yahweh.
נשא לבבנו אל כפים אל אל בשמים 41
Na tunyanyue mioyo yetu na mikono yetu kwa Yahweh mbinguni:
נחנו פשענו ומרינו אתה לא סלחת 42
“Tumekosea na kuasi, na haujasamehe.
סכותה באף ותרדפנו הרגת לא חמלת 43
Umejifunika na hasira na kutukimbiza, umeua na haujanusuru.
סכותה בענן לך מעבור תפלה 44
Umejifunika na wingu ili kwamba kusiwe na ombi linaloweza kupita.
סחי ומאוס תשימנו בקרב העמים 45
Umetufanya kama uchafu na taka miongoni mwa mataifa.
פצו עלינו פיהם כל איבינו 46
Maadui wetu wote wametulaani,
פחד ופחת היה לנו השאת והשבר 47
wasiwasi na shimo limetujia, maafa na uharibifu.
פלגי מים תרד עיני על שבר בת עמי 48
Macho yangu yanatiririka na miferiji ya machozi kwasababu ya watu wangu.
עיני נגרה ולא תדמה מאין הפגות 49
Macho yangu yatatoa machozi pasipo kikomo; pasipo hauweni,
עד ישקיף וירא יהוה משמים 50
mpaka atakapo tazama chini na Yahweh ataona kutoka mbinguni.
עיני עוללה לנפשי מכל בנות עירי 51
Macho yangu yana ni sababishia uzuni kwasababu ya mabinti wa mji wangu.
צוד צדוני כצפור איבי חנם 52
Nimewindwa kama ndege hao walio kuwa maadui zangu; wameniwinda pasipo sababu.
צמתו בבור חיי וידו אבן בי 53
Wamenitupa kwenye shimo na wakanitupia jiwe,
צפו מים על ראשי אמרתי נגזרתי 54
na maji yaka mwagika juu ya kichwa changu. Nilisema, “Nimekatwa mbali!”
קראתי שמך יהוה מבור תחתיות 55
Nililiita jna lako, Yahweh, kutoka kina cha shimo.
קולי שמעת אל תעלם אזנך לרוחתי לשועתי 56
Ulisikia sauti yangu. Ulisikia sauti yangu nilipo sema, “Usifunge sikio lako kwa kilio changu cha msaada.”
קרבת ביום אקראך אמרת אל תירא 57
Ulikuja karibu siku niliyo kuiita; ulisema, “Usiogope”
רבת אדני ריבי נפשי גאלת חיי 58
Bwana, ulitetea kesi yangu, uliokoa maisha yangu!
ראיתה יהוה עותתי שפטה משפטי 59
Yahweh, umeona mabaya waliyo ni fanyia, hukumu kesi yangu.
ראיתה כל נקמתם--כל מחשבתם לי 60
Umeona matusi yao, mipango yao yote dhidi yangu -
שמעת חרפתם יהוה כל מחשבתם עלי 61
Umesikia dhihaka yao, Yahweh, na mipango yao kunihusu.
שפתי קמי והגיונם עלי כל היום 62
Midomo ya hao wanao inuka kinyume changu, na mashtaka yao, inakuja dhidi yangu siku nzima.
שבתם וקימתם הביטה אני מנגינתם 63
Ngalia jinsi wanavyo keti na kuinuka; wana nidhihaki na nyimbo zao.
תשיב להם גמול יהוה כמעשה ידיהם 64
Walipize, Yahweh, kwa kadiri ya waliyo fanya.
תתן להם מגנת לב תאלתך להם 65
Utaacha mioyo yao bila lawama! Hukumu yako iwe juu yao!
תרדף באף ותשמידם מתחת שמי יהוה 66
Una wakimbiza kwa hasira na kuwaharibu nchini ya mbingu, Yahweh!

< איכה 3 >