< איכה 2 >

איכה יעיב באפו אדני את בת ציון--השליך משמים ארץ תפארת ישראל ולא זכר הדם רגליו ביום אפו 1
Bwana amemfunika binti wa Sayuni chini ya wingu la hasira yake. Ametupa utukufu wa Israeli chini kutoka mbinguni hadi duniani. Hajakumba stuli yake ya miguu siku ya hasira yake.
בלע אדני לא (ולא) חמל את כל נאות יעקב--הרס בעברתו מבצרי בת יהודה הגיע לארץ חלל ממלכה ושריה 2
Bwana amemeza na hajawa na huruma kwa miji yote ya Yakobo. Siku za hasira zake ameangusha miji imara ya binti wa Yuda; kwa aibu ameshusha chini ufalme na watala wake.
גדע בחרי אף כל קרן ישראל--השיב אחור ימינו מפני אויב ויבער ביעקב כאש להבה אכלה סביב 3
Kwa hasira kali amekata kila pembe ya Israeli. Ameurudisha mkono wake kutoka kwa adui. Amechoma Yakobo kama moto mkali unao teketeza kila kitu karibu yake.
דרך קשתו כאויב נצב ימינו כצר ויהרג כל מחמדי עין באהל בת ציון שפך כאש חמתו 4
Kama adui amepindisha upinde wake kuelekea kwetu, na wakulia wake yupo tayari kushambulia. Amewachinja wote walio kuwa wanampendeza katika hema la binti wa Sayuni; Amemwaga gadhabu yake kama moto
היה אדני כאויב בלע ישראל--בלע כל ארמנותיה שחת מבצריו וירב בבת יהודה תאניה ואניה 5
Bwana amekuwa kama adui. Amemeza Israeli. Amemeza majumba yake yote. Ameharibu ngome zake. Ameongeza kilio na maombolezo kati ya mabinti wa Yuda.
ויחמס כגן שכו שחת מעדו שכח יהוה בציון מועד ושבת וינאץ בזעם אפו מלך וכהן 6
Ameshambulia hema lake la kukutania kama kajumba cha bustani. Ameharibu sehemu ya kukusanyikia. Yahweh amesababisha kukusanyika na Sabato kusahaulika Sayuni, kwa kuwa amemdharau mfalme na kuhani katika ukali wa hasira yake.
זנח אדני מזבחו נאר מקדשו--הסגיר ביד אויב חומת ארמנותיה קול נתנו בבית יהוה כיום מועד 7
Bwana amekataa madhabahu yake na kukana sehemu yake takatifu. Ametoa kuta za majumba mikononi mwa adui. Wamepaza sauti nyumbani mwa Yahweh, kama siku ya sherehe.
חשב יהוה להשחית חומת בת ציון--נטה קו לא השיב ידו מבלע ויאבל חל וחומה יחדו אמללו 8
Yahweh aliamua kuharibu ukuta wa mji wa binti wa Sayuni. Amenyoosha kamba ya kipimo na hajauzuia mkono wake kutoharibu ukuta. Amefanya minara na ukuta kuomboleza; pamoja vilipotea.
טבעו בארץ שעריה אבד ושבר בריחיה מלכה ושריה בגוים אין תורה--גם נביאיה לא מצאו חזון מיהוה 9
Malango yake yameanguka chini, ameharibu na kuvunja chuma za ukuta. Mfalme wake na watoto wa mfalme wapo miongoni mwa mataifa, sheria haipo tena na manabii wake hawapati maono kutoka kwa Yahweh.
ישבו לארץ ידמו זקני בת ציון--העלו עפר על ראשם חגרו שקים הורידו לארץ ראשן בתולת ירושלם 10
Wazee wa binti wa Sayuni wameketi chini na ukimya. Wamerusha vumbi kichwani mwao na kuvaa magunia. Mabikra wa Yerusalemu wameinamisha vichwa vyao chini.
כלו בדמעות עיני חמרמרו מעי--נשפך לארץ כבדי על שבר בת עמי בעטף עולל ויונק ברחבות קריה 11
Macho yangu yamekaukiwa machozi yake; tumbo langu la nguruma; sehemu zangu za ndani zimemwagika chini kwasababu ya uharibifu wa binti wa watu wangu, watoto na wachanga wamezimia mitaani mwa mji.
לאמתם יאמרו איה דגן ויין בהתעטפם כחלל ברחבות עיר--בהשתפך נפשם אל חיק אמתם 12
Wanasema kwa mama zao, “Mbegu ziko wapi na mvinyo?” kama wanavyo zimia kama mtu aliye jeruhiwa mitaani mwa mji, maisha yao yamemwaga kwenye kifua cha mama zao.
מה אעידך מה אדמה לך הבת ירושלם--מה אשוה לך ואנחמך בתולת בת ציון כי גדול כים שברך מי ירפא לך 13
Nini naeza kusema kwako, binti wa Yerusalemu? Naweza kufananisha na nini, ili ni kufariji, binti bikra wa Sayuni? Jera lako ni kubwa kama bahari. Nani anaweza kukuponya?
נביאיך חזו לך שוא ותפל ולא גלו על עונך להשיב שביתך (שבותך) ויחזו לך משאות שוא ומדוחים 14
Manabii wako wameona uongo na maono batili kwa ajili yako. Hawaja weka wazi dhambi zako kurejesha mali zako, lakini kwako wametoa matamko ya uongo na ya kupotosha.
ספקו עליך כפים כל עברי דרך--שרקו וינעו ראשם על בת ירושלם הזאת העיר שיאמרו כלילת יפי--משוש לכל הארץ 15
Wote wanao pita pembeni mwa barabara wana piga makofi kwako. Wanaguna na kutikisa vichwa vyao dhidi ya binti wa Yerusalemu na kusema, “Huu ndio mji walio uita 'Ukamilifu wa uzuri,' 'Furaha ya Dunia Yote'?”
פצו עליך פיהם כל איביך--שרקו ויחרקו שן אמרו בלענו אך זה היום שקוינהו מצאנו ראינו 16
Maadui zako wote walifungua vinywa vyao na kukudhihaki. Walizomea na kusaga meno na kusema, “Tumemmeza yeye! Hii ni siku tulio subiri! Tumeishi kuweza kuiona!”
עשה יהוה אשר זמם בצע אמרתו אשר צוה מימי קדם--הרס ולא חמל וישמח עליך אויב הרים קרן צריך 17
Yahweh amefanya alivyo panga kufanya. Ametimiza neno lake. Amekupindua bila huruma, kwa kuwa amemruhusu adui kukusherehekea; amenyanyua pembe za maadui zako.
צעק לבם אל אדני חומת בת ציון הורידי כנחל דמעה יומם ולילה--אל תתני פוגת לך אל תדם בת עינך 18
Mioyo yao ikamlilia Bwana, kuta za binti wa Sayuni! Fanya machozi yako kutiririka chini kama mto usiku na mchana. Usijipatie hauweni, macho yako bila hauweni.
קומי רני בליל (בלילה) לראש אשמרות--שפכי כמים לבך נכח פני אדני שאי אליו כפיך על נפש עולליך--העטופים ברעב בראש כל חוצות 19
Nyanyuka, lia usiku, mwanzo usiku wa manane! Mwaga moyo wako kama maji mbele za uso wa Bwana. Nyoosha juu mikono yako kwa ajili ya uzima wa watoto wako wanao zimia kwa njaa kwenye njia ya kila mtaa.
ראה יהוה והביטה למי עוללת כה אם תאכלנה נשים פרים עללי טפחים אם יהרג במקדש אדני כהן ונביא 20
Ona, Yahweh, na ukumbuke hao ulio watende haya. Wanawake wale tunda la uzazi wao, watoto walio wajali? Makuhani na manabii wa chinjwe sehemu takatifu ya Bwana?
שכבו לארץ חוצות נער וזקן בתולתי ובחורי נפלו בחרב הרגת ביום אפך טבחת לא חמלת 21
Wote wadogo kwa wakubwa wana keti kwenye udongo wa mitaa. Wanawake wangu wadogo na wanaume wangu wadogo wameanguaka kwa upanga; umewachinja pasipo kuwa hurumia.
תקרא כיום מועד מגורי מסביב ולא היה ביום אף יהוה פליט ושריד אשר טפחתי ורביתי איבי כלם 22
Umeitisha, kama ungewaita watu katika siku ya maakuli, hofu yangu kila sehemu, katika siku ya hasira ya Yahweh hakuna aliye toroka; hao niliyo wajali na kuwakuza, adui wangu amewaharibu.

< איכה 2 >