< איוב 7 >
הלא-צבא לאנוש על- (עלי-) ארץ וכימי שכיר ימיו | 1 |
“Je, mwanadamu hana kazi ngumu duniani? Siku zake si kama zile za mtu aliyeajiriwa?
כעבד ישאף-צל וכשכיר יקוה פעלו | 2 |
Kama mtumwa anavyovionea shauku vivuli vya jioni, au mtu aliyeajiriwa anavyoungojea mshahara wake,
כן הנחלתי לי ירחי-שוא ולילות עמל מנו-לי | 3 |
ndivyo nilivyogawiwa miezi ya ubatili, nami nimeandikiwa huzuni usiku hata usiku.
אם-שכבתי-- ואמרתי מתי אקום ומדד-ערב ושבעתי נדדים עדי-נשף | 4 |
Wakati nilalapo ninawaza, ‘Itachukua muda gani kabla sijaamka?’ Usiku huwa mrefu, nami najigeuzageuza hadi mapambazuko.
לבש בשרי רמה וגיש (וגוש) עפר עורי רגע וימאס | 5 |
Mwili wangu umevikwa mabuu na uchafu, ngozi yangu imetumbuka na kutunga usaha.
ימי קלו מני-ארג ויכלו באפס תקוה | 6 |
“Siku zangu zinapita upesi kuliko mtande wa kufuma, nazo zinafikia mwisho wake bila matumaini.
זכר כי-רוח חיי לא-תשוב עיני לראות טוב | 7 |
Kumbuka, Ee Mungu, maisha yangu ni kama pumzi; macho yangu kamwe hayataona tena raha.
לא-תשורני עין ראי עיניך בי ואינני | 8 |
Lile jicho linaloniona sasa halitaniona tena; utanitafuta, wala sitakuwepo.
כלה ענן וילך כן יורד שאול לא יעלה (Sheol ) | 9 |
Kama vile wingu liondokavyo na kutoweka, vivyo hivyo yeye ashukaye kaburini harudi tena. (Sheol )
לא-ישוב עוד לביתו ולא-יכירנו עוד מקמו | 10 |
Kamwe harudi tena nyumbani mwake; wala mahali pake hapatamjua tena.
גם-אני לא אחשך-פי אדברה בצר רוחי אשיחה במר נפשי | 11 |
“Kwa hiyo sitanyamaza; nitanena kutokana na maumivu makuu ya roho yangu, nitalalama kwa uchungu wa nafsi yangu.
הים-אני אם-תנין כי-תשים עלי משמר | 12 |
Je, mimi ni bahari, au mnyama mkubwa mno akaaye vilindini, hata uniweke chini ya ulinzi?
כי-אמרתי תנחמני ערשי ישא בשיחי משכבי | 13 |
Ninapofikiri kwamba kitanda changu kitanifariji, nacho kiti changu cha fahari kitapunguza malalamiko yangu,
וחתתני בחלמות ומחזינות תבעתני | 14 |
ndipo wanitisha kwa ndoto na kunitia hofu kwa maono,
ותבחר מחנק נפשי מות מעצמותי | 15 |
hivyo ninachagua kujinyonga na kufa, kuliko huu mwili wangu.
מאסתי לא-לעלם אחיה חדל ממני כי-הבל ימי | 16 |
Ninayachukia maisha yangu; nisingetamani kuendelea kuishi. Niache; siku zangu ni ubatili.
מה-אנוש כי תגדלנו וכי-תשית אליו לבך | 17 |
“Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki, kwamba unamtia sana maanani,
ותפקדנו לבקרים לרגעים תבחננו | 18 |
kwamba unamwangalia kila asubuhi na kumjaribu kila wakati?
כמה לא-תשעה ממני לא-תרפני עד-בלעי רקי | 19 |
Je, hutaacha kamwe kunitazama, au kuniacha japo kwa kitambo kidogo tu?
חטאתי מה אפעל לך-- נצר האדם למה שמתני למפגע לך ואהיה עלי למשא | 20 |
Ikiwa nimetenda dhambi, nimekufanyia nini, Ewe mlinzi wa wanadamu? Kwa nini umeniweka niwe shabaha yako? Je, nimekuwa mzigo kwako?
ומה לא-תשא פשעי-- ותעביר את-עוני כי-עתה לעפר אשכב ושחרתני ואינני | 21 |
Kwa nini husamehi makosa yangu na kuachilia dhambi zangu? Kwa kuwa hivi karibuni nitalala mavumbini; nawe utanitafuta, wala sitakuwepo.”