< איוב 35 >

ויען אליהו ויאמר 1
Aidha, Elihu aliendelea kusema,
הזאת חשבת למשפט אמרת צדקי מאל 2
“Je unadhani hii ni sawa unaposema, 'Haki yangu mbele ya Mungu?
כי-תאמר מה-יסכן-לך מה-אעיל מחטאתי 3
Kwa kuwa unauliza, 'Inafaa nini kwangu' na 'Ingekuwa nzuri kwangu kama ningekuwa nimetenda dhambi?'
אני אשיבך מלין-- ואת-רעיך עמך 4
Nitakujibu, wewe pamoja na marafiki zako.
הבט שמים וראה ושור שחקים גבהו ממך 5
Tazama juu angani, na ulione; angalia anga, ambalo liko juu sana kuliko wewe.
אם-חטאת מה-תפעל-בו ורבו פשעיך מה-תעשה-לו 6
Kama umetenda dhambi, ni madhara gani huwa unayafanya kwa Mungu? Ikiwa makosa yako yameongezeka zaidi, je huwa unafanya nini kwake?
אם-צדקת מה-תתן-לו או מה-מידך יקח 7
Kama wewe ni mwenye haki, unaweza kumpa nini? Je atapokea nini mkononi mwako?
לאיש-כמוך רשעך ולבן-אדם צדקתך 8
Uovu wako waweza kuwaumiza mtu, kama ulivyo wewe ni mtu, na haki yako yaweza kumnufaisha mwana mwingine wa mtu.
מרב עשוקים יזעיקו ישועו מזרוע רבים 9
Watu wanalia kwasababu ya matendo mengi ya unyanyasaji; wanaomba msaada katika mikono ya watu wenye nguvu.
ולא-אמר--איה אלוה עשי נתן זמרות בלילה 10
Lakini hakuna hata mmoja asemaye, ' Mungu Muumba wangu yuko wapi, ambaye hutoa nyimbo wakati wa usiku,
מלפנו מבהמות ארץ ומעוף השמים יחכמנו 11
ambaye hutufundisha sisi zaidi anavyowafundisha wanyama wa dunia, na ambaye hutufanya sisi kuwa wenye hekima kuliko ndege wa angani?
שם יצעקו ולא יענה-- מפני גאון רעים 12
Huko wanalia, lakini Mungu hawajibu kwasababu ya kibriu ya watu waovu.
אך-שוא לא-ישמע אל ושדי לא ישורנה 13
Kwa hakika Mungu hatasikia kilio cha kipumbavu; Mwenye nguvu wala hatajali.
אף כי-תאמר לא תשורנו דין לפניו ותחולל לו 14
Ni kwa namna gani atakujibu ikiwa unasema haumwoni, na ya kwamba hoja yako iko mbele yake, na ya kuwa unamngojea yeye!
ועתה--כי-אין פקד אפו ולא-ידע בפש מאד 15
Ni kwa jinsi gani atakujibu kama unasema kwamba hamwadhibu yeyote kwa hasira, na ya kwamba hajishughulishi na kiburi cha watu.
ואיוב הבל יפצה-פיהו בבלי-דעת מלין יכבר 16
Basi Ayubu hufumbua kinywa chake tu ili kusema upumbavu; huongeza maneno bila maarifa.”

< איוב 35 >