< איוב 33 >
ואולם--שמע-נא איוב מלי וכל-דברי האזינה | 1 |
“Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu; zingatia kila kitu nitakachosema.
הנה-נא פתחתי פי דברה לשוני בחכי | 2 |
Karibu nitafungua kinywa changu; maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu.
ישר-לבי אמרי ודעת שפתי ברור מללו | 3 |
Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu; midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo.
רוח-אל עשתני ונשמת שדי תחיני | 4 |
Roho wa Mungu ameniumba; pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai.
אם-תוכל השיבני ערכה לפני התיצבה | 5 |
Unijibu basi, kama unaweza; jiandae kunikabili mimi.
הן-אני כפיך לאל מחמר קרצתי גם-אני | 6 |
Mimi ni kama wewe mbele za Mungu; mimi pia nimetolewa kwenye udongo.
הנה אמתי לא תבעתך ואכפי עליך לא-יכבד | 7 |
Huna sababu ya kuniogopa, wala mkono wangu haupaswi kukulemea.
אך אמרת באזני וקול מלין אשמע | 8 |
“Lakini umesema nikiwa ninakusikia, nami nilisikia maneno yenyewe:
זך אני בלי-פשע חף אנכי ולא עון לי | 9 |
‘Mimi ni safi na sina dhambi; mimi ni safi na sina hatia.
הן תנואות עלי ימצא יחשבני לאויב לו | 10 |
Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu, naye ananiona kama adui yake.
ישם בסד רגלי ישמר כל-ארחתי | 11 |
Ananifunga miguu kwa pingu, tena anaziangalia njia zangu zote kwa karibu.’
הן-זאת לא-צדקת אענך כי-ירבה אלוה מאנוש | 12 |
“Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa, kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.
מדוע אליו ריבות כי כל-דבריו לא יענה | 13 |
Kwa nini unamlalamikia kwamba yeye hamjibu mwanadamu?
כי-באחת ידבר-אל ובשתים לא ישורנה | 14 |
Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, au wakati mwingine kwa njia nyingine, ingawa mwanadamu anaweza asielewe.
בחלום חזיון לילה--בנפל תרדמה על-אנשים בתנומות עלי משכב | 15 |
Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu wasinziapo vitandani mwao,
אז יגלה אזן אנשים ובמסרם יחתם | 16 |
anaweza akasemea masikioni mwao, na kuwatia hofu kwa maonyo,
להסיר אדם מעשה וגוה מגבר יכסה | 17 |
ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya na kumwepusha na kiburi,
יחשך נפשו מני-שחת וחיתו מעבר בשלח | 18 |
kuiokoa nafsi yake na shimo, uhai wake usiangamizwe kwa upanga.
והוכח במכאוב על-משכבו וריב (ורוב) עצמיו אתן | 19 |
Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake,
וזהמתו חיתו לחם ונפשו מאכל תאוה | 20 |
kiasi kwamba maisha yake yenyewe yanakataa chakula nayo nafsi yake ikakichukia kabisa hata chakula kizuri.
יכל בשרו מראי ושפי (ושפו) עצמתיו לא ראו | 21 |
Nyama ya mwili wake huisha kwa kukonda, nayo mifupa yake ambayo mwanzoni ilikuwa imefichika, sasa inatokeza nje.
ותקרב לשחת נפשו וחיתו לממתים | 22 |
Nafsi yake inakaribia kaburi, nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo.
אם-יש עליו מלאך--מליץ אחד מני-אלף להגיד לאדם ישרו | 23 |
“Kama bado kuna malaika upande wake kama mtetezi, mmoja miongoni mwa elfu, wa kumwambia mwanadamu lililo jema kwake,
ויחננו--ויאמר פדעהו מרדת שחת מצאתי כפר | 24 |
kumwonea huruma na kusema, ‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni; nimepata ukombozi kwa ajili yake’:
רטפש בשרו מנער ישוב לימי עלומיו | 25 |
ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto; hurudishwa upya kama siku za ujana wake.
יעתר אל-אלוה וירצהו וירא פניו בתרועה וישב לאנוש צדקתו | 26 |
Humwomba Mungu, akapata kibali kwake, huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha; Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu.
ישר על-אנשים ויאמר חטאתי וישר העויתי ולא-שוה לי | 27 |
Ndipo huja mbele za watu na kusema, ‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki, lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili.
פדה נפשי (נפשו) מעבר בשחת וחיתי (וחיתו) באור תראה | 28 |
Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni, nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’
הן-כל-אלה יפעל-אל-- פעמים שלוש עם-גבר | 29 |
“Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu; mara mbili hata mara tatu,
להשיב נפשו מני-שחת-- לאור באור החיים | 30 |
ili aigeuze nafsi yake toka shimoni, ili nuru ya uzima imwangazie.
הקשב איוב שמע-לי החרש ואנכי אדבר | 31 |
“Ayubu, zingatia, nisikilize mimi; nyamaza, nami nitanena.
אם-יש-מלין השיבני דבר כי-חפצתי צדקך | 32 |
Kama unalo lolote la kusema, unijibu; sema, kwa maana ninataka uonekane huna hatia.
אם-אין אתה שמע-לי החרש ואאלפך חכמה | 33 |
Lakini kama huna la kusema, basi nisikilize mimi; nyamaza, nami nitakufundisha hekima.”