< איוב 18 >

ויען בלדד השחי ויאמר 1
Bildadi Mshuhi akajibu:
עד-אנה תשימון קנצי למלין תבינו ואחר נדבר 2
“Je, ni lini utafika mwisho wa maneno haya? Uwe mwenye busara, nasi ndipo tutakapoweza kuongea.
מדוע נחשבנו כבהמה נטמינו בעיניכם 3
Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama, na kuonekana wajinga machoni pako?
טרף נפשו באפו הלמענך תעזב ארץ ויעתק-צור ממקמו 4
Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande katika hasira yako, je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake?
גם אור רשעים ידעך ולא-יגה שביב אשו 5
“Taa ya mwovu imezimwa, nao mwali wa moto wake umezimika.
אור חשך באהלו ונרו עליו ידעך 6
Mwanga hemani mwake umekuwa giza; taa iliyo karibu naye imezimika.
יצרו צעדי אונו ותשליכהו עצתו 7
Nguvu za hatua zake zimedhoofishwa; shauri lake baya litamwangusha.
כי-שלח ברשת ברגליו ועל-שבכה יתהלך 8
Miguu yake imemsukumia kwenye wavu, naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu.
יאחז בעקב פח יחזק עליו צמים 9
Tanzi litamkamata kwenye kisigino; mtego utamshikilia kwa nguvu.
טמון בארץ חבלו ומלכדתו עלי נתיב 10
Kitanzi kimefichwa ardhini kwa ajili yake; mtego uko kwenye njia yake.
סביב בעתהו בלהות והפיצהו לרגליו 11
Vitisho vimemtia hofu kila upande, na adui zake humwandama kila hatua.
יהי-רעב אנו ואיד נכון לצלעו 12
Janga linamwonea shauku; maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo.
יאכל בדי עורו יאכל בדיו בכור מות 13
Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake; mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake.
ינתק מאהלו מבטחו ותצעדהו למלך בלהות 14
Atangʼolewa kutoka usalama wa hema lake, na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.
תשכון באהלו מבלי-לו יזרה על-נוהו גפרית 15
Moto utakaa katika hema lake; moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake.
מתחת שרשיו יבשו וממעל ימל קצירו 16
Mizizi yake chini itakauka na matawi yake juu yatanyauka.
זכרו-אבד מני-ארץ ולא-שם לו על-פני-חוץ 17
Kumbukumbu lake litatoweka katika dunia, wala hatakuwa na jina katika nchi.
יהדפהו מאור אל-חשך ומתבל ינדהו 18
Ameondolewa nuruni na kusukumiwa gizani, naye amefukuzwa mbali atoke duniani.
לא נין לו ולא-נכד בעמו ואין שריד במגוריו 19
Hana mtoto wala mzao miongoni mwa watu wake, wala aliyenusurika mahali alipoishi.
על-יומו נשמו אחרנים וקדמנים אחזו שער 20
Watu wa magharibi watashangaa yaliyompata; watu wa mashariki watapatwa na hofu.
אך-אלה משכנות עול וזה מקום לא-ידע-אל 21
Hakika ndivyo yalivyo makao ya mtu mwovu; ndivyo palivyo mahali pake mtu asiyemjua Mungu.”

< איוב 18 >