< איוב 16 >

ויען איוב ויאמר 1
Kisha Ayubu akajibu:
שמעתי כאלה רבות מנחמי עמל כלכם 2
“Nimepata kusikia mambo mengi kama haya, nanyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha!
הקץ לדברי-רוח או מה-ימריצך כי תענה 3
Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho? Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno?
גם אנכי-- ככם אדברה לו יש נפשכם תחת נפשי-- אחבירה עליכם במלים ואניעה עליכם במו ראשי 4
Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi, kama mngekuwa katika hali yangu; ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu, na kuwatikisia ninyi kichwa changu.
אאמצכם במו-פי וניד שפתי יחשך 5
Lakini kinywa changu kingewatia moyo; faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu.
אם-אדברה לא-יחשך כאבי ואחדלה מה-מני יהלך 6
“Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi; nami kama nikijizuia, wala hayaondoki.
אך-עתה הלאני השמות כל-עדתי 7
Ee Mungu, hakika umenichakaza; umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote.
ותקמטני לעד היה ויקם בי כחשי בפני יענה 8
Umenikunjakunja, nalo limekuwa ushahidi; nako kukonda kwangu kumeongezeka sana na kushuhudia dhidi yangu.
אפו טרף וישטמני--חרק עלי בשניו צרי ילטש עיניו לי 9
Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake, na kunisagia meno yake; adui yangu hunikazia macho yake makali.
פערו עלי בפיהם--בחרפה הכו לחיי יחד עלי יתמלאון 10
Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki; hunipiga shavuni mwangu kwa dharau, na kuungana pamoja dhidi yangu.
יסגירני אל אל עויל ועל-ידי רשעים ירטני 11
Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya, na kunitupa katika makucha ya waovu.
שלו הייתי ויפרפרני-- ואחז בערפי ויפצפצני ויקימני לו למטרה 12
Mambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja; amenikamata shingo na kuniponda. Amenifanya mimi kuwa shabaha yake;
יסבו עלי רביו-- יפלח כליותי ולא יחמל ישפך לארץ מררתי 13
wapiga upinde wake wananizunguka. Bila huruma, huchoma figo zangu, na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi.
יפרצני פרץ על-פני-פרץ ירץ עלי כגבור 14
Huniponda tena na tena; hunishambulia kama shujaa wa vita.
שק תפרתי עלי גלדי ועללתי בעפר קרני 15
“Nimejishonea nguo ya gunia juu ya mwili wangu nami nimekizika kipaji cha uso wangu kwenye vumbi.
פני חמרמרה (חמרמרו) מני-בכי ועל עפעפי צלמות 16
Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia, macho yangu yamepigwa na giza kuu.
על לא-חמס בכפי ותפלתי זכה 17
Hata hivyo mikono yangu haijafanya jeuri, na maombi yangu ni safi.
ארץ אל-תכסי דמי ואל-יהי מקום לזעקתי 18
“Ee nchi, usiifunike damu yangu, nacho kilio changu kisinyamazishwe kamwe.
גם-עתה הנה-בשמים עדי ושהדי במרמים 19
Hata sasa shahidi wangu yuko mbinguni; wakili wangu yuko juu.
מליצי רעי אל-אלוה דלפה עיני 20
Mwombezi wangu ni rafiki yangu macho yangu yamwagapo machozi kwa Mungu;
ויוכח לגבר עם-אלוה ובן-אדם לרעהו 21
kwa niaba ya mtu anamsihi Mungu kama mtu anavyosihi kwa ajili ya rafiki yake.
כי-שנות מספר יאתיו וארח לא-אשוב אהלך 22
“Ni miaka michache tu itapita kabla sijaenda safari ambayo sitarudi.

< איוב 16 >