< איוב 15 >

ויען אליפז התימני ויאמר 1
Ndipo Elifazi Mtemani alijibu na kusema,
החכם יענה דעת-רוח וימלא קדים בטנו 2
Mtu mwenye hekima anapaswa kujibu kwa maarifa yasiyofaa na kujijaza mwenyewe na upepo wa mashariki?
הוכח בדבר לא-יסכון ומלים לא-יועיל בם 3
Anapaswa kuhojiana na mazungumzo yasiyo na faida au na hotuba ambazo kwa hizo yeye hawezi kufanya mema?
אף-אתה תפר יראה ותגרע שיחה לפני-אל 4
Dhahiri, wewe wafifisha heshima ya Mungu; Wewe wazuia heshima kwa yeye,
כי יאלף עונך פיך ותבחר לשון ערומים 5
kwa maana uovu wako hufundisha midomo yako; Wewe wachagua kuwa na ulimi wa mtu mwenye hila.
ירשיעך פיך ולא-אני ושפתיך יענו-בך 6
Mdomo wako mwenyewe hukukukumu wewe, siyo wangu; hakika, midomo yako mwenyewe hushuhudia dhidi yako wewe.
הראישון אדם תולד ולפני גבעות חוללת 7
Je, wewe ni mwanadamu wa kwanza ambaye aliyezaliwa? Wewe ulikuwepo kabla ya vilima kuwepo?
הבסוד אלוה תשמע ותגרע אליך חכמה 8
Wewe Umewahi kusikia maarifa ya siri ya Mungu? Je, wewe wajihesabia mwenye hekima wewe mwenyewe?
מה-ידעת ולא נדע תבין ולא-עמנו הוא 9
Ni kitu gani unachokifahamu wewe ambacho sisi hatukijui? Ni kitu gani unachokifahamu wewe ambacho hakiko katika sisi?
גם-שב גם-ישיש בנו-- כביר מאביך ימים 10
Pamoja nasi wapo pia wenye mvi na watu wazee sana ambao ni wazee zaidi kuliko baba yako.
המעט ממך תנחומות אל ודבר לאט עמך 11
Je, faraja ya Mungu ni ndogo sana kwako, maneno ambayo ni ya upole dhidi yako wewe?
מה-יקחך לבך ומה-ירזמון עיניך 12
Kwa nini moyo wako wewe unakupeleka mbali? Kwa nini macho yako yananga'ra,
כי-תשיב אל-אל רוחך והצאת מפיך מלין 13
ili ya kwamba kuirejesha roho yako kwa Mungu na kuyatoa maneno hayo kutoka katika mdomo wako?
מה-אנוש כי-יזכה וכי-יצדק ילוד אשה 14
Je, mwanadamu yeye ni nini kwamba yeye anapaswa kuwa safi? Yeye mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ni nini kwamba yeye anapaswa awe mwenye haki?
הן בקדשו לא יאמין ושמים לא-זכו בעיניו 15
Tazama, Mungu haweki tumaini lake hata kwa mmoja wake aliye mtakatifu; Hakika, mbingu haziko safi machoni pake yeye;
אף כי-נתעב ונאלח איש-שתה כמים עולה 16
jinsi gani asivyo safi ni mmoja aliye mbaya na mla rushwa, mtu ambaye hunywa uovu kama maji!
אחוך שמע-לי וזה-חזיתי ואספרה 17
Mimi nitakuonyesha wewe; Nisikilize mimi; Mimi nitakutangazia wewe vitu ambavyo nimeviona,
אשר-חכמים יגידו ולא כחדו מאבותם 18
vitu ambavyo watu wenye hekima wamepita chini yake kutoka kwa baba zao, vile vitu ambavyo mababu zao hawakuvificha.
להם לבדם נתנה הארץ ולא-עבר זר בתוכם 19
Hawa walikuwa mababu zao, ambao kwao pekee nchi walipewa, na miongoni mwao hakuna mgeni aliyepita.
כל-ימי רשע הוא מתחולל ומספר שנים נצפנו לעריץ 20
Mtu mwovu hupitia katika maumivu siku zake zote, idadi ya miaka iliyowekwa juu kwa mtesaji kuteseka.
קול-פחדים באזניו בשלום שודד יבואנו 21
Sauti ya vitisho katika masikio yake; pindi yeye yuko katika kufanikiwa, mharibu atakuja juu yake yeye.
לא-יאמין שוב מני-חשך וצפו (וצפוי) הוא אלי-חרב 22
Yeye hafikiri kwamba yeye atarudi kutoka katika giza; Upanga humngojea yeye.
נדד הוא ללחם איה ידע כי-נכון בידו יום-חשך 23
Yeye huenda sehemu mbali mbali kwa ajili ya mkate, akisema, 'Kiko wapi? ' Yeye anatambua kuwa siku ya giza iko mkononi.
יבעתהו צר ומצוקה תתקפהו כמלך עתיד לכידור 24
Dhiki na mateso makali humfanya aogope; wao hushinda dhidi yake yeye, kama mfalme tayari kwa vita.
כי-נטה אל-אל ידו ואל-שדי יתגבר 25
Kwa sababu yeye ameunyosha mkono wake dhidi ya Mungu na ameishi kwa kiburi dhidi ya aliye mkuu,
ירוץ אליו בצואר בעבי גבי מגניו 26
huyu mtu mwovu hukimbia kwa Mungu na shingo ngumu, kwa vifundo vikubwa vya ngao.
כי-כסה פניו בחלבו ויעש פימה עלי-כסל 27
Hii ni kweli, hata ingawa yeye amefunika uso wake kwa mafuta yake na amekusanya mafuta juu ya viuno vyake,
וישכון ערים נכחדות--בתים לא-ישבו למו אשר התעתדו לגלים 28
na ameishi katika miji yenye ukiwa; katika nyumba ambazo hakuna mwanadamu anayeishi humo sasa na ambazo zilikuwa tayari kuwa magofu.
לא-יעשר ולא-יקום חילו ולא-יטה לארץ מנלם 29
Yeye hatakuwa tajiri; utajiri wake yeye hautadumu; hata kivuli chake hakitadumu katika nchi.
לא-יסור מני-חשך--ינקתו תיבש שלהבת ויסור ברוח פיו 30
Yeye hatatoka nje ya giza; mwali wa moto utakausha matawi yake; katika pumzi ya kinywa cha Mungu yeye ataenda zake.
אל-יאמן בשו נתעה כי-שוא תהיה תמורתו 31
Mwacheni yeye asitumaini katika vitu visivyofanya kazi, akijidanganya yeye mwenyewe; maana upuuzi utakuwa mshahara wake yeye.
בלא-יומו תמלא וכפתו לא רעננה 32
Itatokea kabla ya wakati wake yeye atapaswa kufa; tawi lake halitakuwa kijani.
יחמס כגפן בסרו וישלך כזית נצתו 33
Yeye atazipukutisha zabibu zake zisizovunwa kama mzabibu; yeye atayaondoa maua yake kama mti wa mzeituni.
כי-עדת חנף גלמוד ואש אכלה אהלי-שחד 34
Kwa maana msaada wa watu wasiomcha Mungu utakuwa tasa; moto utateketeza hema za rushwa.
הרה עמל וילד און ובטנם תכין מרמה 35
Wao wanabeba mimba yenye ubaya na kuzaa uovu; tumbo lao hutunga mimba ya udanganifu.

< איוב 15 >