< ירמיה 20 >
וישמע פשחור בן אמר הכהן והוא פקיד נגיד בבית יהוה את ירמיהו נבא את הדברים האלה | 1 |
Pashuri, mwana wa Imeri, kuhani, alikuwa msimamizi mkuu, akamsikia Yeremia akihubiri maneno haya mbele ya nyumba ya Bwana.
ויכה פשחור את ירמיהו הנביא ויתן אתו על המהפכת אשר בשער בנימן העליון אשר בבית יהוה | 2 |
Basi Pashuri akampiga nabii Yeremia, akamtia katika masanduku yaliyokuwa kwenye lango la juu la Benyamini ndani ya nyumba ya Bwana.
ויהי ממחרת ויצא פשחור את ירמיהו מן המהפכת ויאמר אליו ירמיהו לא פשחור קרא יהוה שמך--כי אם מגור מסביב | 3 |
Ikawa siku ya pili Pashuri akamtoa Yeremia nje ya makabati. Yeremia akamwambia, “Bwana hakukuita Pashuri, lakini wewe ni Magor-Misabibu.
כי כה אמר יהוה הנני נתנך למגור לך ולכל אהביך ונפלו בחרב איביהם--ועיניך ראות ואת כל יהודה אתן ביד מלך בבל והגלם בבלה והכם בחרב | 4 |
Kwa maana Bwana asema hivi, 'Tazama, nitakufanya kuwa kitu cha kutisha, wewe na wapendwa wako wote; kwa maana wataanguka kwa upanga wa adui zao, na macho yako yataona. Nitawatia Yuda mkononi mwa mfalme wa Babeli. Atawafanya kuwa mateka huko Babeli au kuwaangamiza kwa upanga.
ונתתי את כל חסן העיר הזאת ואת כל יגיעה ואת כל יקרה ואת כל אוצרות מלכי יהודה אתן ביד איביהם ובזזום ולקחום והביאום בבלה | 5 |
Nitampa mali zote za jiji hili na utajiri wake wote, vitu vyote vya thamani na hazina zote za wafalme wa Yuda. Nitaweka vitu hivi mikononi mwa adui zako, nao watawakamata. Nao watawachukua na kuwaleta Babeli.
ואתה פשחור וכל ישבי ביתך תלכו בשבי ובבל תבוא ושם תמות ושם תקבר--אתה וכל אהביך אשר נבאת להם בשקר | 6 |
Lakini wewe Pashuri, na wenyeji wote wa nyumba yako watakwenda mateka. Utakwenda Babeli na kufa huko. Wewe na wapendwa wako wote ambao uliwatabiria maneno ya uongo mtazikwa huko.'”
פתיתני יהוה ואפת חזקתני ותוכל הייתי לשחוק כל היום כלה לעג לי | 7 |
“Umenidanganya, Bwana. Kwa hakika nimedanganyika. Wewe ulinikamata na kunishinda. Nimekuwa kitu cha kuchekesha. Watu wananidharau kila siku, siku zote.
כי מדי אדבר אזעק חמס ושד אקרא כי היה דבר יהוה לי לחרפה ולקלס כל היום | 8 |
Kwa maana wakati wowote nimenena, nimeita na kutangaza, 'Vurugu na uharibifu.' Na neno la Bwana limefanywa shutumu na dhihaka kwangu kila siku.
ואמרתי לא אזכרנו ולא אדבר עוד בשמו והיה בלבי כאש בערת עצר בעצמתי ונלאיתי כלכל ולא אוכל | 9 |
Nami nikisema, 'Sitafikiria juu ya Bwana tena. Sitatangaza tena jina lake.' Ni kama moto moyoni mwangu, uliofanyika ndani ya mifupa yangu. Kwa hiyo ninajitahidi kustahimili lakini siwezi.
כי שמעתי דבת רבים מגור מסביב הגידו ונגידנו כל אנוש שלמי שמרי צלעי אולי יפתה ונוכלה לו ונקחה נקמתנו ממנו | 10 |
Nimesikia habari za ugaidi kutoka kwa watu wengi pande zote. 'Mshitaki! Lazima tumshitaki' Wale walio karibu nami kuangalia kama nitaanguka. 'Labda anaweza kudanganywa. Ikiwa ndivyo, tunaweza kumshinda na kujilipiza kisasi kwake.'
ויהוה אותי כגבור עריץ על כן רדפי יכשלו ולא יכלו בשו מאד כי לא השכילו כלמת עולם לא תשכח | 11 |
Lakini Bwana yu pamoja nami kama mpiganaji mwenye nguvu, hivyo wale wanaonifuata watajikwaa. Hawatanishinda. Watakuwa na aibu sana, kwa sababu hawatafanikiwa. Watakuwa na aibu ya kudumu, haitasahauliwa kamwe.
ויהוה צבאות בחן צדיק ראה כליות ולב אראה נקמתך מהם כי אליך גליתי את ריבי | 12 |
Lakini wewe, Bwana wa majeshi, wewe unayemtazama wenye haki na ambaye huona akili na moyo. Hebu nipate kuona kisasi chako juu yao kwa maana nimekuletea shitaka langu kwako.
שירו ליהוה--הללו את יהוה כי הציל את נפש אביון מיד מרעים | 13 |
Mwimbieni Bwana! Msifuni Bwana! Kwa kuwa ameokoa maisha ya wale waliokandamizwa kutoka kwenye mikono ya waovu.
ארור היום אשר ילדתי בו יום אשר ילדתני אמי אל יהי ברוך | 14 |
Na ilaaniwe siku niliyozaliwa. Usiruhusu siku ambayo mama yangu alinizaa ibarikiwe.
ארור האיש אשר בשר את אבי לאמר ילד לך בן זכר--שמח שמחהו | 15 |
Na alaaniwe mtu aliyemwambia baba yangu akisema, 'Amezaliwa mtoto wa kiume,' na kusababisha furaha kubwa.
והיה האיש ההוא כערים אשר הפך יהוה ולא נחם ושמע זעקה בבקר ותרועה בעת צהרים | 16 |
Mtu huyo atakuwa kama miji ambayo Bwana aliiangamiza bila huruma. Na asikie wito wa msaada asubuhi na sauti ya vita wakati wa mchana.
אשר לא מותתני מרחם ותהי לי אמי קברי ורחמה הרת עולם | 17 |
Hiyo itatokea, kwa kuwa Bwana hakuniua tumboni au kumfanya mama yangu kaburi langu, tumbo la ujauzito milele.
למה זה מרחם יצאתי לראות עמל ויגון ויכלו בבשת ימי | 18 |
Kwa nini nilitoka tumboni ili kuona matatizo na uchungu, ili siku zangu zijazwe na aibu?”