< ירמיה 11 >

הדבר אשר היה אל ירמיהו מאת יהוה לאמר 1
Hili ndilo neno lililojia Yeremia kutoka kwa Bwana, akasema,
שמעו את דברי הברית הזאת ודברתם אל איש יהודה ועל ישבי ירושלם 2
“Sikiliza maneno ya agano hili, uwaambie kila mtu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu.
ואמרת אליהם כה אמר יהוה אלהי ישראל ארור האיש--אשר לא ישמע את דברי הברית הזאת 3
Uwaambie, 'Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: na alaaniwe yeyote asiyesikiliza maneno ya agano hili.
אשר צויתי את אבותיכם ביום הוציאי אותם מארץ מצרים מכור הברזל לאמר שמעו בקולי ועשיתם אותם ככל אשר אצוה אתכם והייתם לי לעם ואנכי אהיה לכם לאלהים 4
Hili ndilo agano nililowaamuru baba zenu walishike siku nilipowatoa kutoka katika nchi ya Misri, kutoka tanuru ya chuma. Nikawaambia, “Sikilizeni sauti yangu na mfanye mambo yote kama nilivyowaamuru, kwa kuwa mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu.”
למען הקים את השבועה אשר נשבעתי לאבותיכם לתת להם ארץ זבת חלב ודבש--כיום הזה ואען ואמר אמן יהוה 5
Nisikilizeni ili nipate kukitimiza kiapo nilichoapa kwa baba zenu, kiapo kwamba nitawapa nchi iliyojaa maziwa na asali kama ilivyo leo.'” Kisha mimi Yeremia nikajibu na kusema, “Ndio, Bwana!”
ויאמר יהוה אלי קרא את כל הדברים האלה בערי יהודה ובחצות ירושלם לאמר שמעו את דברי הברית הזאת ועשיתם אותם 6
Bwana akaniambia, “Hubiri habari hizi yote katika miji ya Yuda, na katika njia za Yerusalemu. Sema, “Sikilizeni maneno ya agano hili na mkayafanye.
כי העד העדתי באבותיכם ביום העלותי אותם מארץ מצרים ועד היום הזה השכם והעד לאמר שמעו בקולי 7
Kwa maana nimewaagiza wazee wenu tangu siku ile niliyowaleta kutoka nchi ya Misri hadi wakati huu wa sasa, nimewaonya mara kwa mara na kusema, “Sikilizeni sauti yangu.'”
ולא שמעו ולא הטו את אזנם וילכו איש בשרירות לבם הרע ואביא עליהם את כל דברי הברית הזאת אשר צויתי לעשות--ולא עשו 8
Lakini hawakusikiliza au wala kutega masikio yao. Kila mtu amekuwa akitembea katika ukaidi wa moyo wake mbaya. Kwa hiyo nilileta laana zote katika agano hili nililoamuru kuja juu yao. Lakini watu bado hawakuitii.”
ויאמר יהוה אלי נמצא קשר באיש יהודה ובישבי ירושלם 9
Kisha Bwana akaniambia, “Njama imeonekana kati ya watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu.
שבו על עונת אבותם הראשנים אשר מאנו לשמוע את דברי והמה הלכו אחרי אלהים אחרים לעבדם הפרו בית ישראל ובית יהודה את בריתי אשר כרתי את אבותם 10
Wameugeukia uovu wa mababu zao wa mwanzo, ambao walikataa kusikiliza neno langu, ambao badala yake walifuata miungu mingine ili kuabudu. Waisraeli na nyumba ya Yuda walivunja agano langu nililoweka na baba zao.
לכן כה אמר יהוה הנני מביא אליהם רעה אשר לא יוכלו לצאת ממנה וזעקו אלי ולא אשמע אליהם 11
Kwa hiyo Bwana asema hivi, 'Tazameni, nitawaletea majanga juu yao, majanga ambayo hawataweza kuyaepuka. Ndipo wataniita, lakini sitawasikiliza.
והלכו ערי יהודה וישבי ירושלם וזעקו אל האלהים אשר הם מקטרים להם והושע לא יושיעו להם בעת רעתם 12
Miji ya Yuda na wenyeji wa Yerusalemu watakwenda na kuiita miungu ambayo walitoa sadaka, lakini hakika hawatawaokoa wakati wa majanga yao.
כי מספר עריך היו אלהיך יהודה ומספר חצות ירושלם שמתם מזבחות לבשת--מזבחות לקטר לבעל 13
Kwa kuwa idadi ya miungu yako ewe Yuda imeongezeka sawa na idadi ya miji yako. Na umefanya idadi ya madhabahu ya aibu huko Yerusalemu, madhabahu ya kufukiza uvumba kwa Baali, sawa na idadi ya njia zake.
ואתה אל תתפלל בעד העם הזה ואל תשא בעדם רנה ותפלה כי אינני שמע בעת קראם אלי--בעד רעתם 14
Kwa hiyo wewe mwenyewe, Yeremia, usiwaombee watu hawa. Lazima usiomboleze au kuomba kwa niaba yao. Kwa maana siwezi kusikiliza wakati wananiita katika majanga yao.
מה לידידי בביתי עשותה המזמתה הרבים ובשר קדש יעברו מעליך כי רעתכי אז תעלזי 15
Mpendwa wangu anafanya nini nyumbani kwangu, ikiwa amekuwa na nia mbaya? Nyama za sadaka yako hazitakusaidia. Unafurahi kwa sababu ya matendo yako mabaya.
זית רענן יפה פרי תאר קרא יהוה שמך--לקול המולה גדלה הצית אש עליה ורעו דליותיו 16
Katika siku za nyuma Bwana alikuita mti wa mzeituni wenye majani, mzuri wenye matunda mazuri. Lakini atawasha moto juu yake ambayo itaonekana kama sauti ya dhoruba; matawi yake yatavunjika.
ויהוה צבאות הנוטע אותך דבר עליך רעה בגלל רעת בית ישראל ובית יהודה אשר עשו להם להכעסני--לקטר לבעל 17
Kwa maana Bwana wa majeshi, aliyekua amekusudia maafa juu yako, kwa sababu ya matendo mabaya ambayo nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda wamefanya-wamenikasirisha kwa kumtolea Baali sadaka.'”
ויהוה הודיעני ואדעה אז הראיתני מעלליהם 18
Bwana alinijulisha mambo haya, kwa hiyo nakayajua. Wewe, Bwana, umenifanya nione matendo yao.
ואני ככבש אלוף יובל לטבוח ולא ידעתי כי עלי חשבו מחשבות נשחיתה עץ בלחמו ונכרתנו מארץ חיים--ושמו לא יזכר עוד 19
Nilikuwa kama kondoo mpole unayeongozwa na mchinjaji. Sikujua kwamba walikuwa wameunda mipango dhidi yangu, “Hebu tuangamize mti na matunda yake! Hebu tumkatilie mbali na nchi ya walio hai ili jina lake lisikumbukwe tena.
ויהוה צבאות שפט צדק בחן כליות ולב אראה נקמתך מהם כי אליך גליתי את ריבי 20
Lakini Bwana wa majeshi ndiye mwamuzi mwenye haki ambaye huchunguza moyo na akili. Mimi nitashuhudia kisasi chako dhidi yao, kwa kuwa nimekuletea kesi yangu kwako.
לכן כה אמר יהוה על אנשי ענתות המבקשים את נפשך לאמר לא תנבא בשם יהוה ולא תמות בידנו 21
Kwa hiyo Bwana asema hivi juu ya watu wa Anathothi, wanaotafuta uhai wako, “wanasema, 'Usifanye unabii kwa jina la Bwana, usije utakufa kwa mkono wetu.'
לכן כה אמר יהוה צבאות הנני פקד עליהם הבחורים ימתו בחרב בניהם ובנותיהם ימתו ברעב 22
Kwa hiyo Bwana wa majeshi asema hivi, 'Tazameni, nitawaadhibu. Vijana wao wenye nguvu watakufa kwa upanga. Wana wao na binti zao watakufa kwa njaa.
ושארית לא תהיה להם כי אביא רעה אל אנשי ענתות שנת פקדתם 23
Hakuna hata mmoja atakayeachwa, kwa maana nitaleta maafa dhidi ya watu wa Anathothi, mwaka wa adhabu yao.'”

< ירמיה 11 >