< ישעה 36 >

ויהי בארבע עשרה שנה למלך חזקיהו עלה סנחריב מלך אשור על כל ערי יהודה הבצרות--ויתפשם 1
Katika mwaka wa kumi na nne wa mfalme Hezekia, Senacherebi, mfalme wa Asiria, alivamia miji yote ya Yuda na kuwakamata.
וישלח מלך אשור את רבשקה מלכיש ירושלמה אל המלך חזקיהו בחיל כבד ויעמד בתעלת הברכה העליונה במסלת שדה כובס 2
Halafu mfalme wa Asiria akamtuma kamanda mkuu na jeshi kubwa kutoka Lachishi mpaka Yerusalemu kwa mfalme Hezekia. Alipofika kwenye mfereji katika kisima cha juu, katika njia kuu na katika shamba la dobi na akasimama pale.
ויצא אליו אליקים בן חלקיהו אשר על הבית--ושבנא הספר ויואח בן אסף המזכיר 3
Maofisa wa Israeli waliotumwa kuzungumza nao walikuwa ni Eliakimu mtoto wa Hilkia, kiongozi wa jumba, Shebna katibu wa mfalme, na Joa mtoto wa Asapha, anayeandika makubaliano ya serekali.
ויאמר אליהם רבשקה אמרו נא אל חזקיהו כה אמר המלך הגדול מלך אשור מה הבטחון הזה אשר בטחת 4
Kamanda mkuu wa jeshi akawaambia wao, ''Mwambieni Hezekia kwamba mfalme mkuu, mfalme Asiria, asema, 'Nini chanzo cha ujasiri wako?
אמרתי אך דבר שפתים עצה וגבורה למלחמה עתה על מי בטחת כי מרדת בי 5
Unaongea maneno yasiyo na maana tu, nasema kama kuna shauri na nguvu za vita. Sasa ni nani unayemuamini? na ni nani aliyekupa ujasiri wa kuniasi mimi.
הנה בטחת על משענת הקנה הרצוץ הזה על מצרים אשר יסמך איש עליו ובא בכפו ונקבה כן פרעה מלך מצרים לכל הבטחים עליו 6
Tazama, umeweka imani yako Misri, maana banzi la mwanzi unalolitumia kama fimbo ya kutembelea, ikiwa mtu ataiegemea na kuishika kwenye mkono wake itamchoma. Hivyo ndovyo jinsi Farao mfalme wa Misri alivyo kwa yeyote anayemuamini.
וכי תאמר אלי אל יהוה אלהינו בטחנו הלוא הוא אשר הסיר חזקיהו את במתיו ואת מזבחתיו ויאמר ליהודה ולירושלם לפני המזבח הזה תשתחוו 7
Lakini ikiwa utasema nami, ''Tunamwamini Yahwe Mungu wetu,''Je sio yeye ambaye Hezekia ameondosha mahali palipoinuka na madhebau, asema kwa Yuda na Yerusalemu, ''Lazima tuabudu mbele ya madhebau hii katika Yerusalemu''?
ועתה התערב נא את אדני המלך אשור ואתנה לך אלפים סוסים--אם תוכל לתת לך רכבים עליהם 8
Hivyo sasa, nataka kukufanya wewe kuwa zawadi nzuri kwa Bwana mfalme Asiria. Nitakupa farasi elfu mbili, kama utaweza kuwatafutia dereva.
ואיך תשיב את פני פחת אחד עבדי אדני--הקטנים ותבטח לך על מצרים לרכב ולפרשים 9
Ni kwa jinsi gani unaweza kumpinga moja kati ya nahodha aliye mdogo katika watumishi wa Bwana wangu? Mmeweka imani yenu Misri katika gari na farasi!
ועתה המבלעדי יהוה עליתי על הארץ הזאת להשחיתה יהוה אמר אלי עלה אל הארץ הזאת והשחיתה 10
Halafu sasa, Je nimewezaje kusafiri mpaka hapa pasipo Yahwe kupigana dhidi ya nchi hii na kuhiaribu? Yahwe asema nami, Vamia nchi hii na uhiharibu.
ויאמר אליקים ושבנא ויואח אל רבשקה דבר נא אל עבדיך ארמית--כי שמעים אנחנו ואל תדבר אלינו יהודית באזני העם אשר על החומה 11
Halafu Eliakimu mtoto wa Hilkia, na Shebna na Joa asema kwa kamanda mkuu, Tafadhali zungumza na watu wako kwa lugha ya kiashuru, maana kiashuru tunakielewa. Usiongee na sisi kwa lugha kiyahudi katika masikio ya watu ambao wako ukutani.''
ויאמר רבשקה האל אדניך ואליך שלחני אדני לדבר את הדברים האלה הלא על האנשים הישבים על החומה לאכל את חראיהם (צואתם) ולשתות את שיניהם (מימי רגליהם) עמכם 12
Lakini kamanda mkuu akasema, ''Je bwana wenu ametuma kwa bwana wako na kuzungumza haya maneno? Je hajanituma kwa watu walio kaa kwenye ukuta, ili wale kinyesi chaao mwenyewe na kunywa mkojo waomwenyewe?
ויעמד רבשקה ויקרא בקול גדול יהודית ויאמר--שמעו את דברי המלך הגדול מלך אשור 13
Halafu kamanda mkuu akasimama na kupiga kelele kwa sauti kubwa kwa lugha ya kiyahudi, na akisema,
כה אמר המלך אל ישא לכם חזקיהו כי לא יוכל להציל אתכם 14
''Mfalme asema, ' Msimruhusu Hezekia awadanganye ninyi, maana hataweza kuwaokoa ninyi.
ואל יבטח אתכם חזקיהו אל יהוה לאמר הצל יצילנו יהוה לא תנתן העיר הזאת ביד מלך אשור 15
Msimruhusu Hezekia awafanye muumuamini Yahwe, Nawambieni Hakika Yahwe atatukomboa sisi; mjii huu hautachukuliwa na mfalme wa Asiria.''
אל תשמעו אל חזקיהו כי כה אמר המלך אשור עשו אתי ברכה וצאו אלי ואכלו איש גפנו ואיש תאנתו ושתו איש מי בורו 16
Msimsikilize Hezekia, maana hivi ndivyo mfalme wa Asiria anavyosema: 'Fanyeni amani na mimi na mje kwangu. Halafu kila mmoja wenu atakula kwenye mzabibu wake mwenyewe na tunda la mti wake mwenyewe, na kunjwa maji ya kisima chake mwenyewe.
עד באי ולקחתי אתכם אל ארץ כארצכם ארץ דגן ותירוש ארץ לחם וכרמים 17
Mtafanya hivi mpaka nije kuwachukua na kuwapeleka kwenye nchi kama ya kwenu. nchi ya mavuno na mvinyo mpya, nchi ya mkate na shamba.
פן יסית אתכם חזקיהו לאמר יהוה יצילנו ההצילו אלהי הגוים איש את ארצו מיד מלך אשור 18
Msimruhusu Hezekia awapotoshe nyie, akisema, Yahwe atatuokoa nyie; Je kuna miungu ya aina yeyote ya watu iliyowakomboa kutoka mikononi mwa mfalme wa Asiria?
איה אלהי חמת וארפד--איה אלהי ספרוים וכי הצילו את שמרון מידי 19
Wako wapi miungu wa Hamathi na Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu? Je wameikomboa Samaria kutoka kwenye nguvu zangu?
מי בכל אלהי הארצות האלה אשר הצילו את ארצם מידי כי יציל יהוה את ירושלם מידי 20
Miongoni mwa miungu yote ya nchi hii, Je kuna miungu ya aina yeyote iliyoikomboa nchi yao kutoka kwenye nguvu yangu, ni kama Yahwe anaweza kuawokoa Yerusalemu kutoka kwenye nguvu yangu?''
ויחרישו ולא ענו אתו דבר כי מצות המלך היא לאמר לא תענהו 21
Lakini watu wanabaki kimya na hawataki kujibu, maana amri ya mfalme ilikuwa, ''Msimjibu''.
ויבא אליקים בן חלקיהו אשר על הבית ושבנא הספר ויואח בן אסף המזכיר אל חזקיהו--קרועי בגדים ויגידו לו את דברי רבשקה 22
Halafu Eliakimu mtoto wa Hilkia, yeye aliye juu ya kaya, Shebna mwandishi, na Joa mtoto wa Asafu, na mtunza kumbukumbu, walikuja kwa Hezekia na nguo zilizotoboka na wakapeleka maneno ya kamanda mkuu.

< ישעה 36 >