< ישעה 33 >

הוי שודד ואתה לא שדוד ובוגד ולא בגדו בו כהתמך שודד תושד כנלתך לבגד יבגדו בך 1
Ole wenu, waharibifu ambao hamjaharibiwa! Ole wao wasaliti ambao hamjaslitiwa! Pindi mtakapoacha uaribifu, nanyi mtaharibiwa. Pindi mtakapoacha usaliti, nayi mtasalitiwa.
יהוה חננו לך קוינו היה זרעם לבקרים אף ישועתנו בעת צרה 2
Yahwe, tuurumie sisi; tumekusubiri wewe; umekuwa mkono wetu kila asubuhi, na wokovu wetu katika kipindi cha mateso.
מקול המון נדדו עמים מרוממתך נפצו גוים 3
Watu wamekimbia kwa kusikia sauti kubwa; uliponyanyuka, mataifa yametawanyika,
ואסף שללכם אסף החסיל--כמשק גבים שקק בו 4
Mateka wako wamejikusanya kama mkasanyiko wa nzige; kama nzige warukavyo, watu wataruka juu yake.
נשגב יהוה כי שכן מרום מלא ציון משפט וצדקה 5
Yahwe ameinuliwa. Anaishi mahali pa juu. Ataijaza Sayuni kwa haki na usawa.
והיה אמונת עתיך חסן ישועת חכמת ודעת יראת יהוה היא אוצרו 6
Atakuwa imara katika kipidi chenu, wingi wa wokovu, busara, na maarifa; hofu ya Yahwe iko katika hazina yake.
הן אראלם צעקו חצה מלאכי שלום מר יבכיון 7
Tazama, wujumbe wanalia mtaani; wanadiplomasia wanamatumaini ya amani kwa kulia kwa uchungu.
נשמו מסלות שבת עבר ארח הפר ברית מאס ערים לא חשב אנוש 8
Barabara kuu imeachwa faragha; hakuna wasafiri tena. Maagano yamevujika, mashahidi wanadharaulika, na utu wa mtu hauheshimiki.
אבל אמללה ארץ החפיר לבנון קמל היה השרון כערבה ונער בשן וכרמל 9
Nchi imeomboleza na kunyaukia mbali; Lebanoni inaibisha na kunyaukia mbali; Sharoni imekuwa kama jangwa wazi; Bashani na Kermeli zimepuputisha majani yake.
עתה אקום יאמר יהוה עתה ארומם--עתה אנשא 10
''Sasa nitanyanyuka, ''asema Yahwe; '' sasa nitanyanyuliwa juu; sasa nitainuliwa.
תהרו חשש תלדו קש רוחכם אש תאכלכם 11
Utashika mimba ya makapi na utazaa mabua; na punzi yako ni moto ambao utakuunguza wewe.
והיו עמים משרפות שיד קוצים כסוחים באש יצתו 12
Watu watachomwa na kuwa kama chokaa, kama miiba ya porini inavyokatwa na kuchomwa.
שמעו רחוקים אשר עשיתי ודעו קרובים גברתי 13
Enyi mlio mbali sana, sikiliza nilicho kifanya; na enyi mlio karibu, kirini ukuu wangu.''
פחדו בציון חטאים אחזה רעדה חנפים מי יגור לנו אש אוכלה--מי יגור לנו מוקדי עולם 14
Watenda zambi wa Sayuni wanogopa; tetemeko limewakuta wasio na Mungu. Ni nani miongoni mwetu anayeweza kukaa kwenye moto mkali? Na ni nani miongoni mwetu anayeweza kukaa kwenye moto wa milele?
הלך צדקות ודבר מישרים מאס בבצע מעשקות נער כפיו מתמך בשחד אטם אזנו משמע דמים ועצם עיניו מראות ברע 15
Nyie mnaotembe katika haki na kuongea kw uaminifu; yeye anayedharau mapato ya ukandamizaji, yeye anayekataa kuchuka rushwa, ambaye hausiki kwenye kupanga vurugu za kihalifu, na ambaye haangali maovu-
הוא מרומים ישכן מצדות סלעים משגבו לחמו נתן מימיו נאמנים 16
Ataiweka nyumba yake juu; sehemu yake ya ulinzi itakuwa ni ngome ya mwamba; chakula na maji yake hayataisha.
מלך ביפיו תחזינה עיניך תראינה ארץ מרחקים 17
Macho yako yatamuona mfalme katika uzuri wake; watatazama nchi kubwa.
לבך יהגה אימה איה ספר איה שקל איה ספר את המגדלים 18
Moyo wako utakumbuka hofu; yuko wapi mwandishi, yuko wapi yule aliayepima pesa? na yuko wapi yeye aesabue minara?
את עם נועז לא תראה עם עמקי שפה משמוע נלעג לשון אין בינה 19
Hautawaona watu wanaopinga, watu weye lugha ya ajabu ambayo hautaweza kuielewa.
חזה ציון קרית מועדנו עיניך תראינה ירושלם נוה שאנן אהל בל יצען בל יסע יתדתיו לנצח וכל חבליו בל ינתקו 20
Itazame Sayuni, mji wa sikukuu yetu; macho yako yataiona Yerusalemu kama makao tulivu, hema ambalo halitatolewa, vigingi vyake havitatolewa wala kamba zake hazitakatika.
כי אם שם אדיר יהוה לנו מקום נהרים יארים רחבי ידים בל תלך בו אני שיט וצי אדיר לא יעברנו 21
Badala yake Yahwe katika ukuu wake atakuwa pamoja na sisi, katika eneo la maji mengi na mifereji mingi. Hakuna manuari na mpiga makasia watakayepita hapo, na hakuna mashua itakayopita uko.
כי יהוה שפטנו יהוה מחקקנו יהוה מלכנו הוא יושיענו 22
Maana Yahwe ni hakimu wetu, Yahwe ni mwanasheria wet, Yahwe ni mfalme wetu; atatukomboa sisi.
נטשו חבליך בל יחזקו כן תרנם בל פרשו נס אז חלק עד שלל מרבה פסחים בזזו בז 23
Kamba zako zimelegea; haziwezi kushika mlingoti katika eneo lake; haziwezi kuzunguka meli; pindi mateka wanavyogawanyika, hata vilema watawatoa nje kama mateka.
ובל יאמר שכן חליתי העם הישב בה נשא עון 24
Na wenyeji watasema, ''Ninaumwa;'' watu wanaoishi pale watasamehewa maovu yao.

< ישעה 33 >