< ישעה 16 >
שלחו כר משל ארץ מסלע מדברה אל הר בת ציון | 1 |
Mpeleke mwana kondoo kuongoza nchi kutoka Sela huko jangwani, kwenye mlima wa binti Sayuni.
והיה כעוף נודד קן משלח--תהיינה בנות מואב מעברת לארנון | 2 |
Kama ndege wazururao, viota vimetapakaa, hivyo basi wanawake wa Moabu watavuka kwenye mto Arnoni.
הביאו (הביאי) עצה עשו פלילה שיתי כליל צלך בתוך צהרים סתרי נדחים--נדד אל תגלי | 3 |
Toa maelekezo, tekeleza haki; toa kivuli kama usiku wakati wa mchana; wahifadhi watuhumiwa; msiwahini watuhumiwa.
יגורו בך נדחי מואב הוי סתר למו מפני שודד כי אפס המץ כלה שד תמו רמס מן הארץ | 4 |
Waache waishi miongoni mwenu, wakimbizi kutoka Moabu; muwe mahali pakujifichia wao wasiangamizwe.'' maana mateso yatakwisha, na uharibifu utapungua utakuwa na kikomo, wale wanotetemeka watapotea katika nchi.
והוכן בחסד כסא וישב עליו באמת באהל דוד שפט ודרש משפט ומהר צדק | 5 |
Kiti cha enzi kitaanzishwa katika agano la uaminifu; na mmoja katika hema la Daudi atakaa pale kwa uaminifu. Atahukumu kwa kufuata haki na atatenda haki.
שמענו גאון מואב גא מאד גאותו וגאונו ועברתו לא כן בדיו | 6 |
Tumesikia kiburi cha Moabu, kiburi chake, majivuno yake, na hasira yake. Lakini majivuno yake ni maneno tu.
לכן ייליל מואב למואב--כלה ייליל לאשישי קיר חרשת תהגו אך נכאים | 7 |
Hivyo basi Moabu atalia juu ya Moabu-wote watalia! wataomboleza, nyie mlioharibiwa kabisa, mikate ya Kira Haresethi.
כי שדמות חשבון אמלל גפן שבמה בעלי גוים הלמו שרוקיה--עד יעזר נגעו תעו מדבר שלחותיה נטשו עברו ים | 8 |
Shamba la Heshboni limekauka kabisa pamoja na mizabibu ya Sibma. Kiongozi wa mataifa amekanyaga mizabibu iliyochaguliwa na kuelekea Jazeri na kuelekea jangwani. Mizizi yake nje ya nchi; imenda juu ya bahari.
על כן אבכה בבכי יעזר גפן שבמה אריוך דמעתי חשבון ואלעלה כי על קיצך ועל קצירך הידד נפל | 9 |
Kweli nitalia pamoja Jazeri kwasababu ya shamba la mizabibu la Sibma. Nitakuloanisha kwa machozi yangu, Heshboni, na Eleale. Maana katika mashamba yenu kipindi cha majira ya joto matunda na mazao nitaishia kwa kupiga kelele za furaha.
ונאסף שמחה וגיל מן הכרמל ובכרמים לא ירנן לא ירעע יין ביקבים לא ידרך הדרך--הידד השבתי | 10 |
Furaha na shangwe zimezimwa na matunda ya miti ya shambani; na hakuna nyimbo wala kelele katika mashamba ya mizabibu, maana nimeweka mwisho wa kupiga kelele kwa yeyote anayetembea.
על כן מעי למואב ככנור יהמו וקרבי לקיר חרש | 11 |
Hivyo, moyo wangu unalia kama kinubi, na ndani yangu maana kwa ajili ya Kiri Hareseth.
והיה כי נראה כי נלאה מואב על הבמה ובא אל מקדשו להתפלל ולא יוכל | 12 |
Pindi ambapo Moabu wamejivika mahali pa juu, na kuingia katika hekalu kuomba, maombi yake hayatatimiza chochote.
זה הדבר אשר דבר יהוה אל מואב--מאז | 13 |
Haya ndio maneno aliyoyazungumza Yahwe kuhusu Moabu iliyopita.
ועתה דבר יהוה לאמר בשלש שנים כשני שכיר ונקלה כבוד מואב בכל ההמון הרב ושאר מעט מזער לוא כביר | 14 |
Tena Yahwe amesema, ''Ndani ya miaka mitatu utukufuwa Moabu utatoweka; japo watu wake wengi, watakao bakia ni wachache, na wasionafaida.