< בראשית 25 >

ויסף אברהם ויקח אשה ושמה קטורה 1
Abraham akaoa mke mwingine; jina lake aliitwa Ketura.
ותלד לו את זמרן ואת יקשן ואת מדן ואת מדין--ואת ישבק ואת שוח 2
Akamzalia Zimrani, Jokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Shua.
ויקשן ילד את שבא ואת דדן ובני דדן היו אשורם ולטושם ולאמים 3
Jokshani akamzaa Sheba na Dedani. Wana wa Dedani walikuwa ni Waashuru, Waletushi, na Waleumi.
ובני מדין עיפה ועפר וחנך ואבידע ואלדעה כל אלה בני קטורה 4
Wana wa Midiani walikuwa ni Efa, Eferi, Hanoki, Abida, na Eldaa. Hawa wote walikuwa ni wana wa Ketura.
ויתן אברהם את כל אשר לו ליצחק 5
Abraham akampatia Isaka vitu vyote alivyokuwa navyo.
ולבני הפילגשים אשר לאברהם נתן אברהם מתנת וישלחם מעל יצחק בנו בעודנו חי קדמה אל ארץ קדם 6
Ingawaje, wakati alipokua angali akiishi, aliwapatia zawadi wana wa masuria wake na kuwapeleka katika nchi ya mashariki, mbali na Isaka, mwanae.
ואלה ימי שני חיי אברהם--אשר חי מאת שנה ושבעים שנה וחמש שנים 7
Hizi ndizo zilikuwa siku za miaka ya uhai wake Abraham alizoishi, miaka 175.
ויגוע וימת אברהם בשיבה טובה זקן ושבע ויאסף אל עמיו 8
Abraham akapumua pumzi ya mwisho na akafa katika uzee mwema, mzee aliye shiba siku, na akakusanywa kwa watu wake.
ויקברו אתו יצחק וישמעאל בניו אל מערת המכפלה אל שדה עפרן בן צחר החתי אשר על פני ממרא 9
Isaka na Ishmaili, wanae wakamzika katika pango la Makipela, katika shamba la Efron mwana wa Soari Mhiti, pango lililokuwa karibu na Mamre.
השדה אשר קנה אברהם מאת בני חת--שמה קבר אברהם ושרה אשתו 10
Shamba hili Abraham alilinunua kwa watoto wa Hethi. Abraham akazikwa pale pamoja na Sara mkewe.
ויהי אחרי מות אברהם ויברך אלהים את יצחק בנו וישב יצחק עם באר לחי ראי 11
Baada ya kifo cha Abraham, Mungu akambariki Isaka mwanae, na Isaka akaishi karibu na Beerlalahairoi.
ואלה תלדת ישמעאל בן אברהם אשר ילדה הגר המצרית שפחת שרה--לאברהם 12
Na sasa hawa ndio walikuwa wana wa Ishimaeli, mwana wa Abraham, ambaye Hajiri Mmisri mtumishi wake Sara, alizaa kwa Abraham.
ואלה שמות בני ישמעאל בשמתם לתולדתם בכר ישמעאל נבית וקדר ואדבאל ומבשם 13
Haya ndiyo yalikuwa majina ya wana wa Ishimaeli, kuanzia mzaliwa wa kwanza: Nebayothi - mzaliwa wa kwanza wa Ishimaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu,
ומשמע ודומה ומשא 14
Mishma, Duma, Masa,
חדד ותימא יטור נפיש וקדמה 15
Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi, na Kedema.
אלה הם בני ישמעאל ואלה שמתם בחצריהם ובטירתם--שנים עשר נשיאם לאמתם 16
Hawa ndio walikuwa wana wa Ishimaeli, na haya ndiyo majina yao, kwa vijiji vyao, na katika vituo vyao; Maseyidi kumi na wawili kufuatana na kabila zao.
ואלה שני חיי ישמעאל--מאת שנה ושלשים שנה ושבע שנים ויגוע וימת ויאסף אל עמיו 17
Hii ndiyo ilikuwa miaka ya Ishimaeli, miaka 137: akapumua pumzi yake ya mwisho na akafa, na akakusanywa pamoja na watu wake.
וישכנו מחוילה עד שור אשר על פני מצרים באכה אשורה על פני כל אחיו נפל 18
Walioshi toka Havila mpaka Shuri, ambayo iko karibu na Misri, kuelekea Ashuru. Waliishi kwa uadui kati yao.
ואלה תולדת יצחק בן אברהם אברהם הוליד את יצחק 19
Haya ndiyo yalikuwa matukio kumuhusu Isaka, mwana wa Abraham: Abraham alimzaa Isaka.
ויהי יצחק בן ארבעים שנה בקחתו את רבקה בת בתואל הארמי מפדן ארם--אחות לבן הארמי לו לאשה 20
Isaka alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomuoa Rebeka, binti wa ethueli Mshami wa Padani Aramu, ndugu wa Labani Mshami.
ויעתר יצחק ליהוה לנכח אשתו כי עקרה הוא ויעתר לו יהוה ותהר רבקה אשתו 21
Isaka akamwomba Yahwe kwa ajili ya mke wake kwa sababu alikuwa tasa, na Yahwe akajibu maombi yake, Rebeka mkewe akabeba mimba.
ויתרצצו הבנים בקרבה ותאמר אם כן למה זה אנכי ותלך לדרש את יהוה 22
Watoto hawa walipokuwa tumboni mwake wakasumbuka, naye akasema, “Kwa nini jambo hili linatokea kwangu mimi?” Akaenda kumuuliza Yahwe kuhusu jambo hili.
ויאמר יהוה לה שני גיים (גוים) בבטנך ושני לאמים ממעיך יפרדו ולאם מלאם יאמץ ורב יעבד צעיר 23
Yahwe akamwambia, “Mataifa mawili yako katika tumbo lako, na mataifa haya mawili yatatengana ndani yako. Taifa moja litakuwa lenye nguvu kuliko lingine, na yule mkubwa atamtumikia mdogo.
וימלאו ימיה ללדת והנה תומם בבטנה 24
Ulipo wadia wakati wa kujifungua, tazama, kulikuwa na mapacha ndani ya tumbo lake.
ויצא הראשון אדמוני כלו כאדרת שער ויקראו שמו עשו 25
Wakwanza akatoka akiwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau.
ואחרי כן יצא אחיו וידו אחזת בעקב עשו ויקרא שמו יעקב ויצחק בן ששים שנה בלדת אתם 26
Baada ya hapo ndugu yake akatoka. Mkono wake ukiwa umeshika kisigino cha Esau. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini wakati mke wake alipo wazaa hawa watoto.
ויגדלו הנערים ויהי עשו איש ידע ציד איש שדה ויעקב איש תם ישב אהלים 27
Vijana hawa wakakua, Hesau akawa mwindaji hodari, mtu wa nyikani; lakini Yakobo alikuwa mtu mkimya, aliye tumia muda wake akiwa katika mahema.
ויאהב יצחק את עשו כי ציד בפיו ורבקה אהבת את יעקב 28
Kisha Isaka akampenda Esau kwa sababu alikula wanyama ambao alikuwa anawinda, lakini Rebeka akampenda Yakobo.
ויזד יעקב נזיד ויבא עשו מן השדה והוא עיף 29
Yakobo akapika mchuzi. Esau akaja kutoka nyikani, akiwa dhaifu kutokana na njaa.
ויאמר עשו אל יעקב הלעיטני נא מן האדם האדם הזה--כי עיף אנכי על כן קרא שמו אדום 30
Esau akamwambia Yakobo, “Nilishe mchuzi mwekundu. Tafadhari, nimechoka!” Na hii ndiyo sababu jina lake aliitwa Edomu.
ויאמר יעקב מכרה כיום את בכרתך לי 31
Yakobo akasema, “Kwanza uniuzie haki yako ya mzaliwa wa kwanza.”
ויאמר עשו הנה אנכי הולך למות ולמה זה לי בכרה 32
Esau akasema, “Tazama, nakaribia kufa. Ni nini kwangu haki ya mzaliwa wa kwanza?”
ויאמר יעקב השבעה לי כיום וישבע לו וימכר את בכרתו ליעקב 33
Yakobo akasema, “Kwanza uape kwangu mimi,” kwa hiyo Esau akaapa kiapo na kwa njia hii akawa ameuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa Yakobo.
ויעקב נתן לעשו לחם ונזיד עדשים ויאכל וישת ויקם וילך ויבז עשו את הבכרה 34
Yakobo akampatia Esau mkate pamoja na mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka na akaenda zake. Kwa njia hii Esau akawa ameidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.

< בראשית 25 >