< יחזקאל 28 >

ויהי דבר יהוה אלי לאמר 1
Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
בן אדם אמר לנגיד צר כה אמר אדני יהוה יען גבה לבך ותאמר אל אני--מושב אלהים ישבתי בלב ימים ואתה אדם ולא אל ותתן לבך כלב אלהים 2
“Mwanadamu, waambie watawala wa Tiro, 'Bwana Yahwe asema hivi: Moyo wako unakiburi! Umesema, “mimi ni mungu! Nitakaa kwenye kiti cha miungu katika moyo wa bahari!” Ingawa wewe ni mtu na sio mungu, unaufanya moyo wako kama moyo wa mungu,
הנה חכם אתה מדנאל (מדניאל) כל סתום לא עממוך 3
unafikiri kwamba unahekima kuliko Danieli, na kwamba hakuna siri ikushangazayo!
בחכמתך ובתבונתך עשית לך חיל ותעש זהב וכסף באוצרותיך 4
Umejitajirisha mwenyewe pamoja na hekima na ujuzi, na kujipatia dhahabu na fedha katika hazina yako!
ברב חכמתך ברכלתך הרבית חילך ויגבה לבבך בחילך 5
Kwa hekima kubwa na kwa biashara yako, umeongeza utajiri wako, hivyo moyo wako una kiburi kwa sababu ya utajiri yako.
לכן כה אמר אדני יהוה יען תתך את לבבך כלב אלהים 6
Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu umetengeza moyo wako kama moyo wa mungu,
לכן הנני מביא עליך זרים--עריצי גוים והריקו חרבותם על יפי חכמתך וחללו יפעתך 7
kwa hiyo nitaleta wageni juu yako, watu wa kuogofya kutoka mataifa mengine. Wataleta panga zao juu hekima ya uzuri wako, na watauchafua uzuri wako.
לשחת יורדוך ומתה ממותי חלל בלב ימים 8
Watakupeleka chini hata kwenye shimo, na utakufa kifo cha waliokufa katika Bahari.
האמר תאמר אלהים אני לפני הרגך ואתה אדם ולא אל ביד מחלליך 9
Je! kweli utasema, “Mimi ni mungu” mbele ya uso wa yule akuuaye? Wewe ni mwanadamu na sio Mungu, na utakuwa kwenye mkono wa yule akujeruaye.
מותי ערלים תמות ביד זרים כי אני דברתי נאם אדני יהוה 10
Utakufa kifo cha asiyetahiriwa kwa mkono wa wageni kwa kuwa nimesema hili-asema Bwana Yahwe.
ויהי דבר יהוה אלי לאמר 11
Neno la Yahwe likanijia, kusema,
בן אדם שא קינה על מלך צור ואמרת לו כה אמר אדני יהוה אתה חותם תכנית מלא חכמה וכליל יפי 12
“Mwanadamu, inua maombolezo kwa ajili ya mfalme wa Tiro na umwambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Uliumbwa mkamilifu, umejaa hekima na ukamilifu wa hekima.
בעדן גן אלהים היית כל אבן יקרה מסכתך אדם פטדה ויהלם תרשיש שהם וישפה ספיר נפך וברקת וזהב מלאכת תפיך ונקביך בך ביום הבראך כוננו 13
Ulikuwa katika Edeni, bustani ya Mungu. Kila jiwe la thamani lilikufunika: akiki, yakuti manjano, almasi, zabarajadi, shohamu, yaspi, yakuti samawi, zumaridi, baharamani, na dhahabu. Ilikuwa siku uliyokuwa umeiumba ambayo walikuwa wameiandaa.
את כרוב--ממשח הסוכך ונתתיך בהר קדש אלהים היית--בתוך אבני אש התהלכת 14
Nimekuweka juu ya mlima mtakatifu wa Mungu kama kerubi nimekutia mafuta kwa ajili ya kumlinda mwanadamu. Ulikuwa kati ya mawe ya moto ulipozunguka.
תמים אתה בדרכיך מיום הבראך עד נמצא עולתה בך 15
Ulikuwa mwadilifu kwenye njia zako kutoka siku ulipoumbwa hadi uovu ulipoonekana ndani yako.
ברב רכלתך מלו תוכך חמס--ותחטא ואחללך מהר אלהים ואבדך כרוב הסכך מתוך אבני אש 16
Kupitia biashara yako kubwa uliyokuwa umeijaza kwa udhalimu, hivyo umetenda dhambi. Hivyo nimekutupilia mbali ya mlima wa Mungu, kama mmoja wao wa aliyekuwa ameninajisi, na nimekuharibu, kerubi mlinzi, na kukutoa miongono mwa mawe ya moto.
גבה לבך ביפיך שחת חכמתך על יפעתך על ארץ השלכתיך לפני מלכים נתתיך--לראוה בך 17
Moyo wako ulikuwa na kiburi kwa uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya fahari yako. Nimekupeleka chini kwenye dunia. Nimekuweka mbele ya wafalme ili waweze kukuona.
מרב עוניך בעול רכלתך חללת מקדשיך ואוצא אש מתוכך היא אכלתך ואתנך לאפר על הארץ לעיני כל ראיך 18
Kwa sababu ya wingi wa dhambi zako na biashara za udanganyifu, umepanajisi mahali pako patakatifu. Basi nimetengeneza moto kutoka ndani yako; utakula wewe. Nitakugeuza kwenye majivu juu ya dunia katika macho ya wote wakutazamao.
כל יודעיך בעמים שממו עליך בלהות היית ואינך עד עולם 19
Wale wote waliokujua miongoni mwa watu watakao kutetemekewa; watakuwa watu wa kutisha, na hutakuwepo tena milele.”'
ויהי דבר יהוה אלי לאמר 20
Kisha neno la Bwana Yahwe likanijia, kusema,
בן אדם שים פניך אל צידון והנבא עליה 21
“Mwanadamu, elekeza uso wako Sidoni na toa utabiri juu yake.
ואמרת כה אמר אדני יהוה הנני עליך צידון ונכבדתי בתוכך וידעו כי אני יהוה בעשותי בה שפטים--ונקדשתי בה 22
Sema, Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Niko juu yako, Sidoni! Kwa kuwa nitatukuzwa kati yako hivyo watu wako watajua kwamba mimi ni Yahwe wakati nitakapokuwa nimezitekeleza hukumu ndani yako. Nitaonyesha utakatifu ndani yako.
ושלחתי בה דבר ודם בחוצותיה ונפלל חלל בתוכה בחרב עליה מסביב וידעו כי אני יהוה 23
Nitapeleka tauni juu yako na tazama mitaa yako, na walioua wataanguka kati yako. Wakati upanga utakapokuja juu yao kutoka pande zote, kisha mtajua kwamba mimi ni Yahwe.
ולא יהיה עוד לבית ישראל סלון ממאיר וקוץ מכאב מכל סביבתם השאטים אותם וידעו כי אני אדני יהוה 24
Kisha hakutakuwa na mtemba uchomao na maumivu ya miba kwa ajili ya nyumba ya Israeli kutoka wale wote waliomzunguka wanaowadharau watu wake, hivyo watajua kwamba mimi ni Bwana Yahwe!'
כה אמר אדני יהוה בקבצי את בית ישראל מן העמים אשר נפצו בם ונקדשתי בם לעיני הגוים וישבו על אדמתם אשר נתתי לעבדי ליעקב 25
Bwana Yahwe asema hivi, Nitakapowakusanya nyumba ya Israeli kutoka miongni mwa watu waliokuwa wamekusanyika, na wakati nilipokuwa nimewatenga miongoni mwao, hivyo mataifa aanaweza kuona, kisha watafanya nyumba zao katika nchi nitakayo mpatia mtumishi wangu Yakobo.
וישבו עליה לבטח ובנו בתים ונטעו כרמים וישבו לבטח בעשותי שפטים בכל השאטים אתם מסביבותם--וידעו כי אני יהוה אלהיהם 26
Kisha wataishi salama ndani yake na kujenga nyumba, kulima mizabibu, na kuishi salama wakati nitakapo zitekeleza hukumu juu ya wote wale ambao sasa wanawadharau kutoka sehemu zote; basi watajua yakwamba mimi ni Yahwe Mungu wao!”'

< יחזקאל 28 >