< יחזקאל 14 >

ויבוא אלי אנשים מזקני ישראל וישבו לפני 1
Baadhi ya viongozi wa Israeli wakaja kwangu na kuketi mbele yangu.
ויהי דבר יהוה אלי לאמר 2
Ndipo neno la Yahwe likanijia, likisema,
בן אדם האנשים האלה העלו גלוליהם על לבם ומכשול עונם נתנו נכח פניהם האדרש אדרש להם 3
“Mwanadamu, hawa watu wamchukua sanamu zao kwenye mioyo yao na kuweka pingamizi la uovu wao mbele ya nyuso zao wenyewe. Je naweza kuulizwa yote na wao?
לכן דבר אותם ואמרת אליהם כה אמר אדני יהוה איש איש מבית ישראל אשר יעלה את גלוליו אל לבו ומכשול עונו ישים נכח פניו ובא אל הנביא אני יהוה נעניתי לו בה (בא)--ברב גלוליו 4
Kwa hiyo watangazie hivi na waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Kila mtu wa nyumba ya Israeli achukuaye sanamu moyoni mwake, au awekeye pingamizi la uovu mbele ya uso wake, na kisha yule ajaye kwa nabii-Mimi, Yahwe, nitamjibu kulingana na sanamu zake.
למען תפש את בית ישראל בלבם אשר נזרו מעלי בגלוליהם כלם 5
Nitafanya hivi ili kwamba niweze kuirudisha nyumba ya Israeli katika mioyo yao ambayo ilikuwa mbali nami kwa ajili ya sanamu zao.'
לכן אמר אל בית ישראל כה אמר אדני יהוה שובו והשיבו מעל גלוליכם ומעל כל תועבתיכם השיבו פניכם 6
Kwa hiyo sema kwa nyumba ya Israeli, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tubuni na rudini kutoka kwenye sanamu zenu! Rudisheni nyuma nyuso zenu kutoka kwenye kachukizo yenu yote.
כי איש איש מבית ישראל ומהגר אשר יגור בישראל וינזר מאחרי ויעל גלוליו אל לבו ומכשול עונו ישים נכח פניו ובא אל הנביא לדרש לו בי--אני יהוה נענה לו בי 7
Kwa kuwa kila mmoja kutoka kwenye nyumba ya Israeli na kila mmoja wa wageni wanaoishi katika Israeli ajitengaye nami, achukuaye sanamu zake kwenye moyo wake na kuweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake mwenyewe, na kisha yule ajaye kwa nabii kunitafuta-mimi, Yahwe, nitamjibu mimi mwenyewe.
ונתתי פני באיש ההוא והשמתיהו לאות ולמשלים והכרתיו מתוך עמי וידעתם כי אני יהוה 8
Hivyo nitauweka uso wangu juu ya huyo mtu na kumfanya ishara na mithali, kwa kuwa nitamkata kutoka kati ya watu wangu, na mtajua kuwa mimi ni Yahwe.
והנביא כי יפתה ודבר דבר--אני יהוה פתיתי את הנביא ההוא ונטיתי את ידי עליו והשמדתיו מתוך עמי ישראל 9
Kama nabii atadanganywa na kuongea ujumbe, kisha Mimi Yahwe, nitamdanganya huyo nabii; Nitanyoosha mkono wangu na kumwangamizaku toka kati watu wangu Israeli.
ונשאו עונם כעון הדרש--כעון הנביא יהיה 10
Watabeba uovu wao wenyewe; uwovu wa nabii utakua uleule kama uovu wa yule aulizaye kutoka kwake.
למען לא יתעו עוד בית ישראל מאחרי ולא יטמאו עוד בכל פשעיהם והיו לי לעם ואני אהיה להם לאלהים--נאם אדני יהוה 11
Kwa sababu hiyo basi, nyumba ya Israeli haitaenda mbali kutoka kunifuata mimi wala kujinajisi wenyewe kupitia dhambi zao zote. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao-hivi ndivyo Yahwe asemavyo.”'
ויהי דבר יהוה אלי לאמר 12
Kisha neno la Yahwe likanijia, likisema,
בן אדם ארץ כי תחטא לי למעל מעל ונטיתי ידי עליה ושברתי לה מטה לחם והשלחתי בה רעב והכרתי ממנה אדם ובהמה 13
“Mwanadamu, wakati nchi itakapo asi dhidi yangu kwa kufanya dhambi ili kwamba ninyooshe mkono wangu dhidi yake na kuvunja tegemea la mkate wake, na kuleta njaa juu yake na kukata mnyama kutoka kwenye nchi;
והיו שלשת האנשים האלה בתוכה--נח דנאל (דניאל) ואיוב המה בצדקתם ינצלו נפשם נאם אדני יהוה 14
kisha hata kama hawa watu watatu-Nuhu, Danieli, na Ayubu-walikuwa katikati ya nchi, wangeweza kuokoa maisha yao wenyewe kwa haki-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
לו חיה רעה אעביר בארץ ושכלתה והיתה שממה מבלי עובר מפני החיה 15
Kama nikileta wanyama waovu kwenye nchi na kuwafanya wasizae hivyo basi itakuwa hakuna mtu asiweze kupita kwa sababu ya hao wanyama,
שלשת האנשים האלה בתוכה--חי אני נאם אדני יהוה אם בנים ואם בנות יצילו המה לבדם ינצלו והארץ תהיה שממה 16
kisha hata kama watu hawa hawa watatu ndani yake-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuwaokoa hata watoto wao wala binti; isipokuwa maisha yao yataokoka, lakini nchi itakuwa ukiwa.
או חרב אביא על הארץ ההיא ואמרתי חרב תעבר בארץ והכרתי ממנה אדם ובהמה 17
Au nikileta upanga juu ya hiyo nchi na kusema, 'Upanga, nenda kwenye nchi na wakate wote mtu na mnyama kutoka huo',
ושלשת האנשים האלה בתוכה--חי אני נאם אדני יהוה לא יצילו בנים ובנות כי הם לבדם ינצלו 18
kisha hata kama hawa watu watatu watakuwa katikatai ya nchi-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuwaokoa japo watoto wao wala binti; ila tu maisha yao wenyewe yangeokolewa.
או דבר אשלח אל הארץ ההיא ושפכתי חמתי עליה בדם להכרית ממנה אדם ובהמה 19
Au kama nikipeleka tauni juu ya nchi na kumwaga dhahabu yangu juu yake kwa damu, ili kuwakata mtu na mnyama,
ונח דנאל (דניאל) ואיוב בתוכה--חי אני נאם אדני יהוה אם בן אם בת יצילו המה בצדקתם יצילו נפשם 20
kisha hata kama Nuhu, Danieli, na Ayubu wangekuwa kwenye hiyo nchi-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuokoa hata watoto wao au binti; maisha yao pekee yangeokoka kwa haki.
כי כה אמר אדני יהוה אף כי ארבעת שפטי הרעים חרב ורעב וחיה רעה ודבר שלחתי אל ירושלם--להכרית ממנה אדם ובהמה 21
Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: hakika nitafanya mambo makali sana kwa kuleta adhabu zangu nne-njaa, upanga, wanyama wa porini, na tauni-juu ya Yerusalemu kuwakata wote mtu na mnyama kutoka kwake.
והנה נותרה בה פלטה המוצאים בנים ובנות--הנם יוצאים אליכם וראיתם את דרכם ואת עלילותם ונחמתם על הרעה אשר הבאתי על ירושלם--את כל אשר הבאתי עליה 22
Kisha, tazama! mabaki yatasalia kwake, watakaokoka wataenda pamoja na wana na binti. Tazama! Watawatokea, na mtaona njia zao na matendo yao yakiwafariji kuhusu adhabu niliyoipeleka Yerusalemu, na kuhusu kila kitu kingine ambacho nilichopeleka juu ya nchi.
ונחמו אתכם כי תראו את דרכם ואת עלילותם וידעתם כי לא חנם עשיתי את כל אשר עשיתי בה--נאם אדני יהוה 23
Waliokoka watawafariji ninyi mtakapoona njia zao na matendo yao, hivyo mtayajua haya mambo niliyoyafanya juu yake, kwamba sijayafanya bure! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

< יחזקאל 14 >