< אסתר 8 >

ביום ההוא נתן המלך אחשורוש לאסתר המלכה את בית המן צרר היהודיים (היהודים) ומרדכי בא לפני המלך--כי הגידה אסתר מה הוא לה 1
Siku hiyo Mfalme Ahusiero akampa Malkia Esta mali yote ya Hamani, adui wa Wayahudi. Na kisha akampandisha cheo Modekai ili atumike mbele zake, kwa sababu Malkia Esta alikuwa amemueleza Mfalme uhusiano wake na Modekai.
ויסר המלך את טבעתו אשר העביר מהמן ויתנה למרדכי ותשם אסתר את מרדכי על בית המן 2
Kisha Mfalme akampa pete yake aliyokuwa amempa Hamani. Malkia Esta akampandisha Modekai ili awe mkuu katika shamba la Hamani.
ותוסף אסתר ותדבר לפני המלך ותפל לפני רגליו ותבך ותתחנן לו להעביר את רעת המן האגגי ואת מחשבתו אשר חשב על היהודים 3
Kisha Esta akaongea tena na mfalme. Akaanguka chini na kulia mbele za mfalme akimsihi Mfalme abatilishe njama ya kuwaua Wayahudi wote iliyokuwa imetangazwa na Hamani Muagagi
ויושט המלך לאסתר את שרבט הזהב ותקם אסתר ותעמד לפני המלך 4
kisha mfalme akamnyoshea Esta fimbo yake ya dhahabu, akainuka na kusimama mbele ya mfalme.
ותאמר אם על המלך טוב ואם מצאתי חן לפניו וכשר הדבר לפני המלך וטובה אני בעיניו--יכתב להשיב את הספרים מחשבת המן בן המדתא האגגי אשר כתב לאבד את היהודים אשר בכל מדינות המלך 5
Esta akasema, “Kama ikikupendeza na kama nimepata kibali mbele zako, agiza mbiu ipigwe ili kubatilisha barua zilizoandikwa na Hamani mwana wa Hammedatha muagagi, barua alizoziandika ili kuwa angamiza Wayahudi wote walikuwa katika majimbo yote ya mfalme.
כי איככה אוכל וראיתי ברעה אשר ימצא את עמי ואיככה אוכל וראיתי באבדן מולדתי 6
Ninawezaje kuona ubaya ukiwapa watu wangu? Ninawezaje kutazama uharibifu wa jamaa zangu?”
ויאמר המלך אחשורש לאסתר המלכה ולמרדכי היהודי הנה בית המן נתתי לאסתר ואתו תלו על העץ--על אשר שלח ידו ביהודיים (ביהודים) 7
Mfalme Ahusiero akamwambia Esta na Modekai, Muyahudi, tazama nimempa Esta nyumba yote ya Hamani na wamemtundika Hamani katika mti kwa sababu alikuwa amekusudia kuwaangamiza Wayahudi wote.
ואתם כתבו על היהודים כטוב בעיניכם בשם המלך וחתמו בטבעת המלך כי כתב אשר נכתב בשם המלך ונחתום בטבעת המלך--אין להשיב 8
Hivyo andika mbiu nyingine kwa ajili ya Wayahudi kwa jina la mfalme na uipige muhuri kwa pete ya mfalme. Kwa sababu mbiu imekwisha andikwa kwa jina la mfalme na kugongwa muhuri kwa pete ya mfamle na haiwezi kubatilishwa.”
ויקראו ספרי המלך בעת ההיא בחדש השלישי הוא חדש סיון בשלושה ועשרים בו ויכתב ככל אשר צוה מרדכי אל היהודים ואל האחשדרפנים והפחות ושרי המדינות אשר מהדו ועד כוש שבע ועשרים ומאה מדינה מדינה ומדינה ככתבה ועם ועם כלשנו ואל היהודים--ככתבם וכלשונם 9
Kisha waandishi wa mfalme wakakusanyika kwa wakati huo huo katika mwezi wa tatu, ambao ni mwezi wa Sivani, siku ya ishirini ya mwezi wa tatu. Mbiu iliandikwa yote ambayo Modekai aliyaamuru kwa Wayahudi watendewe na wenyeji wa kila jimbo. Mbiu iliandikwa kwa maakida magavana na wakuu wa majimbo yote yaliyokuwa toka India hadi Ethiopia, majimbo 127 kila jimbo iliandikwa kuwa maandishi yake, na kila watu kwa lugha yao, na kwa Wayahudi kwa maandishi na lugha yao.
ויכתב בשם המלך אחשורש ויחתם בטבעת המלך וישלח ספרים ביד הרצים בסוסים רכבי הרכש האחשתרנים--בני הרמכים 10
Modekai akaandika kwa jina la Mfalme Ahusiero na akazipiga muhuri kwa pete ya mfalme. Akapeleka nyaraka kwa matarishi, akawapandisha kwenye farasi waendao kwa haraka waliotumika kwa huduma ya mfalme, waliozaliwa kwa mfalme.
אשר נתן המלך ליהודים אשר בכל עיר ועיר להקהל ולעמד על נפשם--להשמיד ולהרג ולאבד את כל חיל עם ומדינה הצרים אתם טף ונשים ושללם לבוז 11
Mfalme akawapa Wayahudi wote katika majimbo ya utawala wake kibali cha kukusanyika na kujilinda na ruhusa ya kuangamiza, kuua na kuharibu mtu yeyote aliyekuwa na kusudi la kuwaua Wayahudi wote na kupora mali zao.
ביום אחד בכל מדינות המלך אחשורוש--בשלושה עשר לחדש שנים עשר הוא חדש אדר 12
Jambo hili lilipaswa litekelezwe katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, siku ya ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ambao ni mwezi wa Adari.
פתשגן הכתב להנתן דת בכל מדינה ומדינה גלוי לכל העמים ולהיות היהודיים (היהודים) עתודים (עתידים) ליום הזה להנקם מאיביהם 13
Nakala ya mbiu ilipaswa kutolewa kama sheria na kutangazwa kwa watu wote. Wayahudi walikuwa tayari kwa siku hiyo kulipa kisasi kwa adui zao.
הרצים רכבי הרכש האחשתרנים יצאו מבהלים ודחופים בדבר המלך והדת נתנה בשושן הבירה 14
Hivyo matarishi wakaendesha farasi waliokuwa wakitumiwa katika huduma za kifalme. Walienda kwa haraka sana. Mbiu hii pia ilikuwa imetolewa katika mji wa Shushani pia.
ומרדכי יצא מלפני המלך בלבוש מלכות תכלת וחור ועטרת זהב גדולה ותכריך בוץ וארגמן והעיר שושן צהלה ושמחה 15
Kisha Mosekai akaondoka mbele za mfalme akiwa amevaa mavazi ya kifalme, nguo buluu na nyeupe na taji kubwa ya dhahabu na joho la zambarau. Mji wa Shushani ukafurahia.
ליהודים היתה אורה ושמחה וששן ויקר 16
Wayahudi walikuwa na nuru, na furaha na heshima. Mji wowote ambao mbiu hii ilipigwa, Wayahudi walifurahia na walifanya karamu na pumziko.
ובכל מדינה ומדינה ובכל עיר ועיר מקום אשר דבר המלך ודתו מגיע שמחה וששון ליהודים משתה ויום טוב ורבים מעמי הארץ מתיהדים--כי נפל פחד היהודים עליהם 17
Watu wengi wakatamani kuwa Wayahudi sababu ya hofu ya Wayahudi iliyokuwa juu yao.

< אסתר 8 >