< אסתר 3 >
אחר הדברים האלה גדל המלך אחשורוש את המן בן המדתא האגגי--וינשאהו וישם את כסאו מעל כל השרים אשר אתו | 1 |
Baada ya mambo haya, Mfalme Ahusiero alimpandisha cheo Hamani mwana wa Hammedatha mwagagi, na akaweka kiti chake cha ukuu juu ya wakuu wote waliokuwa pamoja naye.
וכל עבדי המלך אשר בשער המלך כרעים ומשתחוים להמן--כי כן צוה לו המלך ומרדכי--לא יכרע ולא ישתחוה | 2 |
Na watumishi wote wa mfalme waliokuwa katika lango la mfalme walipaswa kupiga magoti na kusujudia Hamani, kama mfalme alivyoagiza. Lakini Modekai hakupiga magoti wala kusujudu mbele ya Hamani.
ויאמרו עבדי המלך אשר בשער המלך--למרדכי מדוע אתה עובר את מצות המלך | 3 |
Kisha watumishi wa mfalme waliokuwa langoni mwa mfalme walimwambia Modekai, kwa nini hautii amri ya mfalme?
ויהי באמרם (כאמרם) אליו יום ויום ולא שמע אליהם ויגידו להמן לראות היעמדו דברי מרדכי--כי הגיד להם אשר הוא יהודי | 4 |
Walisema naye siku kwa siku, lakini alikataa kufuata matakwa yao. Hivyo wakaongea na Hamani kuona kama swala la Modekai lingebaki hivyo alikuwa amewataarifu kuwa Modekai alikuwa Muyahudi.
וירא המן--כי אין מרדכי כרע ומשתחוה לו וימלא המן חמה | 5 |
Hamani alipoona kuwa Modekai hapigi magoti wala kumsujudia, alipatwa na hasira.
ויבז בעיניו לשלח יד במרדכי לבדו--כי הגידו לו את עם מרדכי ויבקש המן להשמיד את כל היהודים אשר בכל מלכות אחשורוש--עם מרדכי | 6 |
Alikuwa na wazo la kumuua Modekai, watumishi wa mfalme walikuwa wamemueleza kuwa Modekai na jamaa zake walikuwa Wayahudi. Hamani akaazimu kuwaangamiza Wayahudi wote, watu wa Modekai, ambao walikuwa katika ufalme wa Ahusiero.
בחדש הראשון הוא חדש ניסן בשנת שתים עשרה למלך אחשורוש הפיל פור הוא הגורל לפני המן מיום ליום ומחדש לחדש שנים עשר--הוא חדש אדר | 7 |
Katika mwezi wa kwanza, (ambao ni mwezi wa Nisani) ndani ya mwaka wa kumi na mbili wa Mfalme Ahusiero, walipiga kura mbele ya Hamani kura kila siku na mwezi, kuchagua siku na mwezi hadi walipochagua mwezi wa kumi na mbili, (mwezi wa Adari.
ויאמר המן למלך אחשורוש--ישנו עם אחד מפזר ומפרד בין העמים בכל מדינות מלכותך ודתיהם שנות מכל עם ואת דתי המלך אינם עשים ולמלך אין שוה להניחם | 8 |
Kisha Hamani akamwambia mfalme Ahusiro, “kuna watu fulani katika majimbo yote ya ufalme wako wasiofuata sheria zako. Na kwa tabia yao ya kutofuata sheria zako hawapasi kuendelea kuwa hai.
אם על המלך טוב יכתב לאבדם ועשרת אלפים ככר כסף אשקול על ידי עשי המלאכה להביא אל גנזי המלך | 9 |
Kama ikimpendeza mfalme, toa amri watu hawa wote wakatiliwe mbali, nami nitapima talanta elfu kumi za fedha katika mikono ya wale ambao ni wasimamizi wa maswala ya mfalme, ili kwamba waweke katika hazina ya mfalme.”
ויסר המלך את טבעתו מעל ידו ויתנה להמן בן המדתא האגגי--צרר היהודים | 10 |
Ndipo mfamle akavua pete yake ya muhuri na kumpa Hamani, adui wa Wayahudi.
ויאמר המלך להמן הכסף נתון לך והעם לעשות בו כטוב בעיניך | 11 |
Mfalme akamwambia Hamani, “Nitahakikisha kwamba fedha inarudi kwako na kwa watu wako. Ili muitumie kama mpendavyo.”
ויקראו ספרי המלך בחדש הראשון בשלושה עשר יום בו ויכתב ככל אשר צוה המן אל אחשדרפני המלך ואל הפחות אשר על מדינה ומדינה ואל שרי עם ועם מדינה ומדינה ככתבה ועם ועם כלשונו בשם המלך אחשורש נכתב ונחתם בטבעת המלך | 12 |
Kisha waandishi wa mfalme walikusanyika katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza, na mbiu iliyokuwa na matakwa ya Hamani yalikuwa yameandikwa na kupelekwa kwa wasimamizi wa majimbo, na wale wote waliokuwa juu ya wasimamizi wa majimbo yote, na wasimamizi wa watu, na kwa kila jimbo kwa andiko lao, na kila watu na lugha yao. Mbiu hii ilikuwa imeandikwa kwa jina la mfalme Ahusiero na kupigwa muhuri wa pete yake.
ונשלוח ספרים ביד הרצים אל כל מדינות המלך--להשמיד להרג ולאבד את כל היהודים מנער ועד זקן טף ונשים ביום אחד בשלושה עשר לחדש שנים עשר הוא חדש אדר ושללם לבוז | 13 |
Barua hizi za kutaka kuwakatilia mbali Wayahudi wote zilizambazwa katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, kuangamiza, kuua na kuwaharibu Wayahudi wote, tangu mdogo hadi mkubwa, watoto na wanawake, ndani ya siku moja katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili (ambao ni mwezi wa Adari) na kuteka mali zo.
פתשגן הכתב להנתן דת בכל מדינה ומדינה גלוי לכל העמים--להיות עתדים ליום הזה | 14 |
Nakala ya ilifanywa kuwa sheria na kupelekwa kila jimbo. Taarifa juu ya maangamizi ya Wayahudi ilienea katika kila jimbo kwamba watu wote wajiandae katika siku hiyo.
הרצים יצאו דחופים בדבר המלך והדת נתנה בשושן הבירה והמלך והמן ישבו לשתות והעיר שושן נבוכה | 15 |
Wasambazajia walisambaza agizo la mfalme. Tangazo hili pioa lilitolewa na kusambazwa katika mji wa Shushani. Mfalme alikuwa na Hamani walikaa na kunywa, lakini mji wa Shushani, lakini mjiwa Shushani ulikuwa katika uangamivu.