< דברים 3 >

ונפן ונעל דרך הבשן ויצא עוג מלך הבשן לקראתנו הוא וכל עמו למלחמה--אדרעי 1
Kisha tuligeuka na kwenda njia ya juu Bashani. Ogi, mfalme wa Bashani, alikuja na kutuvamia, yeye na watu wake wote, kupigana huko Edrei.
ויאמר יהוה אלי אל תירא אתו--כי בידך נתתי אתו ואת כל עמו ואת ארצו ועשית לו--כאשר עשית לסיחן מלך האמרי אשר יושב בחשבון 2
Yahwe aliniambia mimi, “Usimuogope; kwa kuwa nimekupa ushindi dhidi yake na nimewaweka watu wake wote na nchi yake chini ya utawala wako. Utamfanya kama ulivyomfanya Sihoni, mfalme wa Amorites, aliyeishi Heshbon.
ויתן יהוה אלהינו בידנו גם את עוג מלך הבשן--ואת כל עמו ונכהו עד בלתי השאיר לו שריד 3
Kwa hiyo Yahwe Mungu wetu pia alitupa ushindi dhidi ya Ogi mfalme wa Bashani, na watu wake wote waliwekwa chini ya utawala wetu. Na tulimpiga mpaka kufa na hakuna yoyote wa watu wake walibaki.
ונלכד את כל עריו בעת ההוא--לא היתה קריה אשר לא לקחנו מאתם ששים עיר כל חבל ארגב ממלכת עוג בבשן 4
Tulichukua miji yake yote kwa wakati huo; hapakuwa na mji hata mmoja ambao hatukuchukua kutoka kwao: miji sitini - mikoa ya Argobi yote, ufalme wa Ogi Bashani.
כל אלה ערים בצרת חומה גבהה--דלתים ובריח לבד מערי הפרזי הרבה מאד 5
Hii ilikuwa miji iliyoimarishwa na kuta ndevu, malango, na vizuizi, hii ilikuwa licha ya vijiji vingi sana vilivyokuwa havina kuta.
ונחרם אותם--כאשר עשינו לסיחן מלך חשבון החרם כל עיר מתם הנשים והטף 6
Tuliviangamiza kabisa, kama tulivyofanya kwa Sihoni mfalme wa Heshbon, kabisa tuliangamiza kila mji- wanaume na wanawake na watoto wadogo.
וכל הבהמה ושלל הערים בזונו לנו 7
Lakini ng'ombe wote na mateka ya miji, tilichukua kama mateka wetu.
ונקח בעת ההוא את הארץ מיד שני מלכי האמרי אשר בעבר הירדן--מנחל ארנן עד הר חרמון 8
Kwa wakati huo tulichukua nchi kutoka kwenye mkono wa wafalme wawili wa Amorites, waliokuwa ng'ambo ya pili ya Yordani, kutoka kwenye bonde la Arnon kwenda mlima wa Hermoni,
צידנים יקראו לחרמון שרין והאמרי יקראו לו שניר 9
(Mlima wa Hermoni, Wasidonia huita Sirioni, na Wamorites huita Seniri)
כל ערי המישר וכל הגלעד וכל הבשן עד סלכה ואדרעי--ערי ממלכת עוג בבשן 10
na miji yote ya tambarare, yote Gileadi, na yote Bashani kupita njia yote ya Salekah na Edrei, miji ya ufalme wa Ogi huko Bashani”.
כי רק עוג מלך הבשן נשאר מיתר הרפאים--הנה ערשו ערש ברזל הלה הוא ברבת בני עמון תשע אמות ארכה וארבע אמות רחבה--באמת איש 11
(Kwa mabaki ya Refaimu, mfalme Ogi pekee wa Bashani alikuwa amebaki. Tazama! Kitanda chake kilikuwa cha chuma. Hakuna huko Rabbah, ambako wazao wa Ammoni waliishi? Ilikuwa dhiraa tisa urefu na dhiraa nne upana, hiyo njia walitumia watu kupima.)
ואת הארץ הזאת ירשנו בעת ההוא מערער אשר על נחל ארנן וחצי הר הגלעד ועריו--נתתי לראובני ולגדי 12
“Hili eneo ambalo tulichukua kumiliki kwa wakati huo-kutoka Aroer, kwamba ni kwa bonde la Arnon, na nusu ya nchi ya mlima wa Gileadi, na miji yake-Nilimpa Reubenites na kwa Gadites.
ויתר הגלעד וכל הבשן ממלכת עוג--נתתי לחצי שבט המנשה כל חבל הארגב לכל הבשן ההוא יקרא ארץ רפאים 13
Waliobaki wa Gileadi na Bashani yote, ufalme wa Ogi, Niliwapa nusu kabila la Manasseh: kwa wote wa Argob, na Bashani yote. (Eneo hilo linaitwa nchi ya Refaim)
יאיר בן מנשה לקח את כל חבל ארגב עד גבול הגשורי והמעכתי ויקרא אתם על שמו את הבשן חות יאיר עד היום הזה 14
Jair, mzao wa Manasseh, alichukuwa mkoa wote wa Argob, kuelekea mpaka wa Geshunites na wa Maacathites. Aliita mkoa hata Bashani kwa jina lake, Havvothi Jair, hadi leo.)
ולמכיר נתתי את הגלעד 15
Nilimpa Gileadi kwa Machir.
ולראובני ולגדי נתתי מן הגלעד ועד נחל ארנן תוך הנחל וגבל--ועד יבק הנחל גבול בני עמון 16
Kwa Reubenites na kwa Gadites nilitoa eneo kutoka kwa Gileadi kuelekea bonde la Arnon- katikati mwa bonde ni mpaka wa eneo- na kuelekea mto wa Jabbok, ambao umepakana ni wazao wa Ammoni.
והערבה והירדן וגבל--מכנרת ועד ים הערבה ים המלח תחת אשדת הפסגה מזרחה 17
Moja ya mipaka mingine pia ni tambarare ya bonde la mto wa Yordani, kutoka Chinnerethi kuelekea bahari ya Arabah(ambayo ni bahari ya Chumvi) kuelekea miteremko wa mlima wa Pisgah mashariki.
ואצו אתכם בעת ההוא לאמר יהוה אלהיכם נתן לכם את הארץ הזאת לרשתה--חלוצים תעברו לפני אחיכם בני ישראל כל בני חיל 18
Nilikuamuru wewe kwa wakati huo, kusema, Yahwe Mungu wako amekupa nchi hii kuimiliki, wewe, wamaume wote wa vita, watapita wakiwa na silaha mbele ya ndugu zako, watu wa Israeli.
רק נשיכם וטפכם ומקנכם ידעתי כי מקנה רב לכם--ישבו בעריכם אשר נתתי לכם 19
Lakini wake zenu, watoto wenu, na ng'ombe zenu (najua ya kuwa una ng'ombe wengi) watabaki katika miji yenu niliyowapa,
עד אשר יניח יהוה לאחיכם ככם וירשו גם הם את הארץ אשר יהוה אלהיכם נתן להם בעבר הירדן ושבתם איש לירשתו אשר נתתי לכם 20
mpaka Yahwe awape pumziko ndugu zenu, kama alivyo kwenu, mpaka wamiliki pia nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa ng'ambo ya pili Yordani, kisha mtageuka, kila mtu wenu, kwa mali zenu ambazo nimekwishawapa.
ואת יהושוע צויתי בעת ההוא לאמר עיניך הראת את כל אשר עשה יהוה אלהיכם לשני המלכים האלה--כן יעשה יהוה לכל הממלכות אשר אתה עבר שמה 21
Nilimwamuru Yoshua kwa wakati huo, kusema, 'Macho yenu yameona yote yale Yahwe Mungu wenu amefanya kwa hawa wafalme wawili; Yahwe atafanya hivyo kwa falme zote kote mtakakoenda.
לא תיראום כי יהוה אלהיכם הוא הנלחם לכם 22
Hamtawaogopa, kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ndiye atakaoawapigania.'
ואתחנן אל יהוה בעת ההוא לאמר 23
Nilimsihi Yahwe kwa wakati huo, kusema,
אדני יהוה אתה החלות להראות את עבדך את גדלך ואת ידך החזקה--אשר מי אל בשמים ובארץ אשר יעשה כמעשיך וכגבורתך 24
'O Bwana Yahwe, umeanza kumuonesha mtumwa wako ukuu wako na mkono wako wa hodari; kwa kuwa nani mungu aliyeko huko mbinguni au duniani ambaye anaweza kufanya kazi zilezile kama ilivyofanya, na matendo yaleyale makuu?
אעברה נא ואראה את הארץ הטובה אשר בעבר הירדן ההר הטוב הזה והלבנן 25
Hebu niende juu, Ninakuoma, na nione nchi nzuri ambayo ng'ambo ya pili ya Yordani, ile nchi nzuri ya mlima, na pia Lebanoni.
ויתעבר יהוה בי למענכם ולא שמע אלי ויאמר יהוה אלי רב לך--אל תוסף דבר אלי עוד בדבר הזה 26
Lakini Yahwe alikuwa amenikasirikia mimi kwa sababu yenu, hakunisikiliza mimi. Yahwe alisema kwangu, “Hebu hii iwe ya kutosha kwako - usizungumze zaidi tena kwangu kuhusu jambo hili.
עלה ראש הפסגה ושא עיניך ימה וצפנה ותימנה ומזרחה--וראה בעיניך כי לא תעבר את הירדן הזה 27
nenda juu ya kilele cha Pisgah na uinue macho yako magharibi, mashariki, kusini na mashariki; tazama kwa macho yako kwa kuwa hautaenda zaidi ya Yordani.
וצו את יהושע וחזקהו ואמצהו כי הוא יעבר לפני העם הזה והוא ינחיל אותם את הארץ אשר תראה 28
Badala yake, mwelekeze Yoshua na kumtia moyo na kumuimarisha, kwa kuwa ataenda zaidi mbele ya watu, na atawasababisha kuirithi nchi ambayo mtaiona.
ונשב בגיא מול בית פעור 29
Kwa hiyo tulibaki katika bonde mkabala mwa Beth Peor.

< דברים 3 >