< דברי הימים ב 35 >

ויעש יאשיהו בירושלם פסח ליהוה וישחטו הפסח בארבעה עשר לחדש הראשון 1
Yosia asherehekea Pasaka kwa ajili ya Yahwe katika Yerusalemu, na wakachinja wanakondoo katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
ויעמד הכהנים על משמרותם ויחזקם לעבודת בית יהוה 2
Akawaweka makauhuni katika nafasi zao na akawatia moyo katika hudumza za nyumba ya Yahwe.
ויאמר ללוים המבונים (המבינים) לכל ישראל הקדושים ליהוה תנו את ארון הקדש בבית אשר בנה שלמה בן דויד מלך ישראל--אין לכם משא בכתף עתה עבדו את יהוה אלהיכם ואת עמו ישראל 3
Akasema kwa Walawi waliowafundisha Israeli wote na waliokuwa wamewekwa wakifu kwa Yahwe. “Liwekeni sanduka takatifu katika nyumba ambayo Selemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli aliijenga. Msilibebe kuzunguka nalo tena mabegani mwenu. Sasa mwabuduni Yahwe Mungu wenu, na watumikieni watu wake Israeli.
והכונו (והכינו) לבית אבותיכם כמחלקותיכם--בכתב דויד מלך ישראל ובמכתב שלמה בנו 4
Jikusanyeni wenyewe kwa majina ya nyumba za babu zenu na zamu zenu, mkifuata maelekezo ya Daudi, mfalme wa Israeli, na yale ya Selemani, mwaye.
ועמדו בקדש לפלוגת בית האבות לאחיכם בני העם--וחלקת בית אב ללוים 5
Simeni katika sehemu takatifu, mkichukua nafasi zenu kwa zamu zenu ndani ya nyumba za mababu wa bdugu zenu, uzao wa watu, na mchukue sehemu zenu kwa zamu zenu ndani ya nyumba za mababu wa Walawi.
ושחטו הפסח והתקדשו והכינו לאחיכם לעשות כדבר יהוה ביד משה 6
Chinjeni wanakondoo wa Paska, jitakaseni wenyewe, andaeni wankondoo kwa ajili ya ndugu zenu, kufanya sawa sawa na neno la Yahwe ambalo lilitolewa kwa mkono wa Musa”.
וירם יאשיהו לבני העם צאן כבשים ובני עזים הכל לפסחים לכל הנמצא למספר שלשים אלף ובקר שלשת אלפים אלה מרכוש המלך 7
Yosia akawapa watu wote wanakondoo elfu thelathini na wanambuzi kutoka katika makundi kwa ajili ya sadaka za Pasaka kwa wote walikuwepo. Pia akatoa ng'ombe dume elfu tatu; hawa walikuwa kutoka katika mali ya mfalame.
ושריו לנדבה לעם לכהנים וללוים--הרימו חלקיה וזכריהו ויחיאל נגידי בית האלהים לכהנים נתנו לפסחים אלפים ושש מאות ובקר שלש מאות 8
Viongozi wake wakatoa sadaka za hiari kwa watu, makuhani, na Walawi. Hilki, Zekaria, na Yeieli, viongozi wasimamizi wa nyumba ya Mungu, wakawapa makuhani ndama 2, 600 na maksai mia tatu kwa ajili ya matoleo ya Paska.
וכונניהו (וכנניהו) ושמעיהו ונתנאל אחיו וחשביהו ויעיאל ויוזבד--שרי הלוים הרימו ללוים לפסחים חמשת אלפים ובקר חמש מאות 9
Pia Konania, Shemaya na Nethaneli, ndugu zake, na Hashabia, Yeieli, na Yazabadi, mkuu wa Walawi, akawapa Walawi ndama elfu tano kwa ajili ya matoleo ya Pasaka.
ותכון העבודה ויעמדו הכהנים על עמדם והלוים על מחלקותם כמצות המלך 10
Kwa hiyo huduma iliandaliwa, na makuhani wakasimama katika sehemu zao, pamoja na Walawi kwa zamu zao, kwa mjibu wa agizo la mfalme.
וישחטו הפסח ויזרקו הכהנים מידם והלוים מפשיטים 11
Wakawachinja wanakondoo wa Pasaka, na makuhani wakainyunyiza damu waliyoipokea kutoka kwenye mikono ya Walawi, na Walawi wakawachuna wanakondoo.
ויסירו העלה לתתם למפלגות לבית אבות לבני העם להקריב ליהוה ככתוב בספר משה וכן לבקר 12
Wakaziondoa sadaka za kuteketezwa, ili kuzisambaza katika makundi ya nyumba za mababu wa watu, ili wamtolee Yahwe, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Musa. Wakafanya vile vile kwa wale ng'ombe dume.
ויבשלו הפסח באש כמשפט והקדשים בשלו בסירות ובדודים ובצלחות ויריצו לכל בני העם 13
Wakawaoka kwa moto wanakondoo wa Pasaka wakifuata maelekezo, kuhusu sadaka takatifu, walizichemsha kwenye vyungu, masufuria na makaangoni, na haraka wayapeleka kwa watu.
ואחר הכינו להם ולכהנים--כי הכהנים בני אהרן בהעלות העולה והחלבים עד לילה והלוים הכינו להם ולכהנים בני אהרן 14
Baadaye waliandaa sadaka kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, kwa sababu makuhani, uzao wa Haruni, walikuwa wametingwa katika kazi ya kutoa sadaka za kuteketezwa na za mafuta hadi usiku ulipoingia, kwa hiyo Walawi wakaandaa sadaka kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, wana wa Haruni.
והמשררים בני אסף על מעמדם כמצות דויד ואסף והימן וידתון חוזה המלך והשערים לשער ושער אין להם לסור מעל עבדתם--כי אחיהם הלוים הכינו להם 15
Waimbaji, wana wa Asafu, walikuwa katika nafasi zao, kama ilivyoagiwa na Daudi, Asafu, Hemani, na Yeduthuni, mwonaji wa mfalme, na walinzi walikuwa katika kila lango. Hawakutakiwa kuviacha vituo vyao, kwa sababu ndugu zao Walawi walifanya maandalizi kwa ajili yao.
ותכון כל עבודת יהוה ביום ההוא לעשות הפסח והעלות עלות על מזבח יהוה--כמצות המלך יאשיהו 16
Kwa hiyo, wakati huo huduma yote ya Yahwe ilifanyika kwa ajili ya kusherekea Pasaka na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Yahwe, Kama alivyoamuru mfalme Yosia.
ויעשו בני ישראל הנמצאים את הפסח בעת ההיא ואת חג המצות שבעת ימים 17
Watu wa Israeli ambao walikuwepo wakaishika Sabato wakati huo, na kisha Sikukuu ya Mikate isiyochachwa kwa siku saba.
ולא נעשה פסח כמהו בישראל מימי שמואל הנביא וכל מלכי ישראל לא עשו כפסח אשר עשה יאשיהו והכהנים והלוים וכל יהודה וישראל הנמצא ויושבי ירושלם 18
Pasika kama hiyo haijafanyika tena katika Israeli tangu siku za nabii Samweli, wala hakuna mfalme yeyote miongoni mwa wafalme wa Israeli ambaye amewahi kusherekea Pasaka kama Yosia alivyofanya, pamoja na makuhani, Walawi, na watu wote wa Yuda na Israeli waliokuwepo, na wakaaji wote wa Yerusalemu.
בשמונה עשרה שנה למלכות יאשיהו--נעשה הפסח הזה 19
Pasaka hii ilitunzwa ndani ya miaka kumi na nane ya utawala wa Yosia.
אחרי כל זאת אשר הכין יאשיהו את הבית עלה נכו מלך מצרים להלחם בכרכמיש על פרת ויצא לקראתו יאשיהו 20
Baada ya haya yote, baada ya Yosia kuliweka hekalu katika utaratibu, Neko, mfalme wa Misiri, akaenda juu kupigana dhidi ya Karkemist karibu na mto Frati, na Yosia akaenda kupigana juu yake.
וישלח אליו מלאכים לאמר מה לי ולך מלך יהודה לא עליך אתה היום כי אל בית מלחמתי ואלהים אמר לבהלני חדל לך מאלהים אשר עמי ואל ישחיתך 21
Lakini Niko akatuma wajumbe kwake, akisema, “Nikufanye nini, mfalme wa Yuda? Leo siji kinyume nawe, lakini dhidi ya nyumba ambayo nafanya vita nayo. Mungu ameniamuru kuwahi, hivyo acha kumwingilia Mungu, ambaye yuko pamoja nami, la sivyo atakuangamiza.”
ולא הסב יאשיהו פניו ממנו כי להלחם בו התחפש ולא שמע אל דברי נכו מפי אלהים ויבא להלחם בבקעת מגדו 22
Hata hivyo, Yosia alipuuzia kurudi nyuma. Akajibadili ili apigane naye. Hakusikiliza maneno ya Neko ambayo yalikuja kutoka kwenye kinywa cha Mungu; hivyo akaenda kupigana kataika bonde la Megido.
וירו הירים למלך יאשיהו ויאמר המלך לעבדיו העבירוני כי החליתי מאד 23
Wapiga upinde wakampiga Mfalme Yosia, na mfalme akawaambia watumishi wake, “Niondoeni hapa, kwa maana nimejeruhiwa vibaya.”
ויעבירהו עבדיו מן המרכבה וירכיבהו על רכב המשנה אשר לו ויוליכהו ירושלם וימת ויקבר בקברות אבתיו וכל יהודה וירושלם מתאבלים על יאשיהו 24
Kwa hiyo watumishi wake wakamtoa nje ya gari, na kumuweka katika gari lake la tahadhari. Wakampeleka Yerusalemu, ambako alikufa. Alzikwa katika makaburi ya babu zake. Yuda wote na Yerusalemu wakamwomboleza.
ויקונן ירמיהו על יאשיהו ויאמרו כל השרים והשרות בקינותיהם על יאשיהו עד היום ויתנום לחק על ישראל והנם כתובים על הקינות 25
Yeremia akamwomboleza Yosia; waimbaji wote wa kiume na wa kike wakaomboleza kuhusu Yosia hata leo. Nyimbo hizi zikawa desturi katika Israeli; tazama, zimeandikwa katika nyimbo za maombolezo.
ויתר דברי יאשיהו וחסדיו--ככתוב בתורת יהוה 26
Kwa mambao mengine kuhusu Yosia, na matendo yake mema aliyoyafanya katika utii kwa kile kilichoandikwa katika sheria ya Yahwe—
ודבריו הראשנים והאחרנים--הנם כתובים על ספר מלכי ישראל ויהודה 27
na matendo yake, kutoka mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.

< דברי הימים ב 35 >