< דברי הימים ב 27 >
בן עשרים וחמש שנה יותם במלכו ושש עשרה שנה מלך בירושלם ושם אמו ירושה בת צדוק | 1 |
Yothamu alikuwa na umri wa mika ishirini na mitano alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yerusha; alikuwa binti Sadoki.
ויעש הישר בעיני יהוה ככל אשר עשה עזיהו אביו--רק לא בא אל היכל יהוה ועוד העם משחיתים | 2 |
Akafanya yaliyomema katika macho ya Yawe, akiufuta mfano wa baba yake, Uzia, katika mabo yote. Pia alijiepusha kuingia katika hekalu la Yahwe. Lakini watu bado walikuwa wanaenda katika njia za uovu.
הוא בנה את שער בית יהוה--העליון ובחומת העפל בנה לרב | 3 |
Akalijenga tena lango la juu la nyumba ya Yahwe, na juu ya kilima cha Ofeli akajenga sana.
וערים בנה בהר יהודה ובחרשים בנה בירניות ומגדלים | 4 |
Vilevile alijenga miji katika kilima cha Yuda, na katika mistu alijenga ngome na minara.
והוא נלחם עם מלך בני עמון ויחזק עליהם ויתנו לו בני עמון בשנה ההיא מאה ככר כסף ועשרת אלפים כרים חטים ושעורים עשרת אלפים זאת השיבו לו בני עמון ובשנה השנית והשלשית | 5 |
Pia alipigana na mfalme wa watu wa Amoni na akawashinda. Katika mwaka huo huo, watu wa Amoni walimpa talanta mia moja za fedha, kori elfu kumi za ngano, kori elfu kumi za shayiri. Watu wa Amoni wakampa hivyo hivyo katika mwaka wa pili na wa tatu.
ויתחזק יותם כי הכין דרכיו לפני יהוה אלהיו | 6 |
Kwa hiyo Yothamu akawa na nguvu sana kwa sababu alitembea imara mbele za Yahwe Mungu wake.
ויתר דברי יותם וכל מלחמתיו ודרכיו--הנם כתובים על ספר מלכי ישראל ויהודה | 7 |
Kwa mambo mengine kuhusu Yothamu, vita vyake vyote, na njia zake zote, ona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.
בן עשרים וחמש שנה היה במלכו ושש עשרה שנה מלך בירושלם | 8 |
Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi na sita kataika Yerusalemu.
וישכב יותם עם אבתיו ויקברו אתו בעיר דויד וימלך אחז בנו תחתיו | 9 |
Yothamu akalala pamoja na babu zake, na wakamzika katika mji wa Daudi. Ahazi, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.