< דברי הימים ב 13 >
בשנת שמונה עשרה למלך ירבעם וימלך אביה על יהודה | 1 |
Katika mwaka wa kumi na nane wa Mfalme Yeroboamu, Abiya akaanza kutawala juu ya Yuda.
שלוש שנים מלך בירושלם ושם אמו מיכיהו בת אוריאל מן גבעה ומלחמה היתה בין אביה ובין ירבעם | 2 |
Akatawala kwa miaka mitatu katika Yerusalemu; jina la mama yake aliitwa Maaka, binti wa Urieli wa Gibea. Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
ויאסר אביה את המלחמה בחיל גבורי מלחמה ארבע מאות אלף איש בחור וירבעם ערך עמו מלחמה בשמונה מאות אלף איש בחור גבור חיל | 3 |
Abiya akaingia vitani na jeshi la askari, wenye nguvu, hodari, 400, 00 wanaume waliochaguliwa. Yeroboamu akapanga mistari ya vita dhidi yake yenye 800, 00 wanaume askari waliochaguliwa, wenye nguvu, hodari.
ויקם אביה מעל להר צמרים אשר בהר אפרים ויאמר שמעוני ירבעם וכל ישראל | 4 |
Abiya akasimama juu ya mlima Semaraimu, uliopo katika kilima cha nchi ya Efraimu, na akasema, “Nisikilizeni, Yeroboamu na Israeli wote!
הלא לכם לדעת כי יהוה אלהי ישראל נתן ממלכה לדויד על ישראל לעולם לו ולבניו ברית מלח | 5 |
Hamjui kwamba Yahwe, Mungu wa Israeli, alitoa sheria juu ya Israeli kwa Daudi milele, kwake na kwa wanaye kwa agano rasimi?
ויקם ירבעם בן נבט עבד שלמה בן דויד וימרד על אדניו | 6 |
Bado Yeroboamu mwana wa Nebati, mtumishi wa Selemani mwana wa Daudi, akainuka na kuasi dhidi ya bwana wake.
ויקבצו עליו אנשים רקים בני בליעל ויתאמצו על רחבעם בן שלמה ורחבעם היה נער ורך לבב ולא התחזק לפניהם | 7 |
Watu wabaya, washirika wa karibu, wakamkusanyikia, wakamjia kinyume Rehoboamu mwana wa Selemani, wakati Rehoboamu alipokuwa mdogo na asiye na uzoefu na hakuweza kuwamudu.
ועתה אתם אמרים להתחזק לפני ממלכת יהוה ביד בני דויד ואתם המון רב ועמכם עגלי זהב אשר עשה לכם ירבעם לאלהים | 8 |
Sasa mnasema kwamba mnaweza kuuzuia utawala wa Yahwe wenye nguvu katika mkono wa uzao wa Daudi. Ninyi ni jeshsi kubwa, na pamoja nanyi kuna ndama wa dhahabu ambao Yeroboamu alitengeneza kama miungu kwa ajili yenu.
הלא הדחתם את כהני יהוה את בני אהרן והלוים ותעשו לכם כהנים כעמי הארצות--כל הבא למלא ידו בפר בן בקר ואילם שבעה והיה כהן ללא אלהים | 9 |
Hamkuwafukuza nje makuhani wa Yahwe, uzao wa Haruni, na Walawi? Hamkujifanyia makuhani katika namna ya watu wa nchi zingine? Yeyote ajaye kujitakasa mwenyewe na ngo'mbe dume kijana, na madume ya kondoo anaweza kuwa kuhani wa kile ambacho siyo miungu.
ואנחנו יהוה אלהינו ולא עזבנהו וכהנים משרתים ליהוה בני אהרן והלוים במלאכת | 10 |
Lakini kwetu, Yahwe ni Mungu wetu, na hatujamsahau. Tuna makuhani, uzao wa Haruni, wakimtumikia Yahwe, na Walawi, ambao wako kataika kazi yao.
ומקטרים ליהוה עלות בבקר בבקר ובערב בערב וקטרת סמים ומערכת לחם על השלחן הטהור ומנורת הזהב ונרתיה לבער בערב בערב--כי שמרים אנחנו את משמרת יהוה אלהינו ואתם עזבתם אתו | 11 |
Kila asubuhi na jioni humtolea Yahwe sadaka za kuteketezwa na uvumba mtamu. Pia hupanga mkate wa uwepo juu ya meza takatifu; pia huweka kinara cha dhahabu pamoaja na taa zake, ili watoe sadaka kila jioni. sisi huzishika sheria za Yahwe, Mungu wetu, Lakini ninyi mmemsahau.
והנה עמנו בראש האלהים וכהניו וחצצרות התרועה--להריע עליכם בני ישראל אל תלחמו עם יהוה אלהי אבתיכם--כי לא תצליחו | 12 |
Ona, Mungu yuko pamoja nasi katika vichwa vyetu, na makuhani wake wako hapa na tarumbeta kwa ajili ya kutoa sauti dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane na Yahwe, Mungu wa babu zenu, kwa maana hamtafanikiwa.”
וירבעם הסב את המארב לבוא מאחריהם ויהיו לפני יהודה והמארב מאחריהם | 13 |
Lakini Yeroboamu akaandaa mavamizi nyuma yao; jeshi lake lilikuwa mbele ya Yuda, na wavamizi nyuma yao.
ויפנו יהודה והנה להם המלחמה פנים ואחור ויצעקו ליהוה והכהנים מחצצרים (מחצרים) בחצצרות | 14 |
Yuda walipoanagalia nyuma, tanzama, mapigano yalikuwa pote mbele na nyuma yao. Wakamlilia Yahwe kwa sauti, na makuhani wakayapuliza matarumbeta.
ויריעו איש יהודה ויהי בהריע איש יהודה והאלהים נגף את ירבעם וכל ישראל לפני אביה ויהודה | 15 |
Kisha wanaume wa Yuda wakapiga kelele; walipopiga kele, ikawa kwamba Mungu akampiga Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Abiya na Yuda.
וינוסו בני ישראל מפני יהודה ויתנם אלהים בידם | 16 |
Watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Yuda, na akawatia kwenye mkono wa Yuda.
ויכו בהם אביה ועמו מכה רבה ויפלו חללים מישראל חמש מאות אלף איש בחור | 17 |
Abiya na jeshi lake wakawaua kwa mauji makuu; 500, 000 watu wanaume waliochaguliwa wa Israeli wakaanguka wamekufa.
ויכנעו בני ישראל בעת ההיא ויאמצו בני יהודה כי נשענו על יהוה אלהי אבותיהם | 18 |
Katika namna hii hii, watu wa Israeli wakatiishwa chini wakati huo, watu wa Yuda wakashinda kwa sababu walimtegemea Yahwe, Mungu wa babu zao.
וירדף אביה אחרי ירבעם וילכד ממנו ערים את בית אל ואת בנותיה ואת ישנה ואת בנותיה ואת עפרון (עפרין) ובנתיה | 19 |
Abiya akamshawishi Yeroboamu; akachukua miji kutoka kwake; Betheli pamoja na vijiji vyake, Yeshana pamoja na vijiji vyake, na Efroni pamoaaja na vijij vyake.
ולא עצר כח ירבעם עוד בימי אביהו ויגפהו יהוה וימת | 20 |
Yeroboamu hakupata naguvu tena katika siku za Abiya; Yahwe akampiga, na akafa.
ויתחזק אביהו--וישא לו נשים ארבע עשרה ויולד עשרים ושנים בנים ושש עשרה בנות | 21 |
Lakini Abiya akawa na nguvu sana; akachukua wanawake kumi na nne kwa ajili yake na akawa baba wa wana ishirini na mbili na mabinti kumi na sita.
ויתר דברי אביה ודרכיו ודבריו--כתובים במדרש הנביא עדו | 22 |
Matendo ya Abiya yaliyosalia, tabia yake na maneno yake yameeandikwa katika kamusi ya nabii Ido.