< דברי הימים א 16 >

ויביאו את ארון האלהים ויציגו אתו בתוך האהל אשר נטה לו דויד ויקריבו עלות ושלמים לפני האלהים 1
Wakaleta ndani Sanduku la Mungu na kuweka katika ya hema ambalo Daudi aliandaa. Kisha wakatoa sadaka ya kuteketeza na sadaka ya ushirika mbele ya Mungu.
ויכל דויד מהעלות העלה והשלמים ויברך את העם בשם יהוה 2
Daudi alipo maliza kutoa dhabiu ya kuteketeza na sadaka za ushirika, aliwabariki watu kwa jina la Yahweh.
ויחלק לכל איש ישראל מאיש ועד אשה--לאיש ככר לחם ואשפר ואשישה 3
Alisambaza kwa kila Misraeli, mwanaume na mwanamke, kipande cha mkate, na kipande cha nyama, na keki ya mzabibu.
ויתן לפני ארון יהוה מן הלוים--משרתים ולהזכיר ולהודות ולהלל ליהוה אלהי ישראל 4
Daudi aliewapangia baadhi ya Walawi kutumika mbele ya sanduku la Yahweh, na kusheherekea, kushukuru na kumsifu Yahweh, Mungu wa Israeli.
אסף הראש ומשנהו זכריה יעיאל ושמירמות ויחיאל ומתתיה ואליאב ובניהו ועבד אדם ויעיאל בכלי נבלים ובכנרות ואסף במצלתים משמיע 5
Hawa Walawi walikuwa Asafu kiongozi, wa pili kutoka kwake Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaia, Obedi Edomu, na Yeieli. Hawa walikuwa wacheze na vyombo vya uzi na vinubi. Asafu alikuwa apige upatu, kwa kelele.
ובניהו ויחזיאל הכהנים--בחצצרות תמיד לפני ארון ברית האלהים 6
Benaia na Yahazieli walikuwa wakupiga tarumbeta kila mara, mbele sanduku la agano la Mungu.
ביום ההוא אז נתן דויד בראש להדות ליהוה--ביד אסף ואחיו 7
Kisha katika hiyo siku Daudi akawachagua Asafu na kaka zake kuimba hii nyimbo ya shukurani kwa Yahweh.
הודו ליהוה קראו בשמו-- הודיעו בעמים עלילתיו 8
Mpeni shukurani Yahweh, liitieni jina lake; fahamisheni mataifa matendo yake.
שירו לו זמרו לו-- שיחו בכל נפלאתיו 9
Mwiimbieni, imbeni sifa kwake; semeni matendo yake ya ajabu.
התהללו בשם קדשו-- ישמח לב מבקשי יהוה 10
Jisifuni katika jina lake takatifu; mioyo ya wanao mtafuta Yahweh ishangilie.
דרשו יהוה ועזו-- בקשו פניו תמיד 11
Mtafute Yahweh na nguvu zake; tafuteni uwepo wake siku zote.
זכרו נפלאתיו אשר עשה-- מפתיו ומשפטי פיהו 12
Kumbukeni matendo aliyo ya fanya kwenu, miujiza yake na amri za kinywa chake,
זרע ישראל עבדו-- בני יעקב בחיריו 13
enyi uzao wa Israeli mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wateule wake.
הוא יהוה אלהינו-- בכל הארץ משפטיו 14
Yeye ni Yahweh, Mungu wetu. Amri zake zipo duniani kote.
זכרו לעולם בריתו-- דבר צוה לאלף דור 15
Tunzeni agano lake akilini mwenu milele, neno alilo liamuru kwa vizazi elfu moja.
אשר כרת את אברהם-- ושבועתו ליצחק 16
Anakumbuka agano alilo lifanya na Ibrahimu, na nadhiri yake kwake Isaka.
ויעמידה ליעקב לחק-- לישראל ברית עולם 17
Hili ndilo alilo lithibitisha kwa Yakobo kama amri maalumu, na kwa Israeli kama agano la milele.
לאמר לך אתן ארץ כנען-- חבל נחלתכם 18
Alisema, “Nitakupa nchi ya Kanani kama sehemu ya urithi wako.”
בהיותכם מתי מספר-- כמעט וגרים בה 19
Nilisema hili mlipo kuwa wachache kwa idadi, wachache sana, mlipo kuwa wageni katika nchi.
ויתהלכו מגוי אל גוי-- ומממלכה אל עם אחר 20
Walienda taifa hadi taifa, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
לא הניח לאיש לעשקם-- ויוכח עליהם מלכים 21
Hakuwaruhusu yeyote awatese; aliwahadhibu wafalme kwa ajili yao.
אל תגעו במשיחי-- ובנביאי אל תרעו 22
Alisema, “Msiwaguse wapakwa mafuta wangu, na msiwadhuru manabii wangu.”
שירו ליהוה כל הארץ-- בשרו מיום אל יום ישועתו 23
Imbeni kwa Yahweh, dunia yote; tangazeni wokovu wake siku hadi siku.
ספרו בגוים את כבודו-- בכל העמים נפלאתיו 24
Kirini utukufu wake kwa mataifa, matendo yake makuu kwa mataifa yote.
כי גדול יהוה ומהלל מאד-- ונורא הוא על כל אלהים 25
Kwa kuwa Yahweh ni mkuu na ni wakusifiwa sana, na ni wakuogopewa kuliko miungu yote.
כי כל אלהי העמים אלילים-- ויהוה שמים עשה 26
Kwa kuwa miungu ya mataifa ni sanamu, lakini ni Yahweh aliye umba mbingu.
הוד והדר לפניו-- עז וחדוה במקמו 27
Uzuri wa ajabu na utukufu upo uweponi mwake. Uwezo na furaha upo kwake.
הבו ליהוה משפחות עמים-- הבו ליהוה כבוד ועז 28
Mpeni sifa Yahweh, enyi koo za watu, mpeni sifa Yahweh utukufu na uwezo;
הבו ליהוה כבוד שמו שאו מנחה ובאו לפניו-- השתחוו ליהוה בהדרת קדש 29
Mpeni Yahweh utukufu upasao jina lake. Leta sadaka na mje kwake. Muinamieni Yahweh katika utakatifu wa uzuri wake.
חילו מלפניו כל הארץ-- אף תכון תבל בל תמוט 30
Mtetemeke mbele zake, dunia yote. Dunia imeimarishwa; haiwezi kutikisika.
ישמחו השמים ותגל הארץ-- ויאמרו בגוים יהוה מלך 31
Mbingu nazo ziwe nafuraha, na dunia ifurahi; na wasema kwa mataifa yote, “Yahweh anatawala.”
ירעם הים ומלואו-- יעלץ השדה וכל אשר בו 32
Bahari na ingurume, na inayo ijaza ipige kelele kwa furaha. Mashamba yawe na furaha tele, na vyote vilivyomo ndani yake.
אז ירננו עצי היער מלפני יהוה--כי בא לשפוט את הארץ 33
Na miti iliyopo misituni ipige kelele kwa Yahweh, kwa kuwa anakuja kuhukumu dunia.
הודו ליהוה כי טוב-- כי לעולם חסדו 34
Toeni shukurani kwa Yahweh, kwa kuwa ni mwema, uaminifu wa agano lake la dumu ata milele.
ואמרו--הושיענו אלהי ישענו וקבצנו והצילנו מן הגוים להדות לשם קדשך להשתבח בתהלתך 35
Kisha sema, “Tuokoe, Mungu wa wokovu wetu. Tukusanye pamoja na utuokoe kutoka kwa mataifa mengine, ilikwamba tutoe shukurani kwa jina lako takatifu na tufurahi katika sifa zako.”
ברוך יהוה אלהי ישראל-- מן העולם ועד העלם ויאמרו כל העם אמן-- והלל ליהוה 36
Na Yahweh, Mungu wa Israeli, asifiwe kutoka milele na milele. Watu wote wakasema, “Amina” na wakamsifu Yahweh.
ויעזב שם לפני ארון ברית יהוה לאסף ולאחיו לשרת לפני הארון תמיד--לדבר יום ביומו 37
Hivyo Daudi akamwacha Asafu na kaka zake pale mbele ya sanduku la Yahweh, kutumika daima mbele ya sanduku, kama kazi za kila siku zilivyo itaji. Obedi Edomu pamoja na ndugu sitini na nane walijumuishwa.
ועבד אדם ואחיהם ששים ושמונה ועבד אדם בן ידיתון וחסה לשערים 38
Obedi Edomu mwana wa Yeduthuni, pamoja na Hosa, walikuwa wawe walinzi wa lango.
ואת צדוק הכהן ואחיו הכהנים לפני משכן יהוה--בבמה אשר בגבעון 39
Zadoki kuhani na makuhani wenzake walikuwa watumike mbele ya hema la Yahweh katika mahali pa juu huko Gibeoni.
להעלות עלות ליהוה על מזבח העלה תמיד--לבקר ולערב ולכל הכתוב בתורת יהוה אשר צוה על ישראל 40
Walikuwa watoe sadaka za kuteketeza kwa Yahweh kwenye madhabahu ya sadaka za kuteketeza daima asubui na jioni, kwa mujibu wa yote yalio andikwa katika amri za Yahweh, aliyo wapa Waisraeli kama sheria.
ועמהם הימן וידותון ושאר הברורים אשר נקבו בשמות--להדות ליהוה כי לעולם חסדו 41
Hemani na Yeduthuni walikuwa nao, pamoja na walio chaguliwa kwa jina, kumpa shukurani Yahweh, kwasababu uaminifu wa agano lake la dumu ata milele
ועמהם הימן וידותון חצצרות ומצלתים למשמיעים וכלי שיר האלהים ובני ידותון לשער 42
Hemani na Yeduthuni walikuwa viongozi wa wao waliopiga tarumbeta, upatu, na vyombo vingine kwa muziki wa kumuabudu Mungu. Wana wa Yeduthuni walilinda lango.
וילכו כל העם איש לביתו ויסב דויד לברך את ביתו 43
Kisha watu wote walirudi nyumbani, na Daudi akarudi kubariki nyumba yake.

< דברי הימים א 16 >