< דברי הימים א 13 >
ויועץ דויד עם שרי האלפים והמאות--לכל נגיד | 1 |
Daudi akashuriana na wakuu wa jeshi la maelfu na mamia, na kila kiongozi.
ויאמר דויד לכל קהל ישראל אם עליכם טוב ומן יהוה אלהינו נפרצה נשלחה על אחינו הנשארים בכל ארצות ישראל ועמהם הכהנים והלוים בערי מגרשיהם ויקבצו אלינו | 2 |
Daudi akasema kwa kusanyiko la Isaraeli, “Kama itakuwa vyema, na kama hii inatoka kwa Yahweh Mungu wetu, na tutume wajumbe kila sehemu kwa ndugu zetu walio baki maeneo yote ya Israeli, na kwa makuhani na Walawi walio kwenye miji yao. Waambiwe wajiunge nasi.
ונסבה את ארון אלהינו אלינו כי לא דרשנהו בימי שאול | 3 |
Na tulete sanduku la Mungu wetu, kwa kuwa hatukutafuta mapenzi yake katika siku za Sauli.”
ויאמרו כל הקהל לעשות כן כי ישר הדבר בעיני כל העם | 4 |
Kusanyiko lote liliafiki kufanya haya yote, kwa kuwa yalionekana sawa machoni pa watu wote.
ויקהל דויד את כל ישראל מן שיחור מצרים ועד לבוא חמת להביא את ארון האלהים מקרית יערים | 5 |
Kwaiyo Daudi akakusanya Israeli yote, kutoka mto Shihori ulio Misri hadi Lebo Hamathi, kuleta sandaku la Mungu kutoka Kiriathi Yearimu.
ויעל דויד וכל ישראל בעלתה אל קרית יערים אשר ליהודה להעלות משם את ארון האלהים יהוה יושב הכרובים--אשר נקרא שם | 6 |
Daudi na Israeli yote walienda mpaka Baala, ambayo ni, Kiriathi Yearimu, ambao ni ya Yuda, kuleta sanduku la Mungu, ambalo linaitwa kwa jina la Yahweh, Yahweh, ambaye ameketi juu ya makerubi.
וירכיבו את ארון האלהים על עגלה חדשה מבית אבינדב ועזא ואחיו נהגים בעגלה | 7 |
Kwaiyo wakaketisha sanduku la Mungu juu ya chombo kipya cha matairi. Wakaleta nje ya nyumba ya Abinadabu. Uza na Ahio walikuwa wakilinda hicho chombo.
ודויד וכל ישראל משחקים לפני האלהים--בכל עז ובשירים ובכנרות ובנבלים ובתפים ובמצלתים ובחצצרות | 8 |
Daudi na Israeli yote walikuwa wakishangilia mbele za Mungu kwa nguvu zao zote. Walikuwa wakiimba na vyombo vya uzi, vinubi, upatu, na tarumbeta.
ויבאו עד גרן כידן וישלח עזא את ידו לאחז את הארון--כי שמטו הבקר | 9 |
Walipo kuja eneo la kupeta mazao huko Kidoni, Uza alinyoosha mkono wake kuzuia sandaku, sababu ng'ombe aliyekuwa amebeba sanduku aliyumba.
ויחר אף יהוה בעזא ויכהו על אשר שלח ידו על הארון וימת שם לפני אלהים | 10 |
Hasira ya Yahweh ikawaka juu ya Uza, na Yahweh akamua kwasababu Uza alishika na mkono wake sanduku. Akafa pale mbele za Mungu.
ויחר לדויד כי פרץ יהוה פרץ בעזא ויקרא למקום ההוא פרץ עזא עד היום הזה | 11 |
Daudi alipatwa na hasira kwa kuwa Yahweh alimshambulia Uza. Hiyo sehemu inaitwa Perezi Uza hadi leo.
ויירא דויד את האלהים ביום ההוא לאמר היך אביא אלי את ארון האלהים | 12 |
Daudi alimuogopa Mungu hiyo siku. Akasema, “Nawezaje kuleta sanduku la Mungu nyumbani mwangu?”
ולא הסיר דויד את הארון אליו אל עיר דויד ויטהו אל בית עבד אדם הגתי | 13 |
Kwaiyo Daudi hakuleta sanduku kwenye mji wa Daudi, lakini aliweka pembeni mwa nyumba ya Obedi Edomu Mgiti.
וישב ארון האלהים עם בית עבד אדם בביתו--שלשה חדשים ויברך יהוה את בית עבד אדם ואת כל אשר לו | 14 |
Sanduku la Mungu lilibaki nyumbani mwa Obedi Edomu kwa miezi mitatu. Kwaiyo Yahweh akabariki nyumba yake na yote aliyo miliki.