< Offenbarung 6 >

1 Und ich sah, als das Lamm eines von den sieben Siegeln öffnete: und ich hörte eines von den vier lebendigen Wesen wie eine Donnerstimme sagen:
Nikatazama wakati mwanakondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema kwa sauti iliyofanana na radi, “Njoo!”
2 Komm! Und ich sah: und siehe, ein weißes Pferd, und der darauf saß hatte einen Bogen; und eine Krone wurde ihm gegeben, und er zog aus, siegend und auf daß er siegte.
Nikatazama na palikuwa na farasi mweupe! Aliyempanda alikuwa na bakuli, na akapewa taji. Alitokea kama mshindi ashindaye ili ashinde.
3 Und als es das zweite Siegel öffnete, hörte ich das zweite lebendige Wesen sagen: Komm!
Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri wa pili, nikasikia mwenye uhai wa pili akisema, “Njoo!”
4 Und es zog aus ein anderes, feuerrotes Pferd; und dem, der darauf saß, ihm wurde gegeben, den Frieden von der Erde zu nehmen, und daß sie einander schlachteten; und ein großes Schwert wurde ihm gegeben.
Kisha farasi mwingine akatokea - mwekundu kama moto. Aliye mpanda alipewa ruhusa ya kuondoa amani duniani, ili kwamba watu wachinjane. Huyu aliye mpanda alipewa upanga mkubwa.
5 Und als es das dritte Siegel öffnete, hörte ich das dritte lebendige Wesen sagen: Komm! Und ich sah: und siehe, ein schwarzes Pferd, und der darauf saß, hatte eine Waage in seiner Hand.
Wakati mwanakondoo alipofungua ule muhuri wa tatu, nikasikia mwenye uhai wa tatu akisema, “Njoo!” Nikaona farasi mweusi, na aliyempanda ana mizani mkononi mwake.
6 Und ich hörte wie eine Stimme inmitten der vier lebendigen Wesen, welche sagte: Ein Chönix Weizen für einen Denar, und drei Chönix Gerste für einen Denar; und das Öl und den Wein beschädige nicht.
Nikasikia sauti iliyoonekana kuwa ya mmoja wa wale wenye uhai ikisema, “kibaba cha ngano kwa dinari moja na vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari moja. Lakini usiyadhuru mafuta na divai.”
7 Und als es das vierte Siegel öffnete, hörte ich [die Stimme des] vierten lebendigen Wesens sagen: Komm!
Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya nne, nilisikia sauti ya mwenye uhai wa nne ikisema, “Njoo!”
8 Und ich sah: und siehe, ein fahles Pferd, und der darauf saß, sein Name war Tod; und der Hades folgte ihm. Und ihm wurde Gewalt gegeben über den vierten Teil der Erde, zu töten mit dem Schwerte und mit Hunger und mit Tod und durch die wilden Tiere der Erde. (Hadēs g86)
Kisha nikaona farasi wa kijivu. Aliye mpanda aliitwa jina lake mauti, na kuzimu ilikuwa ikimfuata. Walipewa mamlaka juu ya robo ya nchi, kuua kwa upanga, kwa njaa na kwa ugonjwa, na kwa wanyama wa mwitu katika nchi. (Hadēs g86)
9 Und als es das fünfte Siegel öffnete, sah ich unter dem Altar die Seelen derer, welche geschlachtet worden waren um des Wortes Gottes und um des Zeugnisses willen, das sie hatten.
Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya tano, niliona chini ya madhabahu roho za wale waliokuwa wameuawa kwa sababu ya neno la Mungu na kutokana na ushuhuda walioushika kwa uthabiti.
10 Und sie riefen mit lauter Stimme und sprachen: Bis wann, o Herrscher, der du heilig und wahrhaftig bist, richtest und rächst du nicht unser Blut an denen, die auf der Erde wohnen?
Wakalia kwa sauti kuu, “mpaka lini, Mtawala wa vyote, mtakatifu na mkweli, utahukumu wakaao juu ya nchi, na kulipiza kisasi damu yetu?”
11 Und es wurde ihnen einem jeden ein weißes Gewand gegeben; und es wurde ihnen gesagt, daß sie noch eine kleine Zeit ruhen sollten, bis auch ihre Mitknechte und ihre Brüder vollendet sein würden, die ebenso wie sie getötet werden würden.
Kisha kila mmoja alipewa kanzu nyeupe na wakaambiwa kuwa wanapaswa kusubiri kidogo hata itakapotimia hesabu kamili ya watumishi wenzao na ndugu zao wa kike na wa kiume itakapotimia ambao watauawa, kama vile ambavyo wao waliuawa.
12 Und ich sah, als es das sechste Siegel öffnete: und es geschah ein großes Erdbeben; und die Sonne wurde schwarz wie ein härener Sack, und der ganze Mond wurde wie Blut,
Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya sita, nilitazama na palikuwa na tetemeko kuu. Jua likawa jeusi kama gunia la singa, na mwezi mzima ukawa kama damu.
13 und die Sterne des Himmels fielen auf die Erde, wie ein Feigenbaum, geschüttelt von einem starken Winde, seine unreifen Feigen abwirft.
Nyota za mbinguni zikaanguka katika nchi, kama mtini upukutishavyo matunda yake ya wakati wa baridi unapotikiswa na kimbunga.
14 Und der Himmel entwich wie ein Buch, das aufgerollt wird, und jeder Berg und jede Insel wurden aus ihren Stellen gerückt.
Anga ilitoweka kama gombo lililoviringishwa. Kila mlima na kisiwa vilihamishwa mahali pake.
15 Und die Könige der Erde und die Großen und die Obersten und die Reichen und die Starken und jeder Knecht und Freie verbargen sich in die Höhlen und in die Felsen der Berge;
Kisha wafalme wa nchi na watu maarufu na majemadari, matajiri, wenye nguvu, na kila mmoja aliye mtumwa na huru, wakajificha katika mapango na katika miamba ya milima.
16 und sie sagen zu den Bergen und zu den Felsen: Fallet auf uns und verberget uns vor dem Angesicht dessen, der auf dem Throne sitzt, und vor dem Zorne des Lammes;
Wakaiambia milima na miamba, “Tuangukieni! Tuficheni dhidi ya uso wake aketiye kwenye kiti cha enzi na kutoka hasira ya mwanakondoo.
17 denn gekommen ist der große Tag seines Zornes, und wer vermag zu bestehen?
Kwa kuwa siku kuu ya gadhabu yao imewadia, na ni nani awezaye kusimama?”

< Offenbarung 6 >