< Isaïe 22 >

1 Oracle contre la vallée des visions. Que t'arrive-t-il donc, que tous tes habitants sont montés sur les toits,
Neno kuhusu Bonde la Maono: Nini kinachokutaabisha sasa, kwamba ninyi nyote mmepanda juu ya mapaa?
2 ville pleine de tumulte, cité bruyante et joyeuse? Tes morts ne seront pas percés par l'épée, ni tués dans le combat.
Ewe mji uliojaa ghasia, ewe mji wa makelele na sherehe! Watu wenu waliokufa hawakuuawa kwa upanga, wala hawakufa vitani.
3 Tous tes généraux fuient ensemble, sont pris par les archers, tous ceux qui se trouvent en ton sein sont pris à la fois, ils fuient au loin.
Viongozi wako wote wamekimbia pamoja, wamekamatwa bila kutumia upinde. Ninyi nyote mliokamatwa mlichukuliwa wafungwa pamoja, mlikimbia wakati adui alipokuwa bado mbali.
4 Aussi dis-je: Détournez les yeux de moi; j'ai à pleurer amèrement: n'insistez pas pour me consoler de la ruine de la fille de mon peuple!
Kwa hiyo nilisema, “Geukia mbali nami, niache nilie kwa uchungu. Usijaribu kunifariji juu ya maangamizi ya watu wangu.”
5 Car c'est une journée de commotion et d'écrasement et de confusion que tient le Seigneur, l'Éternel des armées, dans la vallée des visions; on sape les murs, et les cris de détresse vont frapper les montagnes.
Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayo siku ya ghasia, ya kukanyaga, na ya kuogofya katika Bonde la Maono, siku ya kuangusha kuta na ya kupiga kelele mpaka milimani.
6 Elam porte le carquois sur des chars pleins d'hommes et de cavaliers, et Kir tire le bouclier du fourreau.
Elamu analichukua podo, pamoja na waendesha magari ya vita na farasi. Kiri anaifungua ngao.
7 Et tes plus belles vallées sont remplies de chars, et les cavaliers prennent position entre tes portes.
Mabonde yako yaliyo mazuri sana yamejaa magari ya vita, nao wapanda farasi wamewekwa kwenye malango ya mji;
8 Et le voile de Juda est levé, et en ce jour tu portes tes regards vers les munitions de la maison de cèdre.
ulinzi wa Yuda umeondolewa. Nawe ulitazama siku ile silaha katika Jumba la Kifalme la Mwituni,
9 Et vous apercevez les brèches de la ville de David, qui sont nombreuses, et vous recueillez les eaux de l'étang inférieur;
mkaona kuwa Mji wa Daudi una matundu mengi katika ulinzi wake, mkaweka akiba ya maji kwenye Bwawa la Chini.
10 et vous comptez les maisons de Jérusalem, et vous en abattez pour fortifier les murs,
Mlihesabu majengo katika Yerusalemu nanyi mkabomoa nyumba ili kuimarisha ukuta.
11 et vous faites un réservoir entre les deux murs pour les eaux de l'antique étang. Mais vous ne regardez pas vers l'auteur de ces choses, et ne tournez pas les yeux vers Celui qui de loin en a formé le plan.
Mlijenga bwawa la maji katikati ya kuta mbili kwa ajili ya maji ya Bwawa la Zamani, lakini hamkumtazama Yule aliyelitengeneza, au kuwa na heshima kwa Yule aliyeubuni tangu zamani za kale.
12 Et en ce jour le Seigneur, l'Éternel des armées, vous convie à pleurer, à gémir, à couper vos cheveux et à ceindre le cilice.
Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, aliwaita siku ile ili kulia na kuomboleza, kungʼoa nywele zenu na kuvaa nguo ya gunia.
13 Mais voici, plaisir et joie; on tue des taureaux, on égorge des brebis, on mange de la chair, et on boit du vin: « Mangeons et buvons, car demain nous mourrons! »
Lakini tazama, kuna furaha na sherehe, kuchinja ngʼombe na kuchinja kondoo, kula nyama na kunywa mvinyo! Mnasema, “Tuleni na kunywa, kwa kuwa kesho tutakufa!”
14 Cependant l'Éternel des armées s'est révélé à mes oreilles: Non, ce crime ne sera pas expié que vous ne soyez morts, dit le Seigneur, l'Éternel des armées.
Bwana Mwenye Nguvu Zote amelifunua hili nikiwa ninasikia: Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asema: “Mpaka siku ya kufa kwenu, dhambi hii haitafanyiwa upatanisho.”
15 Ainsi parle le Seigneur, l'Éternel des armées: Va, rends-toi vers ce courtisan, vers Sebna préposé au palais!
Hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asemalo: “Nenda ukamwambie huyu wakili Shebna, ambaye ni msimamizi wa jumba la kifalme:
16 « Qu'as-tu à faire ici? et qui as-tu ici, que tu te creuses ici un tombeau, creusant un tombeau sur la hauteur, te taillant dans le roc une demeure?
Unafanya nini hapa, na ni nani aliyekupa ruhusa kujikatia kaburi lako mwenyewe, ukichonga kaburi lako mahali palipo juu, na kutoboa kwa patasi mahali pako pa kupumzikia katika mwamba?
17 Voici, l'Éternel te jettera bas d'un coup vigoureux, et te saisira;
“Jihadhari, Bwana yu karibu kukukamata thabiti, na kukutupa mbali, ewe mtu mwenye nguvu.
18 Il te fera rouler, rouler, comme une balle sur une terre vaste et spacieuse; là tu mourras, et là seront tes chars magnifiques, toi l'opprobre de la maison de ton maître.
Atakuvingirisha uwe kama mpira na kukutupa katika nchi kubwa. Huko ndiko utakakofia, na huko ndiko magari yako ya vita ya fahari yatabakia, wewe unayeifedhehesha nyumba ya bwana wako!
19 Et je te culbuterai de ton poste, et Il te débusquera de ta place. »
Nitakuondoa kutoka kazi yako, nawe utaondoshwa kutoka nafasi yako.
20 Et en ce jour même j'adresserai vocation à mon serviteur Eliacim, fils de Hilkia;
“Katika siku ile, nitamwita mtumishi wangu, Eliakimu mwana wa Hilkia.
21 et je le revêtirai de ton manteau et le ceindrai de ta ceinture, et je mettrai ton pouvoir en sa main, et il sera un père pour les habitants de Jérusalem et pour la maison de Juda.
Nitamvika joho lako, nami nitamfunga mshipi wako kiunoni mwake, na kumkabidhi mamlaka yako. Yeye atakuwa baba kwa wale wanaoishi Yerusalemu na kwa nyumba ya Yuda.
22 Et je mettrai la clef de la maison de David sur son épaule, et il ouvrira, et personne ne fermera; il fermera, et personne n'ouvrira.
Nitaweka mabegani mwake ufunguo wa nyumba ya Daudi. Kile afunguacho hakuna awezaye kufunga, na kile afungacho hakuna awezaye kufungua.
23 Et je l'enfoncerai comme un clou en lieu sûr, et il sera un trône glorieux pour la maison de son père;
Nitamgongomea kama kigingi kilicho mahali palipo imara, naye atakuwa kiti cha enzi cha heshima kwa ajili ya nyumba ya baba yake.
24 et il sera le soutien de tout ce qui est la gloire de la maison de son père, des rejetons et des surgeons, de tous les petits vases depuis les bassins jusqu'à toutes les coupes.
Utukufu wote wa jamaa yake utakuwa juu yake: Watoto wa jamaa hiyo na machipukizi yake, vyombo vyake vyote vidogo, tangu bakuli hadi magudulia yote.”
25 En ce même jour, dit l'Éternel des armées, sera ôté le clou enfoncé en lieu sûr; il sera abattu et tombera, et le fardeau qu'il portait croulera, car l'Éternel l'a prononcé.
Bwana Mwenye Nguvu Zote asema, “Katika siku ile, kigingi kilichogongomewa mahali imara kitaachia njia. Kitakatwa, nacho kitaanguka na mzigo ulioningʼinia juu yake utaanguka chini.” Bwana amesema.

< Isaïe 22 >