< Ézéchiel 27 >
1 Et la parole de l’Éternel vint à moi, disant:
Neno la Bwana likanijia kusema:
2 Et toi, fils d’homme, élève une complainte sur Tyr,
“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Tiro.
3 et dis à Tyr: [Toi] qui demeures aux avenues de la mer, qui trafiques avec les peuples dans beaucoup d’îles, ainsi dit le Seigneur, l’Éternel: Tyr, tu as dit: Je suis parfaite en beauté.
Umwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “‘Ee Tiro, wewe umesema, “Mimi ni mkamilifu katika uzuri.”
4 Tes frontières sont au cœur des mers; ceux qui t’ont bâtie ont rendu ta beauté parfaite.
Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari, wajenzi wako walikamilisha uzuri wako.
5 Avec le cyprès de Senir ils construisaient tous tes doubles bordages; ils prenaient le cèdre du Liban pour faire ta mâture;
Walizifanya mbao zako zote kwa misunobari itokayo Seniri; walichukua mierezi kutoka Lebanoni kukutengenezea mlingoti.
6 avec les chênes de Basan ils faisaient tes rames; ils faisaient tes ponts d’ivoire enchâssé dans le buis des îles de Kittim.
Walichukua mialoni toka Bashani wakakutengenezea makasia yako; kwa miti ya msanduku kutoka pwani ya Kitimu wakatengeneza sitaha yako na kuipamba kwa pembe za ndovu.
7 Le fin lin brodé d’Égypte était ta voile [et] te servait de pavillon; le bleu et la pourpre des îles d’Élisha étaient ta tente;
Kitani safi kilichotariziwa kutoka Misri kilikuwa tanga lako, nacho kilikuwa bendera yako; chandarua chako kilikuwa cha rangi ya buluu na ya zambarau kutoka visiwa vya Elisha.
8 les habitants de Sidon et d’Arvad étaient tes rameurs. Tes sages, ô Tyr, qui étaient en toi, étaient tes pilotes.
Watu kutoka Sidoni na Arvadi walikuwa wapiga makasia yako; watu wako wenye ustadi, ee Tiro, walikuwa ndio mabaharia wako.
9 Les anciens de Guebal et ses sages étaient en toi, réparant tes fissures; tous les navires de la mer et leurs marins étaient chez toi, pour faire trafic avec toi.
Wazee wa Gebali pamoja na mafundi stadi walikuwa mafundi wako melini. Meli zote za baharini na mabaharia wao walikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako.
10 La Perse, et Lud, et Puth, étaient dans ton armée tes hommes de guerre; ils suspendaient chez toi le bouclier et le casque, ils faisaient ta splendeur.
“‘Watu wa Uajemi, Ludi na Putu walikuwa askari katika jeshi lako. Walitundika ngao zao na chapeo zao kwenye kuta zako, wakileta fahari yako.
11 Les fils d’Arvad et ton armée étaient tout autour sur tes murailles, et [tes] guerriers étaient dans tes tours; ils suspendaient leurs boucliers à tes murailles tout autour, ils rendaient parfaite ta beauté. –
Watu wa Arvadi na wa Heleki walikuwa juu ya kuta zako pande zote; watu wa Gamadi walikuwa kwenye minara yako. Walitundika ngao zao kuzizunguka kuta zako; wakaukamilisha uzuri wako.
12 Tarsis commerçait avec toi pour l’abondance de tous biens; d’argent, de fer, d’étain, et de plomb, ils fournissaient tes marchés.
“‘Tarshishi walifanya biashara nawe kwa sababu ya utajiri wako mkubwa wa bidhaa, walibadilisha fedha, chuma, bati na risasi kwa mali zako.
13 Javan, Tubal et Méshec étaient tes marchands; ils fournissaient à ton trafic des âmes d’hommes et des ustensiles d’airain.
“‘Uyunani, Tubali na Mesheki, walifanya biashara nawe, walibadilisha watumwa na vyombo vya shaba kwa bidhaa zako.
14 De la maison de Togarma ils fournissaient tes marchés en chevaux, et en cavaliers, et en mulets.
“‘Watu wa Beth-Togarma walibadilisha farasi wa mizigo, farasi wa vita na nyumbu kwa mali zako.
15 Les fils de Dedan étaient tes marchands; de nombreuses îles étaient en relation de commerce avec toi; elles te donnaient en retour des dents d’ivoire et de l’ébène.
“‘Watu wa Dedani walifanya biashara nawe, watu wengi wa nchi za pwani walikuwa wachuuzi wako, walikulipa kwa pembe za ndovu na mpingo.
16 La Syrie commerçait avec toi à cause de la multitude de tes ouvrages; ils fournissaient tes marchés d’escarboucles, de pourpre, de broderie, et de fin lin, et de corail, et de rubis.
“‘Watu wa Aramu walifanya biashara nawe kwa ajili ya wingi wa kazi za mikono yako, wakibadilishana kwa almasi, vitambaa vya rangi ya zambarau, vitambaa vilivyotariziwa, kitani safi, matumbawe na akiki nyekundu.
17 Juda et le pays d’Israël étaient tes marchands; ils fournissaient à ton trafic du froment de Minnith, et de la pâtisserie, et du miel, et de l’huile, et du baume.
“‘Yuda na Israeli walifanya biashara nawe, walibadilishana kwa ngano kutoka Minithi, mtama, asali, mafuta na zeri ya kuponyeshea.
18 Pour la multitude de tes ouvrages, à cause de l’abondance de tous biens, Damas commerçait avec toi en vin de Helbon et en laine blanche.
“‘Dameski, kwa sababu ya wingi wa kazi za mikono yako na ukuu wa utajiri wa mali, walifanya biashara nawe wakibadilishana mvinyo kutoka Helboni na sufu kutoka Zahari.
19 Vedan, et Javan d’Uzal, fournissaient tes marchés de fer ouvragé; la casse et le roseau aromatique étaient dans ton trafic.
“‘Wadani na Wayunani kutoka Uzali, walikuletea mali za biashara, nao wakabadilishana nawe chuma kilichofuliwa, mdalasini na mchaichai.
20 Dedan était ton marchand en draps précieux pour housses de cheval.
“‘Dedani alifanya biashara nawe kwa matandiko ya farasi.
21 L’Arabie et tous les princes de Kédar étaient en relation de commerce avec toi; en agneaux, en béliers et en boucs, en ces choses-là, ils étaient tes commerçants.
“‘Arabuni na wakuu wote wa Kedari walikuwa wanunuzi wako waliobadilishana bidhaa zako na wana-kondoo, kondoo dume na mbuzi.
22 Les marchands de Sheba et de Rahma étaient tes marchands; ils fournissaient tes marchés de tout aromate excellent, et de toute pierre précieuse, et d’or.
“‘Wafanyabiashara wa Sheba na wa Raama walifanya biashara nawe, wakabadilishana bidhaa zako na aina zote za vikolezi, vito vya thamani na dhahabu.
23 Charan, et Canné, et Éden, les marchands de Sheba, Assur, Kilmad, ta marchande,
“‘Harani, Kane na Edeni na wafanyabiashara wa Sheba, Ashuru na Kilmadi walifanya biashara nawe.
24 ceux-là trafiquaient avec toi en objets de prix, en draps bleus, et en broderies, et en caisses de riches étoffes, liées de cordes et [faites] de cèdre, entre tes marchandises.
Kwenye soko lako, walifanya biashara nawe kwa mavazi mazuri, vitambaa vya buluu, nguo za kutariziwa na mazulia ya rangi mbalimbali yenye kamba zilizosokotwa na kuwekwa mafundo imara.
25 Les navires de Tarsis étaient tes caravanes, pour ton trafic; et tu as été remplie et tu es devenue extrêmement glorieuse au cœur des mers.
“‘Merikebu za Tarshishi ndizo zinazokusafirishia bidhaa zako. Umejazwa shehena kubwa katika moyo wa bahari.
26 Tes rameurs t’ont amenée dans de grandes eaux; le vent d’orient t’a brisée au cœur des mers.
Wapiga makasia wako wanakupeleka mpaka kwenye maji makavu. Lakini upepo wa mashariki umekuvunja vipande vipande katika moyo wa bahari.
27 Tes richesses et tes échanges, ton trafic, tes marins et tes pilotes, ceux qui réparent tes fissures, et ceux qui font trafic avec toi, et tous tes hommes de guerre qui sont en toi, et toute ta multitude qui est au milieu de toi, tomberont au cœur des mers, au jour de ta chute.
Utajiri wako, bidhaa zako na mali zako, mabaharia wako, manahodha wako, mafundi wako wa meli, wafanyabiashara wako na askari wako wote, na kila mmoja aliyeko melini atazama kwenye moyo wa bahari siku ile ya kuvunjika kwa meli yako.
28 Les lieux ouverts trembleront au bruit du cri de tes pilotes.
Nchi za pwani zitatetemeka wakati mabaharia wako watakapopiga kelele.
29 Et tous ceux qui manient la rame, les marins, tous les pilotes de la mer, descendront de leurs navires; ils se tiendront sur la terre,
Wote wapigao makasia wataacha meli zao, mabaharia wote na wanamaji wote watasimama pwani.
30 et feront entendre leur voix sur toi, et crieront amèrement; et ils jetteront de la poussière sur leurs têtes, ils se rouleront dans la cendre;
Watapaza sauti zao na kulia sana kwa ajili yako; watajitupia mavumbi juu ya vichwa vyao na kujivingirisha kwenye majivu.
31 et ils se rendront chauves à cause de toi, et se ceindront de sacs, et pleureront sur toi avec amertume d’âme, avec un deuil amer.
Watanyoa nywele zao kwa ajili yako, nao watavaa nguo za magunia. Watakulilia kwa uchungu wa moyo na kwa maombolezo makuu.
32 Et dans leur gémissement ils élèveront sur toi une complainte, ils se lamenteront sur toi: Qui fut comme Tyr, comme celle qui est détruite au milieu de la mer?
Watakapokuwa wanalia na kuomboleza juu yako, watafanya maombolezo kukuhusu wakisema: “Ni nani aliyepata kuangamizwa kama Tiro, katika moyo wa bahari?”
33 Par les débouchés de tes marchés au-delà des mers tu as rassasié beaucoup de peuples; par l’abondance de tes richesses et de ton trafic tu as enrichi les rois de la terre.
Wakati bidhaa zako zilipotoka baharini, ulitosheleza mataifa mengi; kwa wingi wa utajiri wako na bidhaa zako ulitajirisha wafalme wa dunia.
34 Au temps où tu as été brisée par les mers dans les profondeurs des eaux, ton trafic et toute ta multitude au milieu de toi sont tombés.
Sasa umevunjavunjwa na bahari, katika vilindi vya maji, bidhaa zako na kundi lako lote vimezama pamoja nawe.
35 Tous les habitants des îles sont dans la stupeur à cause de toi, et leurs rois frémiront d’horreur, leurs visages sont agités.
Wote waishio katika nchi za pwani wanakustaajabia; wafalme wao wanatetemeka kwa hofu kuu, nazo nyuso zao zimekunjamana kwa woga.
36 Les marchands parmi les peuples ont sifflé sur toi; tu es devenue une terreur, et tu ne seras plus, à jamais.
Wafanyabiashara miongoni mwa mataifa wanakucheka; umefikia mwisho wa kutisha nawe hutakuwepo tena.’”