< Esdras 8 >

1 Voici les chefs de famille de leurs pères, et voici la généalogie de ceux qui sont montés avec moi de Babylone, sous le règne du roi Artaxerxès:
Hawa ni viongozi wa watangulizi familia ambazo zilitoka babeli pamoja nami kipindi cha utawala wa mfalme Artashasta.
2 Des fils de Phinées: Guershom. Des fils d'Ithamar, Daniel. Des fils de David, Hattush.
Mwana wa Finehasi, Gershoni. Mwana wa Ithamari, Daniel. Mwana wa Daudi, Hatushi ambaye ni mwana Shekania,
3 Des fils de Shecania, des fils de Parosh, Zacharie; et avec lui, cent cinquante mâles, classés par généalogie.
ambaye pia ni mwana wa Paroshi na Zekaria na pamoja na yeye kulikuwa na wanaume mia moja na hamsini walitajwa kwenye idadi ya ukoo wake.
4 Des fils de Pahathmoab, Eliehœnaï, fils de Zerahia, et avec lui deux cents mâles.
Wana wa Pahath- Moabu, Eliehoenai mwana wa Zerahia na pamoja naye wanaume mia mbili. Wana wa
5 Des fils de Shecania, fils de Jahaziel, et avec lui trois cents mâles.
Shekaniah, Yahazieli na pamoja naye wanaume mia tatu. Wana wa
6 Parmi les fils d'Adin, Ebed, fils de Jonathan, et avec lui cinquante mâles.
adini, Ebedi mwana wa Yonathani na pamoja naye waliorodheshwa wanaume hamsini.
7 Des fils d'Élam, Jéschaia, fils d'Athalie, et avec lui soixante-dix mâles.
Wana wa Elamu, Yeshaya mwana wa Athalia na pamoja naye waliorodheshwa wanaume sabini.
8 Parmi les fils de Schephatia, Zebadia, fils de Micaël, et avec lui quatre-vingts mâles.
Wana wa Shefatia, Zebadia, mwana wa Mikaeli na pamoja naye waliorodheshwa wanaume themanini.
9 Parmi les fils de Joab, Abdias, fils de Jehiel, et avec lui deux cent dix-huit mâles.
Wana wa Yoabu, Obadia mwana wa Yehieli pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume mia mbili kumi na wanane. Wana wa Binui,
10 Des fils de Schelomith, fils de Josiphia, et avec lui cent soixante mâles.
Sheromithi, mwana wa Yosifia na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume mia moja na sitini.
11 Parmi les fils de Bebaï, Zacharie, fils de Bebaï, et avec lui vingt-huit mâles.
Wana wa Bebai, zekaria mwana wa Bebai na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume ishirini na wanane.
12 Des fils d'Azgad, Jochanan, fils de Hakkatan, et avec lui cent dix mâles.
Wana wa Azgadi, Yohana mwana wa Hakatani na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume mia moja na kumi.
13 Parmi les fils d'Adonikam, qui furent les derniers, leurs noms sont: Eliphelet, Jeuel, et Shemaiah; et avec eux soixante mâles.
Wale wana wa Adonikamu wakaja baadaye. Na haya ndio majina yao: Elifereti, Yeueli na Shemaya na pamoja na wao wakaja wanaume sitini.
14 Des fils de Bigvaï, Uthaï et Zabbud, et avec eux soixante-dix mâles.
Wana wa Bigwai, Uthai, mwana wa zabudi na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume sabini
15 Je les rassemblai jusqu'au fleuve qui coule vers Ahava, et nous y campâmes trois jours. Je regardai autour de moi le peuple et les prêtres, et je trouvai qu'il n'y avait aucun des fils de Lévi.
Nikawakusanya wasafiri bandari iliyokuwa inaelekea Ahava. Tukaweka kambi muda wa siku tatu, nikawachunguza watu na makuhani, lakini sikuwaona wana wa Levi miongoni.
16 J'envoyai chercher Éliézer, Ariel, Shemahia, Elnathan, Jarib, Elnathan, Nathan, Zacharie et Meshullam, chefs de famille, ainsi que Jojarib et Elnathan, qui étaient maîtres.
Hivyo nikatuma kwa Eliezeri, arieli, Shemaya, Elnathani, Yaribu na Elnathani na Nathani, Zekaria na Meshulamu waliokuwa viongozi na kwa Yoyaribu na Elnathani ambao walikuwa ni walimu.
17 Je les envoyai vers Iddo, le chef du lieu de Casiphia, et je leur dis ce qu'ils devaient dire à Iddo et à ses frères, les serviteurs du temple du lieu de Casiphia, afin qu'ils nous amènent des ministres pour la maison de notre Dieu.
Tena nikawatuma kwa Ido, kiongozi wa Kasifia. Nikawaaambia kile watachomweleza Ido. na jamaa zake, watumishi wa Hekalu waliishi Kasifia, kwa hiyo, kutuma kwetu watumishi kwa ajili ya nyumba ya Mungu.
18 Selon la bonne main de notre Dieu sur nous, ils nous amenèrent un homme de confiance, d'entre les fils de Mahli, fils de Lévi, fils d'Israël, à savoir Sherebia, avec ses fils et ses frères, dix-huit;
Hivyo wakatutuma sisi kwa Mungu na mkono mzuri wa mtu aliyeitwa Ishekeli. Alikuwa mwana wa mali Mwana wa Levi mwana wa Israel. Akaja na wana kumi na wanane na ndugu,
19 Haschabia, et avec lui Jeshaiah, des fils de Merari, ses frères et leurs fils, vingt;
pamoja naye Hashabia, pamoja na Yeshaya wa wana wa Merari na ndugu zake na wana wake jumla watu ishirini wote. Miongoni
20 et d'entre les serviteurs du temple, que David et les princes avaient donnés pour le service des Lévites, deux cent vingt serviteurs du temple. Tous furent mentionnés par leur nom.
mwao walichaguliwa kutumika katika Hekalu, ambapo Daudi na wakuu waliwapa kuwahudumia walawi: mia mbili ishirini kila mmoja wao aliagizwa kwa majina.
21 Et j'ai proclamé un jeûne au bord de la rivière Ahava, pour que nous nous humiliions devant notre Dieu et que nous lui demandions un chemin droit pour nous, pour nos enfants et pour tous nos biens.
Tena nikatangaza kufunga mto Ahava ili kujinyenyekeza mbele za Mungu, kutafuta njia iliyoonyoka kutoka kwake kwa ajili yetu, watoto wetu na mali zetu,
22 Car j'avais honte de demander au roi une troupe de soldats et de cavaliers pour nous aider contre l'ennemi en chemin, parce que nous avions dit au roi: « La main de notre Dieu est sur tous ceux qui le cherchent, pour le bien; mais sa puissance et sa colère sont contre tous ceux qui l'abandonnent. »
Niliona aibu kumwomba mfalme kwa ajili ya jeshi au mpandafarasi kwa ajili ya kutulinda tunapokuwa njiani, tangu tumemwambia mfalme “mkono wa Mungu uko pamoja na wote wanaomtafuta kwa mazuri. lakini uweza wake na ghazabu yake ni juu ya wale wote wanaomwasi yeye.
23 Nous avons donc jeûné et supplié notre Dieu pour cela, et il a exaucé notre demande.
Hivyo tulifunga na kumsihi Mungu kwa jambo hilo.
24 Je mis à part douze des chefs des sacrificateurs, Schérébia, Haschabia, et dix de leurs frères avec eux.
Tena nikachagua watu kumi na wawili kutoka kwa kuhani: Sherebia na Hashabia na ndugu zao wengine kumi.
25 Je leur pesai l'argent, l'or et les ustensiles, l'offrande pour la maison de notre Dieu, que le roi, ses conseillers, ses chefs, et tout Israël présent, avaient présentée.
Nikapima kwa ajili yao fedha, dhahabu na vyombo na sadaka kwa ajili ya nyumba ya Mungu kwa wafalme, washauri, na wakuu na Israel wote walitoa kwa hiari.
26 J'ai pesé entre leurs mains six cent cinquante talents d'argent, cent talents de vases d'argent, cent talents d'or,
Hivyo nikawapimia kwenye mikono yao talanta za fedha mia sita na hamsini, talanta mia moja ya vyombo vya fedha, talanta mia moja za dhahabu.
27 vingt coupes d'or pesant mille dariques, et deux vases de bronze fin et brillant, précieux comme l'or.
vifaa ishirini vya dhahabu kwa pamoja vilikuwa na thamani ya elfu moja darkoni na vitu viwili vya sanamu vivyonakshiwa kama dhahabu ya kupendeza.
28 Je leur dis: « Vous êtes saints pour Yahvé, et les vases sont saints. L'argent et l'or sont une offrande volontaire à Yahvé, le Dieu de vos pères.
Kisha nikawaambia, mmewekwa wakfu kwa Bwana, na hivi vyombo pia na fedha na dhahabu, vimetolewa kwa hiari kwa Yahwe, Mungu wa watangulizi wenu.
29 Veillez et gardez-les jusqu'à ce que vous les pesiez devant les chefs des prêtres, les lévites et les chefs de famille d'Israël, à Jérusalem, dans les salles de la maison de Yahvé. »
mviangalie na kuvitunza hadi mtakapovipima mbele ya makuhani, walawi, na viongozi wa wataangulizi wa jamii ya Israel katika Yerusalem katika nyumba ya Mungu.
30 Les prêtres et les lévites reçurent donc le poids de l'argent, de l'or et des objets, pour les apporter à Jérusalem, dans la maison de notre Dieu.
Makuhani na walawi walikubali vipimo vya fedha na dhahabu na vyombo kwa ajili ya kuvichukua na kuvipeleka Yerusalem, kwenye nyumba ya Mungu wetu.
31 Et nous partîmes du fleuve Ahava, le douzième jour du premier mois, pour aller à Jérusalem. La main de notre Dieu était sur nous, et il nous délivra de la main de l'ennemi et des brigands en chemin.
Tukatoka kwenda mto Ahava siku ya kumi na mbili katika mwezi wa kwanza kwenda Yerusalem, Mkono wa Mungu ulikuwa pamoja nasi, ulitulinda na mikono ya adui na wale waliotaka kutufanyia fujo njiani.
32 Nous arrivâmes à Jérusalem, où nous restâmes trois jours.
Hivyo tukaingia Yerusalem na kukaa humo kwa siku tatu.
33 Le quatrième jour, l'argent, l'or et les ustensiles furent pesés dans la maison de notre Dieu, entre les mains de Merémoth, fils du prêtre Urie, d'Eléazar, fils de Phinées, de Jozabad, fils de Josué, et de Noadia, fils de Binnui, les Lévites.
Tena siku ya nne fedha na dhahabu na vyombo vilipimwa ndani ya nyumba ya Mungu wetu kwa mikono ya Meremothi mwana wa Uria kuhani, na pamoja nao alikuwepo Eleazari mwana wa Finehasi, Yozabadi mwana wa Yeshua, na Noadia mwana wa Binui, Walawi.
34 Tout fut compté et pesé, et tout le poids fut écrit en ce temps-là.
Idadi na uzito wa kila kitu uliweza kujulikana. Uzito wote uliweza kuandikwa katika kipindi hicho
35 Les enfants de la captivité, qui étaient sortis de l'exil, offrirent des holocaustes au Dieu d'Israël: douze taureaux pour tout Israël, quatre-vingt-seize béliers, soixante-dix-sept agneaux et douze boucs pour le sacrifice pour le péché. Tout cela constituait un holocauste à Yahvé.
Na wale waliokuja kutoka matekani, watu wa uhamisho, wakatoa sadaka ya kutekezwa kwa Mungu wa Israel, kondoo tisini na sita, wana-kondoo sabini na saba na mbuzi wa kiume kumi na wawili kama sadaka ya dhambi. Zote zilikuwa sadaka za kutekezwa kwa ajili ya Yahwe.
36 Ils remettaient les ordres du roi aux gouverneurs locaux et aux gouverneurs de l'autre côté du fleuve. Ils soutenaient ainsi le peuple et la maison de Dieu.
Tena wakawapa amri za mfalme kwa wakuu wa wafalme na wakuu katika mji ngambo ya mto, na wakawasaidia watu na nyumba ya Mungu.

< Esdras 8 >