< 2 Chronicles 11 >

1 And Rehoboam cometh in to Jerusalem, and assembleth the house of Judah and Benjamin, a hundred and eighty thousand chosen warriors, to fight with Israel, to bring back the kingdom to Rehoboam.
Rehoroboamu alipofiki Yerusalemu, akawakusanya nyumba ya Yuda na Benyamini, wanaume 180, 000 walaiaochaguliwa amabao wliakuwa wanajeshi, kwa ajili ya kupigana dhiidi ya Israeli, ili kuurudisha ufalme kwa Rehoboamu.
2 And a word of Jehovah is unto Shemaiah, a man of God, saying,
Lakini neno la Yahwe likamjia Shemaya mtu wa Mungu, likisema,
3 'Speak unto Rehoboam son of Solomon king of Judah, and unto all Israel in Judah and Benjamin, saying,
“Sema kwa Rehoboamu mwana wa Selemani, mfalme wa Yuda, na kwa Israeli kataika Yuda na Benyamaini,
4 Thus said Jehovah, Ye do not go up nor fight with your brethren, turn back each to his house, for from Me hath this thing been;' and they hear the words of Jehovah, and turn back from going against Jeroboam.
Yahwe anasema hivi, “Msivamie wala kufanya vita dhidi ya ndugu zako. Kila mmoja lazima arudi kwenye nyumba yake, kwa maana nimesababisha jambo hili kutokea.” Kwa hiyo wakayatii maneno ya Yahwe na kuacha kumvamia Yeroboamu.
5 And Rehoboam dwelleth in Jerusalem, and buildeth cities for a bulwark in Judah,
Yeroboamu akaishi katika Yerusalemu na kujenga miji katika Yuda kwa ajili ya kujilinda.
6 yea, he buildeth Beth-Lehem and Etam, and Tekoa,
Akaijenga Bethelehemu, EtamuTekoa,
7 and Beth-Zur, and Shocho, and Adullam,
Bethsusi, Soko, Adulamu,
8 and Gath, and Mareshah, and Ziph,
Gathi, Maresha, Zifu,
9 and Adoraim, and Lachish, and Azekah,
Adoraimu, Lakishi, Azeka,
10 and Zorah, and Aijalon, and Hebron, that [are] in Judah and in Benjamin, cities of bulwarks.
Sora, Aiyaloni, na Hebroni. Hii ni miji yenye ngome katika Yuda na Benyamini.
11 And he strengtheneth the bulwarks, and putteth in them leaders, and treasures of food, and oil, and wine,
Akaziimarisha ngome na kuweka maamri jeshsi ndani yake, pamaoja na hazina ya chakula, mafuta, na divai.
12 and in every city and city targets and spears, and strengtheneth them very greatly; and he hath Judah and Benjamin.
Akaweka ngao na mikuki katika miji yote na kuifanya imara sana. Kwa hiyo Yuda na Benyamini zikawa zake.
13 And the priests, and the Levites, that [are] in all Israel, have stationed themselves by him, out of all their border,
Makuhani na Walawi waliokuwa katika Israeli yote wakaenda kwake kutoka ndani ya mipaka yao.
14 for the Levites have left their suburbs and their possession, and they come to Judah and to Jerusalem, for Jeroboam and his sons have cast them off from acting as priests to Jehovah,
Kwa kuwa Walawi waliacha nchi za malisho yao na mali zao ili kuja Yuda na Yerusalemu, kwa maana
15 and he establisheth to him priests for high places, and for goats, and for calves, that he made —
Yeroboamu na wanaaye walikuwa wamewafukuza, ili kwamba wasifanye majukumu yao ya kikuhani kwa ajili ya sehemu za juu na mbuzi na sanamu za ndama alizokuwa ametengeneza.
16 and after them, out of all the tribes of Israel, those giving their heart to seek Jehovah, God of Israel, have come in to Jerusalem to sacrifice to Jehovah, God of their father.
Watu kutoka kabila zote za Israeli wakaja nyuma yao, wale walio wameiilekeza mioyo yao kumtafuta Yahwe, Mungu wa Israeli; wakaja Yerusalemu kwa ajili ya kumtolea dhabihu Yahwe. Mungu wa baba zao.
17 And they strengthen the kingdom of Judah, and strengthen Rehoboam son of Solomon, for three years, because they walked in the way of David and Solomon for three years.
Kwa hiyo wakauimarisha ufalame wa Yuda na kumfanya imara Rehoboamu mwana wa Selemani kwa miaka mitatu, na wakatembea kwa miaka mitatu katika njia ya Daudi na Selemani.
18 And Rehoboam taketh to him a wife, Mahalath, child of Jerimoth son of David, [and] Abigail daughter of Eliab, son of Jesse.
Rehoboamu akajitwalia mke: Mahalathi, binti wa Yerimothi, mwana wa Daudi na wa Abihaili, binti wa Eliabu, mwana wa Yese.
19 And she beareth to him sons, Jeush, and Shamaria, and Zaham.
Akamzalia wana: Yeushi, Shemaraia, na Zahamu.
20 And after her he hath taken Maachah daughter of Absalom, and she beareth to him Abijah, and Attai, and Ziza, and Shelomith.
Baaad ya Mahalathi, Rehoboamu akamchukua Maaka, binti Absalomu; akamzalia Abiya, Atai, Ziza, na Shelomithi.
21 And Rehoboam loveth Maachah daughter of Absalom above all his wives and his concubines — for eighteen wives he hath taken, and sixty concubines — and he begetteth twenty and eight sons, and sixty daughters.
Rehoboamu akampenda Maaka, binti Solomoni, zaidi kuliko wake za wengine wote na masuria (alichukua wake kumi na nane na masuria sitini, na akawa baba wa wana ishirini na nane na mabinti sitini).
22 And Rehoboam appointeth for head Abijah son of Maachah, for leader among his brethren, for to cause him to reign.
Rehoboamu akamteua Abiya mwana wa Maaka kuwa mkuu, kiongozi miongoni mwa ndugu zake alikuwa na wazo la kumfanya mfalme.
23 And he hath understanding, and spreadeth out of all his sons to all lands of Judah and Benjamin, to all cities of the bulwarks, and giveth to them provision in abundance; and he asketh a multitude of wives.
Rehoboamu akatawala kwa hekima; akawatawanya wanaye katika nchi yote ya Yuda na Benyamini katika kila mji imara. Pia akawapa chakula kwa wingi na akatafuta wake wengi kwa ajili yao.

< 2 Chronicles 11 >