< Mark 1 >

1 The bigynnyng of the gospel of Jhesu Crist, the sone of God.
Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.
2 As it is writun in Ysaie, the prophete, Lo! Y sende myn aungel bifor thi face, that schal make thi weie redi bifor thee.
Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie; yeye atakutayarishia njia yako.
3 The vois of a crier in desert, Make ye redi the weie of the Lord, make ye hise paththis riyt.
Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni mapito yake.”
4 Joon was in desert baptisynge, and prechynge the baptym of penaunce, in to remissioun of synnes.
Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba ni lazima watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao.
5 And al the cuntre of Judee wente out to hym, and alle men of Jerusalem; and thei weren baptisid of hym in the flom Jordan, `and knoulechiden her synnes.
Watu kutoka sehemu zote za Yudea na wenyeji wote wa Yerusalemu walimwendea, wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.
6 And Joon was clothid with heeris of camels, and a girdil of skyn was about hise leendis; and he ete hony soukis, and wilde hony, and prechide,
Yohane alikuwa amevaa vazi lililofumwa kwa manyoya ya ngamia, na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
7 and seide, A stronger than Y schal come aftir me, and Y am not worthi to knele doun, and vnlace his schoone.
Naye alihubiri akisema, “Baada yangu anakuja mwenye uwezo zaidi kuliko mimi, ambaye mimi sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake.
8 Y haue baptisid you in watir; but he schal baptise you in the Hooli Goost.
Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”
9 And it was don in tho daies, Jhesus cam fro Nazareth of Galilee, and was baptisid of Joon in Jordan.
Siku hizo, Yesu alifika kutoka Nazareti, mji wa Galilaya, akabatizwa na Yohane katika mto Yordani.
10 And anoon he wente up of the watir, and saye heuenes opened, and the Hooli Goost comynge doun as a culuer, and dwellynge in hym.
Mara tu alipotoka majini, aliona mbingu zimefunguliwa, na Roho akishuka juu yake kama njiwa.
11 And a vois was maad fro heuenes, Thou art my loued sone, in thee Y am plesid.
Sauti ikasikika kutoka mbinguni: “Wewe ni Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe.”
12 And anoon the Spirit puttide hym forth in to deseert.
Mara akaongozwa na Roho kwenda jangwani,
13 And he was in deseert fourti daies and fourti nyytis, and was temptid of Sathanas, and he was with beestis, and aungels mynystriden to hym.
akakaa huko siku arubaini akijaribiwa na Shetani. Alikuwa huko pamoja na wanyama wa porini, nao malaika wakawa wanamtumikia.
14 But aftir that Joon was takun, Jhesus cam in to Galilee, and prechide the gospel of the kyngdoom of God,
Yohane alipokwisha fungwa gerezani, Yesu alikwenda Galilaya, akahubiri Habari Njema ya Mungu, akisema,
15 and seide, That the tyme is fulfillid, and the kyngdoom of God schal come nyy; do ye penaunce, and bileue ye to the gospel.
“Wakati umetimia, na Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema!”
16 And as he passide bisidis the see of Galilee, he say Symount, and Andrew, his brother, castynge her nettis in to the see; for thei weren fisscheris.
Alipokuwa anapita kando ya ziwa Galilaya, aliwaona wavuvi wawili: Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa wavu.
17 And Jhesus seide to hem, Come ye aftir me; Y schal make you to be maad fisscheris of men.
Yesu akawaambia, “Nifuateni nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu.”
18 And anoon thei leften the nettis, and sueden hym.
Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
19 And he yede forth fro thennus a litil, and siy James of Zebedee, and Joon, his brother, in a boot makynge nettis.
Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Nao pia walikuwa ndani ya mashua yao wakizitengeneza nyavu zao.
20 And anoon he clepide hem; and thei leften Zebedee, her fadir, in the boot with hiryd seruauntis, and thei suweden hym.
Yesu akawaita mara, nao wakamwacha baba yao Zebedayo katika mashua pamoja na wafanyakazi, wakamfuata.
21 And thei entriden in to Capharnaum, and anoon in the sabatys he yede in to a synagoge, and tauyte hem.
Wakafika mjini Kafarnaumu, na mara ilipofika Sabato, Yesu akaingia katika Sunagogi, akaanza kufundisha.
22 And thei wondriden on his teching; for he tauyte hem, as he that hadde power, and not as scribis.
Watu wote waliomsikia walishangazwa na mafundisho yake, maana hakuwa anafundisha kama walimu wao wa Sheria, bali kama mtu mwenye mamlaka.
23 And in the synagoge of hem was a man in an vnclene spirit, and he criede out,
Mara akatokea mle ndani ya sunagogi mtu mmoja mwenye pepo mchafu,
24 and seide, What to vs and to thee, thou Jhesu of Nazareth? hast thou come to distrie vs? Y woot that thou art the hooli of God.
akapaaza sauti, “Una nini nasi, wewe Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!”
25 And Jhesus thretenede hym, and seide, Wex doumbe, and go out of the man.
Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.”
26 And the vnclene spirit debreidynge hym, and criynge with greet vois, wente out fro hym.
Basi, huyo pepo mchafu akamtikisatikisa mtu huyo, kisha akalia kwa sauti kubwa, akamtoka.
27 And alle men wondriden, so that thei souyten with ynne hem silf, and seiden, What thing is this? what newe doctrine is this? for in power he comaundith to vnclene spiritis, and thei obeyen to hym.
Watu wote wakashangaa, wakaulizana, “Ni mambo gani haya? Je, ni mafundisho mapya? Mtu huyu anayo mamlaka ya kuamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!”
28 And the fame of hym wente forth anoon in to al the cuntree of Galilee.
Habari za Yesu zikaenea upesi kila mahali katika wilaya ya Galilaya.
29 And anoon thei yeden out of the synagoge, and camen into the hous of Symount and of Andrewe, with James and Joon.
Wakatoka katika sunagogi, wakaenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea; Yakobo na Yohane walikwenda pamoja nao.
30 And the modir of Symountis wijf lay sijk in fyueris; and anoon thei seien to hym of hyr.
Basi, mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa kitandani ana homa kali. Wakamwarifu Yesu mara alipowasili.
31 And he cam nyy, and areride hir, and whanne he hadde take hir hoond, anoon the feuer lefte hir, and sche seruede hem.
Yesu akamwendea huyo mama, akamshika mkono, akamwinua. Na ile homa ikamwacha, akaanza kuwatumikia.
32 But whanne the euentid was come, and the sonne was gon doun, thei brouyten to hym alle that weren of male ese, and hem that hadden fendis.
Jioni, jua lilipokwisha tua, wakamletea Yesu wagonjwa wote na watu waliopagawa na pepo.
33 And al the citee was gaderid at the yate.
Watu wote wa mji ule wakakusanyika nje ya mlango.
34 And he heelide many, that hadden dyuerse sijknessis, and he castide out many feendis, and he suffride hem not to speke, for thei knewen hym.
Naye Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa mbalimbali; aliwafukuza pepo wengi, lakini hakuwaruhusu kusema kitu maana walikuwa wanamjua yeye ni nani.
35 And he roos ful eerli, and yede out, and wente in to a desert place, and preiede there.
Kesho yake, kabla ya mapambazuko, Yesu alitoka, akaenda mahali pa faragha kusali.
36 And Symount suede hym, and thei that weren with hym.
Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta.
37 And whanne thei hadden founde hym, thei seiden to hym, That alle men seken thee.
Walipomwona wakamwambia, “Kila mtu anakutafuta.”
38 And he seide to hem, Go we in to the next townes and citees, that Y preche also there, for her to Y cam.
Yesu akawaambia, “Twendeni katika miji mingine ya jirani nikahubiri huko pia, maana nimekuja kwa sababu hiyo.”
39 And he prechide in the synagogis of hem, and in al Galilee, and castide out feendis.
Basi, akaenda kila mahali Galilaya akihubiri katika masunagogi na kufukuza pepo.
40 And a leprouse man cam to hym, and bisouyte, `and knelide, and seide, If thou wolt, thou maist clense me.
Mtu mmoja mwenye ukoma alimwendea Yesu, akapiga magoti, akamwomba, “Ukitaka, waweza kunitakasa!”
41 And Jhesus hadde mercy on hym, and streiyte out his hoond, and towchyde hym, and seide to hym, I wole, be thou maad cleene.
Yesu akamwonea huruma, akanyosha mkono wake, akamgusa na kumwambia, “Nataka, takasika!”
42 And whanne he hadde seide this, anoon the lepre partyde awey fro hym, and he was clensyd.
Mara ukoma ukamwacha mtu huyo, akatakasika.
43 And Jhesus thretenede hym, and anoon Jhesus putte hym out,
Kisha Yesu akamwambia aende zake upesi na kumwonya vikali,
44 and seyde to hym, Se thou, seye to no man; but go, schewe thee to the pryncys of prestys, and offre for thi clensynge in to wytnessyng to hem, tho thingis that Moyses bad.
“Usimwambie mtu yeyote jambo hili, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani; kisha utoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama alivyoamuru Mose, iwe uthibitisho kwao kwamba umepona.”
45 And he yede out, and bigan to preche, and publische the word, so that now he myyte not go opynli in to the citee, but be withoutforth in desert placis; and thei camen to hym on alle sidis.
Lakini huyo mtu akaenda, akaanza kueneza habari hiyo kila mahali na kusema mambo mengi hata Yesu hakuweza tena kuingia katika mji wowote waziwazi; ikamlazimu kukaa nje, mahali pa faragha. Hata hivyo, watu wakamwendea kutoka kila upande.

< Mark 1 >