< 2 Corinthians 9 >

1 Now concerning the relief intended for the saints, it is superfluous for me to write to you:
Si lazima kuandika zaidi kuhusu huduma hiyo yenu kwa ajili ya watu wa Mungu.
2 for I know your readiness of mind, which I boast of concerning you to the Macedonians, that Achaia was ready a year ago; and your zeal hath excited many.
Ninajua jinsi mlivyo na moyo wa kusaidia, na nilijivuna juu yenu kuhusu jambo hilo mbele ya watu wa Makedonia. Niliwaambia: “Ndugu zetu wa Akaya wako tayari tangu mwaka jana.” Hivyo, moto wenu umekwisha wahimiza watu wengi zaidi.
3 But I have sent the brethren, that our boasting of you might not become vain in this respect, but that ye might be ready, as I had said:
Basi, nimewatuma ndugu zetu hao, ili fahari yetu juu yenu ionekane kwamba si maneno matupu, na kwamba mko tayari kabisa na msaada wenu kama nilivyosema.
4 least if the Macedonians should come with me, and find you unprepared, we should be ashamed (not to say you also) in this confident boasting.
Isije ikawa kwamba watu wa Makedonia watakapokuja pamoja nami tukawakuta hamko tayari, hapo sisi tutaaibika—bila kutaja aibu mtakayopata ninyi wenyewe—kwa sababu tutakuwa tumewatumainia kupita kiasi.
5 Therefore I thought it necessary to exhort the brethren to go first to you, and before our coming to collect your bounty beforementioned, that it may be ready, as of munificence, and not of force.
Kwa hiyo, nimeona ni lazima kuwaomba hawa ndugu watutangulie kuja kwenu, wapate kuweka tayari zawadi yenu kubwa mliyoahidi; nayo ionyeshe kweli kwamba ni zawadi iliyotolewa kwa hiari na si kwa kulazimishwa.
6 But this I say, He that soweth sparingly shall reap also sparingly; and he that soweth bountifully shall also reap bountifully.
Kumbukeni: “Apandaye kidogo huvuna kidogo; apandaye kwa wingi huvuna kwa wingi.”
7 Let every one give as he chuses in his own heart; not with reluctance, or constraint: for God loveth a chearful giver.
Kila mmoja, basi, na atoe kadiri alivyoamua, kwa moyo na wala si kwa huzuni au kwa kulazimishwa, maana Mungu humpenda yule mwenye kutoa kwa furaha.
8 And God is able to make all grace abound towards you; that having always all sufficiency in every thing, ye may abound in every good work:
Mungu anaweza kuwapeni ninyi zaidi ya yale mnayoyahitaji, mpate daima kuwa na kila kitu mnachohitaji, na hivyo mzidi kusaidia katika kila kazi njema.
9 (as it is written, "He hath dispersed, he hath given to the poor, his righteousness continueth for ever." (aiōn g165)
Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Yeye hutoa kwa ukarimu, huwapa maskini, wema wahudumu milele.” (aiōn g165)
10 And may He, who supplieth seed to the sower, and giveth bread for food, furnish and multiply your sowing, and increase the fruits of your bounty: )
Na Mungu ampaye mkulima mbegu na mkate kwa chakula, atawapa ninyi pia mbegu mnazohitaji, na atazifanya ziote, ziwe na kuwapa mavuno mengi ya ukarimu wenu.
11 being in every thing enriched to all liberality, which produceth through us thanksgiving to God.
Yeye atawatajirisha ninyi daima kwa kila kitu, ili watu wapate kumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi zenu wanazozipokea kwa mikono yetu.
12 For the ministration of this service not only supplieth the wants of the saints, but aboundeth also, through many thanksgivings, to the glory of God.
Maana huduma hii takatifu mnayoifanya si tu kwamba itasaidia mahitaji ya watu wa Mungu, bali pia itasababisha watu wengi wamshukuru Mungu.
13 (While from the experience of this ministration they glorify God for your professed subjection to the gospel of Christ, and the liberality of your communication to them, and to all men.)
Kutokana na uthibitisho unaoonyeshwa kwa huduma hii yetu, watu watamtukuza Mungu kwa sababu ya uaminifu wenu kwa Habari Njema ya Kristo mnayoiungama, na pia kwa sababu ya ukarimu mnaowapa wao na watu wote.
14 And in their prayer for you, who long after you because of the transcendent grace of God towards you.
Kwa hiyo watawaombea ninyi kwa moyo kwa sababu ya neema ya pekee aliyowajalieni Mungu.
15 Thanks be to God for his inexpressible gift!
Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi yake isiyo na kifani!

< 2 Corinthians 9 >