< Esther 10 >
1 King Ahasuerus laid a tribute on the land and on the islands of the sea.
Kisha Mfalme Ahusiero akaweka kodi juu ya nchi na maeneo ya bahari.
2 Aren’t all the acts of his power and of his might, and the full account of the greatness of Mordecai, to which the king advanced him, written in the book of the chronicles of the kings of Media and Persia?
Mafanikio yote na nguvu na ukuu wake, pamoja na wa Modekai ambao mfalme alimwinua, yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu ya wafalme wa Wamedi na Waajemi.
3 For Mordecai the Jew was next to King Ahasuerus, and great among the Jews and accepted by the multitude of his brothers, seeking the good of his people and speaking peace to all his descendants.
Modekai Muyahudi alikuwa wa pili kutoka kwa Mfalme Ahusiero. Alikuwa mkuu na maarufu miongoni mwa ndugu zake Wayahudi, kwa sababu alitetea mahitaji ya watu wake na haki za watu na akatetea amani kwa watu wote.