< Isaiah 32 >
1 Behold, a king shall reign in righteousness, and princes shall rule in justice.
Tazama, mfalme atatawala kwa haki, wakuu wataongoza kwa haki.
2 A man shall be as a hiding place from the wind, and a covert from the storm, as streams of water in a dry place, as the shade of a large rock in a weary land.
Kila mmoja atakuwa kama makazi kutoka kwenye upepo na kimbilio kutoka kwenye dhoruba, kama mifereji kwenye sehemu kavu, kama kivuli kwenye mwamba mkubwa katika nchi iliyochoka.
3 The eyes of those who see will not be dim, and the ears of those who hear will listen.
Halafu macho ya waie wanaoona hayataona giza, na masikio ya wale wanosikia yatasikia vizuri.
4 The heart of the rash will understand knowledge, and the tongue of the stammerers will be ready to speak plainly.
Wenye upele watafikiria kwa makini kwa uelewa wao, na wenye kigugumizi watazungumza dhahiri na kwa urahisi.
5 The fool will no longer be called noble, nor the scoundrel be highly respected.
Mjinga hataitwa tena muheshimiwa, wala muongo hataitwa mkuu.
6 For the fool will speak folly, and his heart will work iniquity, to practise profanity, and to utter error against the LORD, to make empty the soul of the hungry, and to cause the drink of the thirsty to fail.
Maana mjinga anazungumza ujinga, na moyo wake unapanga maovu na matendo ya wasiomcha Mungu, na anaongea mambo mabaya kuhusu Yahwe. Na anawafanya wenye njaa kuwa tupu na wenye kiu kukosa maji
7 The ways of the scoundrel are evil. He devises wicked plans to destroy the humble with lying words, even when the needy speaks right.
Njia ya muongo ni maovu. Anajua kubuni mipango mibaya ya kuwalagai masikini kwa uongo, na hata kama masikini atazungumza ukweli.
8 But the noble devises noble things, and he will continue in noble things.
Lakini watu wa heshima wanapanga mipango ya kuheshimika; na kwa sabaubau ya matendo ya wenye heshima tuatasimama.
9 Rise up, you women who are at ease! Hear my voice! You careless daughters, give ear to my speech!
Nyanyukeni juu, enyi wanawake mlio wepesi, na sikilizeni sauti yangu; enyi mabinti msiowangalifu, nisikilizeni mimi.
10 For days beyond a year you will be troubled, you careless women; for the vintage will fail. The harvest won’t come.
Maana kwa mda mfupi zaidi ya mwaka ujasiri wenu utavunjika, nyie wanawake msiojali, maana mavuno ya zabibu yatakwama, mavuno hayatakuwepo.
11 Tremble, you women who are at ease! Be troubled, you careless ones! Strip yourselves, make yourselves naked, and put sackcloth on your waist.
Tetemekeni, enyi wanawake, mliowadhaifu; taabikeni enyi msikuwa wangalifu; ondoeni nguo zenu nzuri mbaki wazi;
12 Beat your breasts for the pleasant fields, for the fruitful vine.
Vaeni nguo za magunia katika viuno vyenu. Ole watakaojichukulia mashamba mazuri, kwa mzabibu ulio zaa sana.
13 Thorns and briers will come up on my people’s land; yes, on all the houses of joy in the joyous city.
Kwenye aridhi ya watu wangu kutamea miiba na mbigiri, hata juu ya nyumba za furaha na mji ulio na shangwe.
14 For the palace will be forsaken. The populous city will be deserted. The hill and the watchtower will be for dens forever, a delight for wild donkeys, a pasture of flocks,
Maana jumba litaachwa, mji uliosongamana utakuwa faragha; kilima na mnara vitakuwa mapango daima, furaha ya punda, malisho ya mifugo;
15 until the Spirit is poured on us from on high, and the wilderness becomes a fruitful field, and the fruitful field is considered a forest.
mpaka roho itushukie sisi kutoka juu, na jangwa litakuwa shamba linalozaa, na shamba linalozaa litachukuliwa kama msitu.
16 Then justice will dwell in the wilderness; and righteousness will remain in the fruitful field.
Wenye haki wataishi jangwani; na wenye haki wataishi katika shamba linalozaa matunda.
17 The work of righteousness will be peace, and the effect of righteousness, quietness and confidence forever.
Kazi ya mwenye haki itakuwa ni ya amani; na matokeo ya wenye haki, ni utulivu na kujiamini daima.
18 My people will live in a peaceful habitation, in safe dwellings, and in quiet resting places,
Watu wangu wataishi katika makao ya amani, na katika nyumba salama na mahali tulivu pa kupumzikia.
19 though hail flattens the forest, and the city is levelled completely.
Lakini hata kama ni mvua ya mawe na msitu umeharibiwa, na mji umeteketezwa,
20 Blessed are you who sow beside all waters, who send out the feet of the ox and the donkey.
yule ambae anaye panda pembezoni mwa mifereji atabarikiwa, na yule atakaye wapeleka ng'ombe na punda kuchunga.