< Genesis 2 >

1 The heavens, the earth, and all their vast array were finished.
Kisha mbingu na nchi zilimalizika, na viumbe hai vyote vilivyo jaza mbingu na nchi.
2 On the seventh day God finished his work which he had done; and he rested on the seventh day from all his work which he had done.
Siku ya saba Mungu alifikia mwisho wa kazi yake ambayo aliifanya, na kwa hiyo alipumzika siku ya saba kutoka kwenye kazi yake yote.
3 God blessed the seventh day, and made it holy, because he rested in it from all his work of creation which he had done.
Mungu akaibarikia siku ya saba na akaitakasa, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kwenye kazi yake yote ambayo aliifanya katika uumbaji.
4 This is the history of the generations of the heavens and of the earth when they were created, in the day that the LORD God made the earth and the heavens.
Haya yalikuwa ni matukio yahusuyo mbingu na nchi, wakati vilipoumbwa, katika siku ambayo Yahwe Mungu aliumba nchi na mbingu.
5 No plant of the field was yet in the earth, and no herb of the field had yet sprung up; for the LORD God had not caused it to rain on the earth. There was not a man to till the ground,
Hapakuwa na msitu wa shambani uliokuwa katika nchi, na hapakuwa na mmea wa shambani uliokuwa umechipuka, kwa kuwa Yahwe Mungu alikuwa hajasababisha mvua kunyesha juu ya nchi, na hapakuwa na mtu wa kulima ardhi.
6 but a mist went up from the earth, and watered the whole surface of the ground.
Lakini ukungu uliinuka juu kutoka kwenye nchi na kuutia maji uso wote wa ardhi.
7 The LORD God formed man from the dust of the ground, and breathed into his nostrils the breath of life; and man became a living soul.
Yahwe Mungu aliumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, na akampulizia puani pumzi ya uhai, na mtu akawa kiumbe hai.
8 The LORD God planted a garden eastward, in Eden, and there he put the man whom he had formed.
Yahwe Mungu aliotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, na pale akamuweka mtu ambaye alimuumba.
9 Out of the ground the LORD God made every tree to grow that is pleasant to the sight, and good for food, including the tree of life in the middle of the garden and the tree of the knowledge of good and evil.
Kutoka ardhini Yahwe Mungu alifanya kila mti uote ambao unapendeza na ni mzuri kwa chakula. Hii ni pamoja na mti wa uzima ambao ulikuwa katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
10 A river went out of Eden to water the garden; and from there it was parted, and became the source of four rivers.
Mto ukatoka nje ya Edeni kuitia maji bustani. Na kutoka pale ukagawanyika na kuwa mito minne.
11 The name of the first is Pishon: it flows through the whole land of Havilah, where there is gold;
Jina la ule wa kwanza ni Pishoni. Huu ni ule ambao unatiririka kupitia nchi yote ya Havila, ambapo kuna dhahabu.
12 and the gold of that land is good. Bdellium and onyx stone are also there.
Dhahabu ya inchi ile ni nzuri. pia kuna bedola na jiwe shohamu.
13 The name of the second river is Gihon. It is the same river that flows through the whole land of Cush.
Jina la mto wa pili ni Gihoni. Huu unatiririka kupitia nchi yote ya kushi.
14 The name of the third river is Hiddekel. This is the one which flows in front of Assyria. The fourth river is the Euphrates.
Jina la mto wa tatu ni Hidekeli, ambao unatiririka mashariki mwa Ashuru. Mto wa nne ni Frati.
15 The LORD God took the man, and put him into the garden of Eden to cultivate and keep it.
Yahwe Mungu alimtwaa mtu na kumweka ndani ya bustani ya Edeni kuilima na kuitunza.
16 The LORD God commanded the man, saying, “You may freely eat of every tree of the garden;
Yahwe Mungu alimuagiza mtu akisema, “kutoka kwenye kila mti bustanini waweza kula kwa uhuru.
17 but you shall not eat of the tree of the knowledge of good and evil; for in the day that you eat of it, you will surely die.”
Lakini kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa kuwa siku utakayo kula kutoka katika mti huo, utakufa hakika.”
18 The LORD God said, “It is not good for the man to be alone. I will make him a helper comparable to him.”
Kisha Yahwe Mungu akasema, “siyo jambo jema kwamba mtu huyu lazima awe pekeyake. Nitamfanyia msaidizi anaye mfaa.”
19 Out of the ground the LORD God formed every animal of the field, and every bird of the sky, and brought them to the man to see what he would call them. Whatever the man called every living creature became its name.
Kutoka ardhini Yahwe Mungu akafanya kila mnyama wa kondeni na kila ndege wa angani. Kisha akawaleta kwa mtu huyu aone angewapatia majina gani. Jina ambalo mtu huyu alimwita kila kiumbe hai, hili ndilo lilikuwa jina lake.
20 The man gave names to all livestock, and to the birds of the sky, and to every animal of the field; but for man there was not found a helper comparable to him.
Mtu huyu akawapatia majina wanyama wote, ndege wote wa angani, na kila mnyama wa mwitu. Lakini kwa mtu mwenyewe hapakuwa na msaidizi wa kumfaa yeye.
21 The LORD God caused the man to fall into a deep sleep. As the man slept, he took one of his ribs, and closed up the flesh in its place.
Yahwe Mungu akaleta usingizi mzito kwa mtu huyu, kwa hiyo mtu huyu akalala. Yahwe Mungu akatwaa moja ya mbavu za mtu huyu na akapafunika pale alipo chukua ubavu.
22 The LORD God made a woman from the rib which he had taken from the man, and brought her to the man.
Kwa ubavu ambao Yahwe Mungu alichukua toka kwa mtu huyu, akafanya mwanamke na akamleta kwa mtu huyu.
23 The man said, “This is now bone of my bones, and flesh of my flesh. She will be called ‘woman,’ because she was taken out of Man.”
Mwanaume akasema, “kwa sasa, huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu. ataitwa 'mwanamke,' kwa sababu ametwaliwa katika mwanaume.
24 Therefore a man will leave his father and his mother, and will join with his wife, and they will be one flesh.
Kwa hiyo mwanaume atawaacha baba yake na mama yake, ataungamanika na mke wake, na watakuwa mwili mmoja.
25 The man and his wife were both naked, and they were not ashamed.
Wote wawili walikuwa uchi, mwanaume na mke wake, lakini hawakuona aibu.

< Genesis 2 >