< Galatians 5 >
1 Stand firm therefore in the liberty by which Messiah has made us free, and don’t be entangled again with a yoke of bondage.
Ni kwa sababu Kristo alitupa uhuru ili tuwe huru. Hivyo, simameni imara wala msinaswe tena katika kongwa la utumwa.
2 Behold, I, Paul, tell you that if you receive circumcision, Messiah will profit you nothing.
Tazama, Mimi Paulo, ninawaambia kwamba ikiwa mtatahiriwa, Kristo hatawafaidia kwa njia yoyote ile.
3 Yes, I testify again to every man who receives circumcision that he is a debtor to do the whole law.
Tena, namshuhudia kila mwanaume aliyetahiriwa kwamba anapaswa kuwajibika kwa sheria yote.
4 You are alienated from Messiah, you who desire to be justified by the law. You have fallen away from grace.
Mmetengwa mbali na Kristo, wale wote “mnaohesabiwa haki” kwa sheria. Mmeanguka mbali na neema.
5 For we through the Spirit, by faith wait for the hope of righteousness.
Maana kwa njia ya Roho, kwa imani tunasubiri ujasiri wa haki.
6 For in Messiah Yeshua neither circumcision nor uncircumcision amounts to anything, but faith working through love.
Katika Kristo Yesu kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuna maana yoyote. Ni imani pekee inayofanya kazi kupitia upendo ndiyo humaanisha kitu.
7 You were running well! Who interfered with you that you should not obey the truth?
Mlikuwa mnapiga mbio vizuri. Nani aliwazuia kutokuitii kweli?
8 This persuasion is not from him who calls you.
Ushawishi wa kufanya hivyo hautoki kwake yeye anayewaita ninyi.
9 A little yeast grows through the whole lump.
Chachu kidogo huathiri donge zima.
10 I have confidence towards you in the Lord that you will think no other way. But he who troubles you will bear his judgement, whoever he is.
Nina matumaini na ninyi katika Bwana kwamba hamtafikiri kwa njia nyingine yoyote. Yeyote yule atakayewapotosha atabeba hukumu yake yeye mwenyewe, yeyote yule.
11 But I, brothers, if I still proclaim circumcision, why am I still persecuted? Then the stumbling block of the cross has been removed.
Ndugu, kama naendelea kutangaza tohara, kwanini bado ninateswa? Kwa suala hilo kile ambacho ni kizuizi cha msalaba kitaweza kuharibiwa.
12 I wish that those who disturb you would cut themselves off.
Ni matakwa yangu kuwa wale wanaowaongoza vibaya watajihasi wenyewe.
13 For you, brothers, were called for freedom. Only don’t use your freedom as an opportunity for the flesh, but through love be servants to one another.
Mungu amewaiteni ninyi, ndugu, kwenye uhuru. Ila msiutumie uhuru wenu kama fursa kwa mwili. Badala yake kwa upendo mhudumiane ninyi kwa ninyi.
14 For the whole law is fulfilled in one word, in this: “You shall love your neighbour as yourself.”
Kwa kuwa sheria yote imekamilika katika amri moja; nayo ni “Ni lazima umpende jirani yako kama wewe mwenyewe.”
15 But if you bite and devour one another, be careful that you don’t consume one another.
Lakini kama mkiumana na kulana, jiangalieni kwamba msijiharibu ninyi kwa ninyi.
16 But I say, walk by the Spirit, and you won’t fulfil the lust of the flesh.
Nasema, tembeeni kwa roho, na wala hamtazitimiza tamaa za mwili.
17 For the flesh lusts against the Spirit, and the Spirit against the flesh; and these are contrary to one another, that you may not do the things that you desire.
Kwa kuwa mwili una tamaa kubwa dhidi ya Roho, na Roho ina tamaa kubwa dhidi ya mwili. Hizi zinapingana kila moja na nyingine. Matokeo ni kwamba hamfanyi vitu mnavyotamani kuvifanya.
18 But if you are led by the Spirit, you are not under the law.
Lakini kama Roho anawaongoza ninyi, hamko chini ya sheria.
19 Now the deeds of the flesh are obvious, which are: adultery, sexual immorality, uncleanness, lustfulness,
Sasa matendo ya mwili yanaonekana. Nayo ni uasherati, uchafu, ufisadi,
20 idolatry, sorcery, hatred, strife, jealousies, outbursts of anger, rivalries, divisions, heresies,
ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, husuda, kuwaka hasira, ushindani, faraka, mgawanyiko wa madhehebu,
21 envy, murders, drunkenness, orgies, and things like these; of which I forewarn you, even as I also forewarned you, that those who practise such things will not inherit God’s Kingdom.
wivu, ulevi, ulafi na mambo mengine kama haya. Nawaonya ninyi, kama nilivyowaonya mwanzoni, kwamba wale wanaofanya mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu.
22 But the fruit of the Spirit is love, joy, peace, patience, kindness, goodness, faith,
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani,
23 gentleness, and self-control. Against such things there is no law.
upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo.
24 Those who belong to Messiah have crucified the flesh with its passions and lusts.
Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya.
25 If we live by the Spirit, let’s also walk by the Spirit.
Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho.
26 Let’s not become conceited, provoking one another, and envying one another.
Tusiwe wa kujivuna, tusichokozane kila mmoja na mwenzake, wala tusioneane wivu.