< Acts 5 >

1 But a certain man named Hananiah, with Shappirah his wife, sold a possession,
Hivyo, mtu mmoja aliyeitwa Anania, na Safira mkewe, waliuza sehemu ya mali,
2 and kept back part of the price, his wife also being aware of it, then brought a certain part and laid it at the emissaries’ feet.
na akaficha sehemu ya fedha waliyouza (mke wake pia alilijua hili), na akaleta sehemu iliyobakia na kuiweka kwenye miguu ya mitume.
3 But Peter said, “Hananiah, why has Satan filled your heart to lie to the Holy Spirit and to keep back part of the price of the land?
Lakini Petro akasema, “Anania, kwa nini shetani ameujaza moyo wako kusema uongo kwa Roho Mtakatifu na kuficha sehemu ya mali ya shamba?
4 While you kept it, didn’t it remain your own? After it was sold, wasn’t it in your power? How is it that you have conceived this thing in your heart? You haven’t lied to men, but to God.”
Wakati lilipokuwa halijauzwa, halikuwa ni mali yako? Na baada ya kuuzwa, halikuwa chini ya uamuzi wako? Ilikuwaje uwaze jambo hili moyoni mwako? Hujawadanganya wanadamu, bali umemdanganya Mungu.”
5 Hananiah, hearing these words, fell down and died. Great fear came on all who heard these things.
Katika kusikia maneno haya, Anania alidondoka chini na akakata roho. Na hofu kubwa iliwajia wote waliolisikia hili.
6 The young men arose and wrapped him up, and they carried him out and buried him.
Vijana wakaja mbele na kumtia katika sanda, na kumpeleka nje na kumzika.
7 About three hours later, his wife, not knowing what had happened, came in.
Baada ya masaa matatu hivi, mke wake aliingia ndani, asijue ni nini kilichokuwa kimetokea.
8 Peter answered her, “Tell me whether you sold the land for so much.” She said, “Yes, for so much.”
Petro akamwambia, “Niambie, kama mliuza shamba kwa thamani hiyo.” Akasema, “Ndiyo, kwa thamani hiyo.”
9 But Peter asked her, “How is it that you have agreed together to tempt the Spirit of the Lord? Behold, the feet of those who have buried your husband are at the door, and they will carry you out.”
Kisha Petro akamwambia, “Inakuwaje kwamba mmepatana kwa pamoja kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu ya wale waliomzika mme wako iko mlangoni, na watakubeba na kukupeleka nje.”
10 She fell down immediately at his feet and died. The young men came in and found her dead, and they carried her out and buried her by her husband.
Ghafla akadondoka miguuni pa Petro, akakata roho, na wale vijana wakaja ndani wakamkuta ameshakufa. Wakambeba kumpeleka nje, na kumzika karibu na mmewe.
11 Great fear came on the whole assembly, and on all who heard these things.
Hofu kubwa ikaja juu ya kanisa zima, na juu ya wote walioyasikia mambo haya.
12 By the hands of the emissaries many signs and wonders were done amongst the people. They were all with one accord in Solomon’s porch.
Ishara nyingi na maajabu vilikuwa vinatokea miongoni mwa watu kupitia mikono ya mitume. Walikuwa pamoja katika ukumbi wa Sulemani.
13 None of the rest dared to join them; however, the people honoured them.
Lakini, hakuna mtu mwingine tofauti aliyekuwa na ujasiri wa kuambatana nao; hata hivyo, walipewa heshima ya juu na watu.
14 More believers were added to the Lord, multitudes of both men and women.
Na pia, waamini wengi walikuwa wakiongezeka kwa Bwana, idadi kubwa ya wanaume na wanawake,
15 They even carried out the sick into the streets and laid them on cots and mattresses, so that as Peter came by, at least his shadow might overshadow some of them.
kiasi kwamba hata waliwabeba wagonjwa mitaani, na kuwalaza vitandani na kwenye makochi, ili kwamba Petro akiwa anapita, kivuli chake kiweze kushuka juu yao.
16 The multitude also came together from the cities around Jerusalem, bringing sick people and those who were tormented by unclean spirits; and they were all healed.
Hapo pia, idadi kubwa ya watu walikuja kutoka miji iliyozunguka Yerusalem, wakiwaleta wagonjwa na wote waliopagawa na roho wachafu, na wote waliponywa.
17 But the high priest rose up, and all those who were with him (which is the sect of the Sadducees), and they were filled with jealousy
Lakini kuhani mkuu aliinuka, na wote waliokuwa pamoja naye (ambao ni wa dhehebu la masadukayo); na walijawa na wivu
18 and laid hands on the emissaries, then put them in public custody.
wakanyosha mikono yao kuwakamata mitume na kuwaweka ndani ya gereza la jumla.
19 But an angel of the Lord opened the prison doors by night, and brought them out and said,
Na wakati wa usiku malaika wa Bwana akaifungua milango ya gereza na kuwaongoza nje na kusema,
20 “Go stand and speak in the temple to the people all the words of this life.”
“Nendeni, mkasimame hekaluni na kuwaambia watu maneno yote ya Uzima huu.”
21 When they heard this, they entered into the temple about daybreak and taught. But the high priest and those who were with him came and called the council together, with all the senate of the children of Israel, and sent to the prison to have them brought.
Waliposikia hili, waliingia hekaluni wakati wa kupambazuka na kufundisha. Lakini, kuhani mkuu alikuja na wote waliokuwa naye, na kuitisha baraza lote kwa pamoja, na wazee wote wa watu wa Israeli, na kuwatuma gerezani ili kuwaleta mitume.
22 But the officers who came didn’t find them in the prison. They returned and reported,
Lakini watumishi waliokwenda, hawakuwakuta gerezani, walirudi na kutoa taarifa,
23 “We found the prison shut and locked, and the guards standing before the doors, but when we opened them, we found no one inside!”
“Tumekuta gereza limefungwa vizuri salama, na walinzi wamesimama langoni, lakini tulipokuwa tukifungua, hatukuona mtu ndani.”
24 Now when the high priest, the captain of the temple, and the chief priests heard these words, they were very perplexed about them and what might become of this.
Sasa wakati jemedari wa hekalu na makuhani wakuu waliposikia maneno haya, waliingiwa na shaka kubwa kwa ajili yao wakiwaza litakuwaje jambo hili.
25 One came and told them, “Behold, the men whom you put in prison are in the temple, standing and teaching the people.”
Kisha mmoja akaja na kuwaambia, “Watu mliowaweka gerezani wamesimama hekaluni na wanafundisha watu.”
26 Then the captain went with the officers, and brought them without violence, for they were afraid that the people might stone them.
Hivyo jemedari alienda pamoja na watumishi, na wakawaleta, lakini bila ya kufanya vurugu, kwa sababu waliwaogopa watu wangeweza kuwapiga kwa mawe.
27 When they had brought them, they set them before the council. The high priest questioned them,
Walipokwisha kuwaleta, waliwaweka mbele ya baraza. Kuhani mkuu aliwahoji
28 saying, “Didn’t we strictly command you not to teach in this name? Behold, you have filled Jerusalem with your teaching, and intend to bring this man’s blood on us.”
akisema, “Tuliwaamuru msifundishe kwa jina hili, na bado mmeijaza Yerusalemu kwa fundisho lenu, na kutamani kuleta damu ya mtu huyu juu yetu.”
29 But Peter and the emissaries answered, “We must obey God rather than men.
Lakini Petro na mitume wakajibu, “Lazima tumtii Mungu kuliko watu.
30 The God of our fathers raised up Yeshua, whom you killed, hanging him on a tree.
Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, mliyemuua, kwa kumtundika juu ya mti.
31 God exalted him with his right hand to be a Prince and a Saviour, to give repentance to Israel, and remission of sins.
Mungu alimtukuza katika mkono wake wa kuume, na kumfanya kuwa Mkuu na mwokozi, kutoa toba kwa Israeli, na msamaha wa dhambi.
32 We are his witnesses of these things; and so also is the Holy Spirit, whom God has given to those who obey him.”
Sisi ni mashahidi wa mambo haya, na Roho Mtakatifu, ambaye Mungu amemtoa kwa wale wanaomtii.”
33 But they, when they heard this, were cut to the heart, and were determined to kill them.
Wajumbe wa baraza waliposikia hivi, walishikwa na hasira wakataka kuwaua mitume.
34 But one stood up in the council, a Pharisee named Gamaliel, a teacher of the Torah, honoured by all the people, and commanded to put the emissaries out for a little while.
Lakini pharisayo aliyeitwa Gamalieli, mwalimu wa sheria, aliyeheshimiwa na watu wote, alisimama na kuwaamuru mitume wachukuliwe nje kwa muda mfupi.
35 He said to them, “You men of Israel, be careful concerning these men, what you are about to do.
Kisha akawaambia, “Wanaume wa Israeli, iweni makini sana na kile mnachopendekeza kuwafanyia watu hawa.
36 For before these days Todah rose up, making himself out to be somebody; to whom a number of men, about four hundred, joined themselves. He was slain; and all, as many as obeyed him, were dispersed and came to nothing.
Kwa sababu, zamani zilizopita, Theuda aliinuka na kujidai kuwa mtu mkuu, na idadi ya watu, wapata mia nne walimfuata. Aliuawa, na wote waliokuwa wanamtii walitawanyika na kupotea.
37 After this man, Judah of Galilee rose up in the days of the enrolment, and drew away some people after him. He also perished, and all, as many as obeyed him, were scattered abroad.
Baada ya mtu huyu, Yuda mgalilaya, aliinuka siku zile za kuandikwa sensa, akavuta watu wengi nyuma yake. Naye pia alipotea na wote waliokuwa wakimtii walitawanyika.
38 Now I tell you, withdraw from these men and leave them alone. For if this counsel or this work is of men, it will be overthrown.
Sasa nawaambia, jiepusheni na watu hawa na muwaache wenyewe, kwa sababu, kama mpango huu au kazi hii ni ya watu itatupwa.
39 But if it is of God, you will not be able to overthrow it, and you would be found even to be fighting against God!”
Lakini kama ni ya Mungu, hamtaweza kuwazuia; mnaweza mkajikuta hata mnashindana na Mungu.” Hivyo, walishawishika na maneno yake.
40 They agreed with him. Summoning the emissaries, they beat them and commanded them not to speak in the name of Yeshua, and let them go.
Kisha, waliwaita mitume ndani na kuwachapa na kuwaamuru wasinene kwa jina la Yesu, na wakawaacha waende zao.
41 They therefore departed from the presence of the council, rejoicing that they were counted worthy to suffer dishonour for Yeshua’s name.
Waliondoka mbele ya baraza wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuteseka na kutoheshimiwa kwa ajili ya Jina hilo.
42 Every day, in the temple and at home, they never stopped teaching and proclaiming Yeshua, the Messiah.
Kwa hiyo, kila siku, ndani ya hekalu na kutoka nyumba hadi nyumba waliendelea kufundisha na kuhubiri Yesu kuwa ni Masihi.

< Acts 5 >