< Song of Solomon 1 >

1 The Song of songs, which is Solomon’s.
Wimbo ulio bora wa Solomoni.
2 Let him kiss me with the kisses of his mouth; for your love is better than wine.
Unibusu kwa busu la kinywa chako, kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai.
3 Your oils have a pleasing fragrance. Your name is oil poured out, therefore the virgins love you.
Manukato yako yananukia vizuri, jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa. Ndiyo sababu wanawali wanakupenda!
4 Take me away with you. Let’s hurry. The king has brought me into his rooms. Friends We will be glad and rejoice in you. We will praise your love more than wine! Beloved They are right to love you.
Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Marafiki Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Mpendwa Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!
5 I am dark, but lovely, you daughters of Jerusalem, like Kedar’s tents, like Solomon’s curtains.
Mimi ni mweusi, lakini napendeza, enyi binti za Yerusalemu, mweusi kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya hema la Solomoni.
6 Don’t stare at me because I am dark, because the sun has scorched me. My mother’s sons were angry with me. They made me keeper of the vineyards. I haven’t kept my own vineyard.
Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. Wana wa mama yangu walinikasirikia na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu. Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha.
7 Tell me, you whom my soul loves, where you graze your flock, where you rest them at noon; for why should I be as one who is veiled beside the flocks of your companions?
Niambie, wewe ambaye ninakupenda, unalisha wapi kundi lako la kondoo na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri. Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela karibu na makundi ya rafiki zako?
8 If you don’t know, most beautiful among women, follow the tracks of the sheep. Graze your young goats beside the shepherds’ tents.
Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote, fuata nyayo za kondoo, na kulisha wana-mbuzi wako karibu na hema za wachungaji.
9 I have compared you, my love, to a steed in Pharaoh’s chariots.
Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao.
10 Your cheeks are beautiful with earrings, your neck with strings of jewels.
Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli, shingo yako ikiwa na mikufu ya vito.
11 We will make you earrings of gold, with studs of silver.
Tutakufanyia vipuli vya dhahabu, vyenye kupambwa kwa fedha.
12 While the king sat at his table, my perfume spread its fragrance.
Wakati mfalme alipokuwa mezani pake, manukato yangu yalisambaza harufu yake nzuri.
13 My beloved is to me a sachet of myrrh, that lies between my breasts.
Mpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha manemane kati ya matiti yangu.
14 My beloved is to me a cluster of henna blossoms from the vineyards of En Gedi.
Mpenzi wangu kwangu mimi ni kama kishada cha maua ya mhina kutoka mashamba ya mizabibu ya En-Gedi.
15 Behold, you are beautiful, my love. Behold, you are beautiful. Your eyes are like doves.
Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Tazama jinsi ulivyo mzuri! Macho yako ni kama ya hua.
16 Behold, you are beautiful, my beloved, yes, pleasant; and our couch is verdant.
Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Ee, tazama jinsi unavyopendeza! Na kitanda chetu ni cha majani mazuri.
17 The beams of our house are cedars. Our rafters are firs.
Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, na mapao yetu ni miberoshi.

< Song of Solomon 1 >