< 1 Chronicles 15 >
1 David made himself houses in David’s city; and he prepared a place for God’s ark, and pitched a tent for it.
Baada ya Daudi kujijengea nyumba zake katika Mji wa Daudi, akatengeneza sehemu kwa ajili ya Sanduku la Mungu, kisha akasimamisha hema kwa ajili yake.
2 Then David said, “No one ought to carry God’s ark but the Levites. For Yahweh has chosen them to carry God’s ark, and to minister to him forever.”
Kisha Daudi akasema, “Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kulibeba Sanduku la Mungu isipokuwa Walawi peke yao, kwa sababu Bwana aliwachagua kulibeba Sanduku la Bwana na kuhudumu mbele zake milele.”
3 David assembled all Israel at Jerusalem, to bring up Yahweh’s ark to its place, which he had prepared for it.
Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu ili kulipandisha Sanduku la Bwana na kulileta hadi kwenye sehemu aliyokuwa ametengeneza kwa ajili yake.
4 David gathered together the sons of Aaron and the Levites:
Kisha Daudi akawakusanya pamoja wazao wa Aroni na Walawi:
5 of the sons of Kohath, Uriel the chief, and his brothers one hundred twenty;
Kutoka wazao wa Kohathi, Urieli kiongozi na ndugu zake 120,
6 of the sons of Merari, Asaiah the chief, and his brothers two hundred twenty;
Kutoka wazao wa Merari, Asaya kiongozi na ndugu zake 220.
7 of the sons of Gershom, Joel the chief, and his brothers one hundred thirty;
Kutoka wazao wa Gershoni, Yoeli kiongozi na ndugu zake 130.
8 of the sons of Elizaphan, Shemaiah the chief, and his brothers two hundred;
Kutoka wazao wa Elisafani, Shemaya kiongozi na ndugu zake 200.
9 of the sons of Hebron, Eliel the chief, and his brothers eighty;
Kutoka wazao wa Hebroni, Elieli kiongozi na ndugu zake 80.
10 of the sons of Uzziel, Amminadab the chief, and his brothers one hundred twelve.
Kutoka wazao wa Uzieli, Aminadabu kiongozi na ndugu zake 112.
11 David called for Zadok and Abiathar the priests, and for the Levites: for Uriel, Asaiah, Joel, Shemaiah, Eliel, and Amminadab,
Kisha Daudi akawaita makuhani Sadoki na Abiathari, pamoja na Walawi Urieli, Asaya, Yoeli, Shemaya, Elieli na Aminadabu.
12 and said to them, “You are the heads of the fathers’ households of the Levites. Sanctify yourselves, both you and your brothers, that you may bring the ark of Yahweh, the God of Israel, up to the place that I have prepared for it.
Akawaambia, “Ninyi ndio viongozi wa jamaa za Walawi. Ninyi pamoja na Walawi wenzenu inawapasa mjitakase na kulipandisha Sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli hadi mahali ambapo nimetengeneza kwa ajili yake.
13 For because you didn’t carry it at first, Yahweh our God broke out in anger against us, because we didn’t seek him according to the ordinance.”
Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku la Bwana mara ya kwanza, hata ikasababisha Bwana Mungu wetu kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumuuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.”
14 So the priests and the Levites sanctified themselves to bring up the ark of Yahweh, the God of Israel.
Kwa hiyo makuhani pamoja na Walawi wakajitakasa ili kulipandisha Sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli.
15 The children of the Levites bore God’s ark on their shoulders with its poles, as Moses commanded according to Yahweh’s word.
Nao Walawi wakalichukua Sanduku la Mungu mabegani mwao wakitumia mipiko, kama vile Mose alivyoamuru sawasawa na neno la Bwana.
16 David spoke to the chief of the Levites to appoint their brothers as singers with instruments of music, stringed instruments, harps, and cymbals, sounding aloud and lifting up their voices with joy.
Daudi akawaambia viongozi wa Walawi kuwaweka ndugu zao waimbaji ili waimbe nyimbo za shangwe, wakiwa na vyombo vya uimbaji: zeze, vinubi na matoazi.
17 So the Levites appointed Heman the son of Joel; and of his brothers, Asaph the son of Berechiah; and of the sons of Merari their brothers, Ethan the son of Kushaiah;
Basi Walawi wakawaweka Hemani mwana wa Yoeli; kutoka miongoni mwa ndugu zake, Asafu mwana wa Berekia; kutoka miongoni mwa ndugu zao Wamerari, Ethani mwana wa Kushaiya;
18 and with them their brothers of the second rank: Zechariah, Ben, Jaaziel, Shemiramoth, Jehiel, Unni, Eliab, Benaiah, Maaseiah, Mattithiah, Eliphelehu, Mikneiah, Obed-Edom, and Jeiel, the doorkeepers.
hawa ndio waliochaguliwa kuwa wasaidizi wao: Zekaria, Yaazieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Benaya, Maaseya, Matithia, Elifelehu, Mikneya, pamoja na mabawabu Obed-Edomu na Yehieli.
19 So the singers, Heman, Asaph, and Ethan, were given cymbals of bronze to sound aloud;
Waimbaji Hemani, Asafu na Ethani walichaguliwa kupiga matoazi ya shaba;
20 and Zechariah, Aziel, Shemiramoth, Jehiel, Unni, Eliab, Maaseiah, and Benaiah, with stringed instruments set to Alamoth;
Zekaria, Azieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Maaseya na Benaya walikuwa wapiga zeze kufuatana na sauti ya alamothi,
21 and Mattithiah, Eliphelehu, Mikneiah, Obed-Edom, Jeiel, and Azaziah, with harps tuned to the eight-stringed lyre, to lead.
na Matithia, Elifelehu, Mikneya, Obed-Edomu, Yehieli na Azazia walikuwa wapiga vinubi, wakiongozwa kwa kufuata sauti ya sheminithi.
22 Chenaniah, chief of the Levites, was over the singing. He taught the singers, because he was skillful.
Kenania kiongozi wa Walawi alikuwa msimamizi wa uimbaji; huu ndio uliokuwa wajibu wake kwa sababu alikuwa stadi katika hilo.
23 Berechiah and Elkanah were doorkeepers for the ark.
Berekia na Elikana walikuwa mabawabu kwa ajili ya Sanduku.
24 Shebaniah, Joshaphat, Nethanel, Amasai, Zechariah, Benaiah, and Eliezer, the priests, blew the trumpets before God’s ark; and Obed-Edom and Jehiah were doorkeepers for the ark.
Shebania, Yoshafati, Nethaneli, Amasai, Zekaria, Benaya na Eliezeri, makuhani, walikuwa wapiga tarumbeta mbele ya Sanduku la Mungu. Obed-Edomu na Yehiya waliwekwa pia kuwa mabawabu wa Sanduku.
25 So David, the elders of Israel, and the captains over thousands went to bring the ark of Yahweh’s covenant up out of the house of Obed-Edom with joy.
Basi Daudi pamoja na wazee wa Israeli na majemadari wa vikosi vya elfu wakaenda ili kulipandisha Sanduku la Agano la Bwana kutoka nyumba ya Obed-Edomu kwa shangwe.
26 When God helped the Levites who bore the ark of Yahweh’s covenant, they sacrificed seven bulls and seven rams.
Kwa sababu Mungu alikuwa amewasaidia Walawi waliokuwa wanalichukua Sanduku la Agano la Bwana, mafahali saba na kondoo dume saba walitolewa dhabihu.
27 David was clothed with a robe of fine linen, as were all the Levites who bore the ark, the singers, and Chenaniah the choir master with the singers; and David had an ephod of linen on him.
Basi Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, kama walivyokuwa wamevaa Walawi wote waliokuwa wanalichukua lile Sanduku, waimbaji nao walivaa vivyo hivyo, pamoja na Kenania aliyekuwa anaongoza nyimbo za waimbaji. Daudi alivaa pia kisibau cha kitani safi.
28 Thus all Israel brought the ark of Yahweh’s covenant up with shouting, with sound of the cornet, with trumpets, and with cymbals, sounding aloud with stringed instruments and harps.
Hivyo Israeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano la Bwana kwa shangwe, wakipiga pembe za kondoo dume, tarumbeta, matoazi, wakipiga zeze na vinubi.
29 As the ark of Yahweh’s covenant came to David’s city, Michal the daughter of Saul looked out at the window, and saw king David dancing and playing; and she despised him in her heart.
Sanduku la Agano la Bwana lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea, akamdharau moyoni mwake.