< Acts 3 >

1 One day Peter and John were going up to the Temple for the hour of prayer--the ninth hour--and, just then,
Siku moja, saa tisa alasiri, Petro na Yohane walikuwa wanakwenda Hekaluni, wakati wa sala.
2 some men were carrying there one who had been lame from birth, whom they were wont to place every day close to the Beautiful Gate (as it was called) of the Temple, for him to beg from the people as they went in.
Na pale karibu na mlango wa Hekalu uitwao “Mlango Mzuri”, palikuwa na mtu mmoja, kiwete tangu kuzaliwa. Watu walimbeba huyo mtu kila siku na kumweka hapo ili aombe chochote kwa wale waliokuwa wakiingia Hekaluni.
3 Seeing Peter and John about to go into the Temple, he asked them for alms.
Alipowaona Petro na Yohane wakiingia Hekaluni, aliwaomba wampe chochote.
4 Peter fixing his eyes on him, as John did also, said, "Look at us."
Petro na Yohane walimkodolea macho, naye Petro akamwambia, “Tutazame!”
5 So he looked and waited, expecting to receive something from them.
Naye akawageukia, akitazamia kupata kitu kutoka kwao.
6 "I have no silver or gold," Peter said, "but what I have, I give you. In the name of Jesus Christ, the Nazarene-- walk!"
Kisha Petro akamwambia, “Sina fedha wala dhahabu lakini kile nilicho nacho nitakupa. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, tembea!”
7 Then taking his hand Peter lifted him up, and immediately his feet and ankles were strengthened.
Halafu, akamshika mkono wa kulia, akamwinua. Papo hapo miguu na magoti yake yakapata nguvu.
8 Leaping up, he stood upright and began to walk, and went into the Temple with them, walking, leaping, and praising God.
Akaruka, akasimama na kuanza kutembea. Halafu akaingia pamoja nao Hekaluni, akitembea na kurukaruka huku akimtukuza Mungu.
9 All the people saw him walking and praising God;
Watu wote waliokuwa hapo walimwona akitembea na kumsifu Mungu.
10 and recognizing him as the man who used to sit at the Beautiful Gate of the Temple asking for alms, they were filled with awe and amazement at what had happened to him.
Walipomtambua kuwa ndiye yule aliyekuwa anaombaomba karibu na ule “Mlango Mzuri” wa Hekalu, wakashangaa mno hata wasiweze kuelewa yaliyompata.
11 While he still clung to Peter and John, the people, awe-struck, ran up crowding round them in what was known as Solomon's Portico.
Watu wote, wakiwa na mshangao mkubwa wakaanza kukimbilia mahali palipoitwa “Ukumbi wa Solomoni,” ambapo yule mtu alikuwa bado anaandamana na Petro na Yohane.
12 Peter, seeing this, spoke to the people. "Israelites," he said, "why do you wonder at this man? Or why gaze at us, as though by any power or piety of our own we had enabled him to walk?
Basi, Petro alipowaona watu hao akawaambia, “Wananchi wa Israeli, kwa nini mnashangazwa na jambo hili? Mbona mnatukodolea macho kana kwamba ni kwa nguvu zetu au utakatifu wetu sisi wenyewe tumemfanya mtu huyu aweze kutembea?
13 The God of Abraham, Isaac, and Jacob, the God of our forefathers, has conferred this honour on His Servant Jesus, whom you delivered up and disowned in the presence of Pilate, when he had decided to let Him go.
Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, Mungu wa baba zetu amemtukuza Yesu mtumishi wake. Yeye ndiye yuleyule mliyemtia mikononi mwa wakuu na kumkataa mbele ya Pilato hata baada ya Pilato kuamua kumwacha huru.
14 Yes, you disowned the holy and righteous One, and asked as a favour the release of a murderer.
Alikuwa mtakatifu na mwema; lakini ninyi mlimkataa, mkataka mtu mwingine aliyekuwa muuaji afunguliwe.
15 The Prince of Life you put to death; but God has raised Him from the dead, and we are witnesses as to that.
Basi, mlimuua yule ambaye ni chanzo cha uzima. Lakini Mungu alimfufua, na sisi ni mashahidi wa tukio hilo.
16 It is His name-- faith in that name being the condition--which has strengthened this man whom you behold and know; and the faith which He has given has made this man sound and strong again, as you can all see.
Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote.
17 "And now, brethren, I know that it was in ignorance that you did it, as was the case with your rulers also.
“Sasa ndugu zangu, nafahamu kwamba ninyi na wakuu wenu mlitenda hayo kwa sababu ya kutojua kwenu.
18 But in this way God has fulfilled the declarations He made through all the Prophets, that His Christ would suffer.
Lakini ndivyo Mungu alivyotimiza yale aliyotangaza zamani kwa njia ya manabii wote, kwamba ilikuwa lazima Kristo wake ateseke.
19 Repent, therefore, and reform your lives, so that the record of your sins may be cancelled, and that there may come seasons of revival from the Lord,
Basi, tubuni mkamrudie Mungu ili afute dhambi zenu.
20 and that He may send the Christ appointed beforehand for you--even Jesus.
Fanyeni hivyo ili Bwana awape nyakati za kuburudika rohoni na kuwaletea yule Kristo aliyemteua ambaye ndiye Yesu.
21 Heaven must receive Him until those times of which God has spoken from the earliest ages through the lips of His holy Prophets--the times of the reconstitution of all things. (aiōn g165)
Ni lazima yeye abaki huko mbinguni mpaka utakapofika wakati wa kurekebishwa vitu vyote, kama Mungu alivyosema kwa njia ya manabii wake watakatifu wa tangu zamani. (aiōn g165)
22 Moses declared, "'The Lord your God will raise up a Prophet for you from among your brethren as He has raised me. In all that He says to you, you must listen to Him.
Kwa maana Mose alisema, Bwana Mungu wenu atawapelekeeni nabii kama mimi kutoka kati yenu ninyi wenyewe.
23 And every one, without exception, who refuses to listen to that Prophet shall be utterly destroyed from among the People.'
Yeyote yule ambaye hatamsikiliza nabii huyo atatengwa mbali na watu wa Mungu na kuangamizwa.
24 Yes, and all the Prophets, from Samuel onwards--all who have spoken--have also announced the coming of this present time.
Manabii wote, kuanzia Samweli na wale waliomfuata, walitangaza habari za mambo haya ambayo yamekuwa yakitendeka siku hizi.
25 "You are the heirs of the Prophets, and of the Covenant which God made with your forefathers when He said to Abraham, 'And through your posterity all the families of the world shall be blessed.'
Ahadi zile Mungu alizotoa kwa njia ya manabii ni kwa ajili yenu; na mnashiriki lile agano Mungu alilofanya na babu zenu, kama alivyomwambia Abrahamu: Kwa njia ya wazawa wako, jamaa zote za dunia zitabarikiwa.
26 It is to you first that God, after raising His Servant from the grave, has sent Him to bless you, by causing every one of you to turn from your wickedness."
Basi, ilikuwa kwa ajili yenu kwanza kwamba Mungu alimfufua mtumishi wake, alimtuma awabariki kwa kumfanya kila mmoja wenu aachane kabisa na maovu yake.”

< Acts 3 >